Kabembe
JF-Expert Member
- Feb 11, 2009
- 2,588
- 1,793
Hili jambo limenistua sana,jana nimeoneshwa ujumbe wa simu wa kuhamasisha na kuhimiza wafanyakazi wa NSSF na marafiki zao kuchangishana pesa hili Dr Dau asomewe dua,kwakweli Mwalimu Nyerere aliona mbali sana pale alipoamua kutuunganisha Watanzania bila kujali makabila na dini zetu.Najiuliza,hivi wakristo wangapi wamatumbuliwa na wala hakuna mtu anaangaika nao wala kuwaonea huruma zaidi ya ndugu na jamaa zao?! Mbona kipindi cha Kikwete tumeshuhudia wakristo wengi wakipelekwa kwa Pilato pale kisutu kwa tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka na wengine kufungwa na hatukusikia Wakristo wakilalama?! Kama hali ndio hii,basi hili taifa tunallpeleka pabaya zaidi.Mtu kala hela ya umma unamwombea dua ya nini? Dua unamwombea kwa Mungu yupi?