Je, bado Kajala Masanja anafaa kuwa Manager wa Harmonize? Jembe ni Jembe unaweza okoa jahazi

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,151
1,489
Hakuna ubishi Msanii Harmonize au kama anavyojiita Konde boy ni msanii mkubwa si kwa Tanzania tu pamoja na mataifa yote ya Afrika. Ukichukua wasanii 3 Wakubwa na bora Tanzania basi bila shaka Harmonize atakwepo, ukichukua Wasanii 20 Wakubwa na bora Afrika Konde boy atakwepo.

Harmonize ni msanii mwenye kipaji kikubwa saaana, ni msanii anayejituma pia. Harmonize anafanya harakati zake za music kupitia Kampuni/lebo yake ya Konde Gang.

Kwa msanii kipaji na kujituma ni kitu kimoja, lakini kwa Msanii anayetaka kufika level za dunia MANAGEMENT ni kila kitu, a strong management ndio inayomfanya msanii afike mbali, abaki kwenye tasnia kwa muda mrefu, apate endorsement kubwa, aweze kushirikiana na wasanii wakubwa Duniani e.t.c

Dada yetu Kajala Masanja, Ni msanii mkongwe kwenye kiwanda cha maigizo( bongo movie), je ana uwezo, connection, ujanja, ubunifu, elimu (japo sio lazima ila ni muhimu), nia, exposure e.t.c ya kuhakikisha kipaji cha Harmonize kinaendelezwa na kufika mbali zaidi ya hapa?

Natambua pale Konde gang kuna Jembe ni Jembe, Jembe ni mtu makini, mwelewa , sina shaka na connection zake, exposure kubwa, Msomi, anajua figisu za kiwanda cha muziki lakini kinachonipa shaka kuna Manager mwingine ambaye pia ni mchumba wa msanii na anaweza kuwa na nguvu za kusikilizwa na maamuzi kuliko Jembe.

Watanzania wote wamekuwa wakimtazama Harmonize kwa kumlinganisha na Diamond. Lebo ya Diamond inaweza kuwa lebo yenye mafanikio makubwa si Tanzanai tu bali Afrika nzima. Kwa mtazamo huu si vibaya Konde gang wakaiga namna campuni zinavyoendeshwa, Diamond linapokuja suala la campuni na wanamusic wake Wachumba zake wote aliyowahi kuwa nao hakuna aliyewahi kupewa nafasi ya Manager licha ya wengine kuwa na exposure na sifa za kuweza kuwa Manager.

No hate, ni mtazamo tu ambao pia unaweza kuwa sio sahihi, hiki kinachoendelea Konde gang kwa Wasanii kuondoka ( hata kama wanaondoka kwa amani) si jambo jema kwa future ya Harmonize na lebo yake, lakini waungwana watauliza kwanini waondoke sasa wakati wa Mchumba kuwa Manager? Yawezekana Manager akisema huyu aondoke basi Harmonize hana budi kuvunja Mkataba.

Jembe my brother, uwezo wako mkubwa saana kwenye industry hii, ili Tanzania ifike mbali inahitaji lebo nyingi zaidi ya WCB, uwezo wako ni level ai zaidi ya Manager Salam, naamini unaweza kuipeleka Konde kimataifa zaidi, hujawahi Kufeli na hutafeli lakini mwambie mdogo wako dada yetu abaki kuwa Mke.

Jembe na Harmonize, kipindi hiki wapinzani wenu watatumia vijana wenu mlio wakuza nakuwekeza fedha kuwachafua, lakini naamini mko imara .

Jembe na Harmonize, Watanzania tunajua mna deni kwa dada yetu Angela, MLIMUAHIDI KUMSAIDIA MATIBABU YA MGUU WAKE NJE YA TANZANIA, MUNGU ATAWABARIKI SANA MKILITIMIZA HILI LICHA YA KUWA ANGELA HAYUKO MIKONONI MWENU KWA SASA.

Najua mmemalizana kwa amani na dada yetu Angela anaenda kutafuta maisha sehemu nyingine( huyu dada asitumiwe nawapinzani wa Konde kama mtu anataka kumsaidia amsaidie kwa nia ya kuendeleza kipaji chake).

Mungu ibariki Tanzania

Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
 
Label imevunjika sababu ya UBINAFSI kila siku anatoa nyimbo yeye hana muda wa kupromote kazi za wasanii wake, anatoa nyinmbo hovyo hovyo hazipi nafasi nyimbo za wasanii wake.

Mondi anawatoa wasanii wake anaweza kukaa zaidi ya nusu mwaka hatoi nyimbo ili tu apate muda wa kumfanyia promo msanii wake na resources zote za WCB zinamtizama msanii mmoja na ndio maana wasanii wake wanafanya vizuri.

Kajala anasingiziwa tu ,KONDE ni mbinafsi kwenye label yake anataka kuonekana yy. Sasa hivi nikikwambia nitajie jina ya EP waizotoa Cheed na Killy ndani ya dk tatu hujui mpaka ugoogle nikikwambia unitajie album ya Killy aliyo itoa mwanzoni mwa mwaka huu ndani ya dk tatu huijui, nikikuuliza Ibraah ana album ngapi hujui.

Killy na Ibraah wameachia album mwaka huu sizani hata majina yake unayajua, kutwa yy anaachia nyimbo, yaani wasanii wake walikuwa wanaenda kibahati bahati.

Halafu hizo takwimu zako kazirudie tena,ukitaja wanamziki hata hamsini bora wa Afrika Konde hayupo, pamoja na kutoa nyimbo na album mfululizo bado kwenye platform anakimbizwa na akina Zuchu na Vannyboy, Mario nae mda si mrefu akiachia album yake atampiga gap kwenye Digital platforms zote.

Ukitaka Konde asonge yeye na label yake.
1.Aache ubinafsi awape nafasi wasanii wake (Japo kabakia Ibraah tuu).
2.Atoe nyimbo kimpangilio na kwa Target na si kutoa ili mradi.
3.Amwache Jembe adominate kwenye swala la Management.

Akileta usela bange hata yeye mwenyewe anaweza kujitoa kwenye label yake ya Kondegang.
 
Label imevunjika sababu ya UBINAFSI kila siku anatoa nyimbo yeye hana muda wa kupromote kazi za wasanii wake, anatoa nyinmbo hovyo hovyo hazipi nafasi nyimbo za wasanii wake.
Uko sahihi kamba0719 kuhusu Diamond kuwapush wanamusic wake, lakini yote hiyo inaweza kuwa ni matokeo ya strong management, lakini kuhusu ukubwa wa mwanamusic hatumpimi kwenye digital platform pekee, takwimu zangu ziko sahihi mkuu, Harmonize bado ni msanii mkubwa tena top 3 kwa Tanzania, Zuchu and rest bado saaana kumfikia Harmonize.

Yes naiona dalili ya kuwa kama Harmonize asipotenganisha mapenz na kazi hata Jembe ni Jembe hatataka kuwa sehemu ya watu waliomkwamisha lazima utaondoka tu
 
Zuchu amfikie mara ngapi, wewe unazani hawa MTV Base/Trace wakitoa list ya wasanii wakubwa moja ya source yao kubwa ni Digital platforms, dogo sasa kawa Nominated na tuzo za MTV Europe ktk wasanii watano waliofanya vizuri Africa nae yumo.

Huyo Rayvanny ndio kabisa ameachieve vitu vikubwa ambavyo Diamond na ukubwa wake hajawahi, tuzo ya BET, kupiga show kwenye majukwa makubwa Latin America huo bila kusahau kufanya show pamoja na Maluma kwenye jukwaa la MTV EMA mwaka jana. Ukubwa haupimwi kwa hisia bali kwa vitu vinavyo onekana.

Jembe ni Jembe kuondoka Konde pale bila taratibu ugomvi wake utakuwa mkubwa sana, sababu Jembe amewekeza kwenye label na kwa Harmonize mwenyewe kwa hiyo timbwili lake litakuwa kubwa sana, Jembe kwanza msomi, Industry ya bongo anaijua tokea mwanzo wale na pili ni mtoto wa mjini.
 
Wasanii 20 Wakubwa na bora Afrika Konde boy atakwepo.
Are you serious ?

20221102_183510.jpg
 
Zuchu amfikie mara ngapi, wewe unazani hawa MTV Base/Trace wakitoa list ya wasanii wakubwa moja ya source yao kubwa ni Digital platforms, dogo sasa kawa Nominated na tuzo za MTV Europe ktk wasanii watano waliofanya vizuri Africa nae yumo.

Huyo Rayvanny ndio kabisa ameachieve vitu vikubwa ambavyo Diamond na ukubwa wake hajawahi, tuzo ya BET,kupiga show kwenye majukwa makubwa Latin America huo bila kusahau kufanya show pamoja na Maluma kwenye jukwaa la MTV EMA mwaka jana .Ukubwa haupimwi kwa hisia bali kwa vitu vinavyo onekana.

Jembe ni Jembe kuondoka Konde pale bila taratibu ugomvi wake utakuwa mkubwa sana,sababu Jembe amewekeza kwenye label na kwa Harmonize mwenyewe kwa hiyo timbwili lake litakuwa kubwa sana, Jembe kwanza msomi,Industry ya bongo anaijua tokea mwanzo wale na pili ni mtoto wa mjini.
Kwahiyo unataka kujustfy Rayvany ni msanii mkubwa kuliko Diamond? Kwa sababu Vany amepanda kwenye majukwa ambayo Diamond hajawahi? Kuwa nominated kwenye tunzo kubwa haimaniishi wewe ni msanii mkubwa kuliko wengine, nakubaliana na wewe kuwa Digital platforms ni moja ya ( narudia ni moja) ya kipimo but not only kipimo.

Despite yote bado Harmonize ni msanii mkubwa kuliko hao uliowataja, Harmonize ameweza Simama yeye kama yeye.

Issue ya Jembe kutoka itategemeana na mwelekeo wa Harmonize, kama haeleweki haitajalisha ni kiasi gani amewekeza ataona bora asepe zake kuliko kuendelea kupoteza muda, jina na heshima yake
 
Hela yake itarudi vipi? Faida jeee......
 
Uko sahihi kamba0719 kuhusu Diamond kuwapush wanamusic wake, lakini yote hiyo inaweza kuwa ni matokeo ya strong management, lakini kuhusu ukubwa wa mwanamusic hatumpimi kwenye digital platform pekee, takwimu zangu ziko sahihi mkuu, Harmonize bado ni msanii mkubwa tena top 3 kwa Tanzania, Zuchu and rest bado saaana kumfikia Harmonize.
Yes naiona dalili ya kuwa kama Harmonize asipotenganisha mapenz na kazi hata Jembe ni Jembe hatataka kuwa sehemu ya watu waliomkwamisha lazima utaondoka tu
Kwa Tanzania ukisema Harmonize yuko katika top 5 nitakubaliana nawe lakini top 3 ni big NO, ni kweli ana diehard fanatics lakini ukubwa wa msanii unaenda sambamba na kukubalika na wengi. Baadhi ya supporters ni wahuni na wavuta bangi wakiamini mihuni mwenzao anapaswa kushabikiwa(hawa wana kelele nyingi sana) na kundi jingine ni lile la haters wa Diamond ambalo lilihama kwa Kiba baada ya kuona Kiba ameishiwa 'pumzi' wakaamini Harmo ndiyo ataweza kumshusha Diamond na hata akiibuka mwingine watakayeamini ndiyo ataweza kumshusha Diamond watahamia kwake.

Sitakuwa nimemtendea haki Harmonize kama sitataja kundi linaloamini kwa dhati kwamba anaimba vizuri na ni mtunzi mzuri, hili kundi lipo bila kusahau ya kuwa strongest base yake iko kusini mwa nchi na hao wanamshabia kwa kuwa ni 'home-boy'.

Kwa Afrika hata katika top 100 hayupo, hapo umelikoroga sana.

NB: Naamini Jembe atakuwa anatafuta style ya kuchomoka, inasemekana dogo akishalikwega kaya hasikilizi la mtu isipokuwa bibie kwani ana hofu ya kwamba asipomsikiliza anaweza akaachwa.
 
Kwahiyo unataka kujustfy Rayvany ni msanii mkubwa kuliko Diamond? Kwa sababu Vany amepanda kwenye majukwa ambayo Diamond hajawahi? Kuwa nominated kwenye tunzo kubwa haimaniishi wewe ni msanii mkubwa kuliko wengine, nakubaliana na wewe kuwa Digital platforms ni moja ya ( narudia ni moja) ya kipimo but not only kipimo.
Despite yote bado Harmonize ni msanii mkubwa kuliko hao uliowataja, Harmonize ameweza Simama yeye kama yeye.
Issue ya Jembe kutoka itategemeana na mwelekeo wa Harmonize, kama haeleweki haitajalisha ni kiasi gani amewekeza ataona bora asepe zake kuliko kuendelea kupoteza muda, jina na heshima yake
Harmonize hafiki levels za Rayvanny na kwa muelekeo huu sidhani kama atakuja kuzifikia, licha ya Zuchu kuwa chini ya label ukweli ni kwamba kwa sasa Zuchu ni msanii mkubwa zaidi ya Harmonize.

Nanukuu kauli kutoka katika post moja, 'ukubwa wa msanii haupimwi kwa hisia'. Kipimo sahihi ni facts na numbers vinginevyo kila mtu atamwaga hisia zake kwa nini msanii A ni mkubwa zaidi ya msanii B.
 
3.Amwache Jembe adominate kwenye swala la Management.

..Kwa experience niliyonayo, msanii mwenye asili ya kusini (mmakonde) akipata jina kidogo anaona kamaliza ya duniani yote na hata sio ajabu baada ya muda ukamsikia akimlalamikia huyo jembe kuwa kamwibia mapato yake..nawajua sana hawa njemba
 
Back
Top Bottom