Harmonize huna kipya cha kuwapa mashabiki, umeshakuwa mzigo jifunze kwa wenzio

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,843
43,312
Wasalaam wanajamvi.
Mimi ni mmoja wa mashabiki wa Harmonize na toka anatoa wimbo wa kwanza kwakweli alionesha ni wazi ana kipaji cha ajabu sana pamoja na kusikika kama Diamond,Mimi ni mmoja wa watu walioamini pengine Harmonize ana kipya cha kutupa mashabiki lakini ukweli ulio wazi Harmonize amechoka na hana kipya cha kuwapa mashabiki na wala habadiliki kabisa ukilinganisha na wenzie wakina Rich Mavoko na Ray vany...

Wakatia ametoa wimbo wa kwanza na wapili Mimi niliamini kabisa Harmonize angebadilika kila leo na kila siku hasa kwenye uimbaji au tungo zake lakini kwangu mimi sioni kipya bali naona mtu ambaye ameshakuwa mzigo kabisa ndani ya WCB na kibaya zaidi kuimba kama Diamond ndio kunazidi kumponza zaidi na zaidi na wala hana mpango wakubadilika kabisa......

Kibaya zaidi ni kwamba yeye pekee ndio anaonekana bado ana uwezo mdogo kabisa na muda mwingine huwa nafikiri pengine Diamond anaona kabisa alikosea kumsign WCB maana ni wazi kabisa amekosa kipya kabisa cha kuwapa mashabiki zaidi ya kuwakumbusha sauti ya Diamond...
hata kwenye wimbo alio imba na Rich mavoko(show me) kwakweli niliyekuwa namsikia ni Diamond na Rich mavoko...

Pia huwa najiuliza ni kweli Harmonize hana cha kujifunza kwa wenzie?Haoni kuwa hana kipya cha kuwapa mashabiki zaidi ya kuwakumbusha sauti ya Diamond jambo ambalo linakera sana tena sana.... Hawaoni wenzie kila wimbo wana uwezo wakuja tofauti na kubadilika?

Karibuni wana jamvi
 
Jamaa ana uwezo mkubwa ila kama humuelewi achana naye. Ukitaka kujua nguvu ya Harmonize muulize Dully Sykes - angekuwa hana impact tusingehangaika hata kumjadili hapa
 
Jamaa ana uwezo mkubwa ila kama humuelewi achana naye. Ukitaka kujua nguvu ya Harmonize muulize Dully Sykes - angekuwa hana impact tusingehangaika hata kumjadili hapa
ile ilikuwa ni nguvu ya sauti ya Diamond na mikogo ya diamond na si Harmonize.
 
ile ilikuwa ni nguvu ya sauti ya Diamond na mikogo ya diamond na si Harmonize.
As long as it makes money hakuna tatizo, tangu aanze kuimba wanasema anafanana sauti na Diamond, lakini kajizolea umaarufu, nguvu, pesa, mashabiki mpaka na ma role models wanaojiboost kupitia jina lake - anataka nini tena ?
 
Back
Top Bottom