Harmonize huna kipya cha kuwapa mashabiki, umeshakuwa mzigo jifunze kwa wenzio

mi siona tatzo kwa hamo kuwa anafanya hivo ulivyozungumza na bado anatoboa vibaya ingekua anaendelea kudidimia katka game yan ngoma zake hazipgwi mtaa wala stations mbali mbali hapo ndipo ningeona hoja yako inamashiko
 
Kwa hiyo na jay z alianzisha lebo kuua vpaji au msanii mwenye lebo ni domo tu dunia nzima?
Kila mtu ana mikakati yake ya kufanikiwa kimaisha. Mwingine anataka kufanikiwa kwa kuzima au kupunguza washindani
 
Wasalaam wanajamvi.
Mimi ni mmoja wa mashabiki wa Harmonize na toka anatoa wimbo wa kwanza kwakweli alionesha ni wazi ana kipaji cha ajabu sana pamoja na kusikika kama Diamond,Mimi ni mmoja wa watu walioamini pengine Harmonize ana kipya cha kutupa mashabiki lakini ukweli ulio wazi Harmonize amechoka na hana kipya cha kuwapa mashabiki na wala habadiliki kabisa ukilinganisha na wenzie wakina Rich Mavoko na Ray vany...

Wakatia ametoa wimbo wa kwanza na wapili Mimi niliamini kabisa Harmonize angebadilika kila leo na kila siku hasa kwenye uimbaji au tungo zake lakini kwangu mimi sioni kipya bali naona mtu ambaye ameshakuwa mzigo kabisa ndani ya WCB na kibaya zaidi kuimba kama Diamond ndio kunazidi kumponza zaidi na zaidi na wala hana mpango wakubadilika kabisa......

Kibaya zaidi ni kwamba yeye pekee ndio anaonekana bado ana uwezo mdogo kabisa na muda mwingine huwa nafikiri pengine Diamond anaona kabisa alikosea kumsign WCB maana ni wazi kabisa amekosa kipya kabisa cha kuwapa mashabiki zaidi ya kuwakumbusha sauti ya Diamond...
hata kwenye wimbo alio imba na Rich mavoko(show me) kwakweli niliyekuwa namsikia ni Diamond na Rich mavoko...

Pia huwa najiuliza ni kweli Harmonize hana cha kujifunza kwa wenzie?Haoni kuwa hana kipya cha kuwapa mashabiki zaidi ya kuwakumbusha sauti ya Diamond jambo ambalo linakera sana tena sana.... Hawaoni wenzie kila wimbo wana uwezo wakuja tofauti na kubadilika?

Karibuni wana jamvi
Wewe ni nini ulichowahi kufanya cha maana zaidi ya kujipendekeza kwa Ma-CCM?

Huyo dogo unayemkandia hapa nadhani ana maendeleo makubwa kimaisha kuliko wewe.
 
hiyo ni kawaida kumbuka Loon na Mase wakati wako chini ya bad boys walikuwa wakirap kama pdidy kabisa ,hata watangazaji wengi hutangaza sauti ya role model wao
 
Back
Top Bottom