Harmonize ameniangusha kwenye Bedroom video

sangujoseph

Senior Member
Nov 30, 2015
164
183
By Sangu Joseph
.
Ninawaza kuwaambia watu nimeiona video ya Bedroom ya Harmonize_tz na hasa nikikumbuka Mzee wangu Jakaya Kikwete alipoteza muda wake kushuhudia uzinduzi wa hii Audio, nadhani kama angejua Video Ingekua hivi ambayo Mimi nimeiona angeagiza usiimbwe pale Mlimani.

Afroeast ya Harmonize ilikua ya watu wote, kuanzia wanasiasa, vijana, wanawake, viongozi wa Serikali, viongozi wa vyama, na alishaipa viwango Album yake ndiyo maana tuliona waalikwa kama Jakaya Kikwete, Tulia Ackson, Waziri Mwakyembe, Humphrey Polepole walishiriki uzinduzi na waliufurahia. (Video haina maadili + Kipindi cha Corona)
.
Viwango vya Jakaya Kikwete, Waziri, Viongozi wa Vyama, nadhani haustahili hii video, ilitakiwa kuwepo kwa video ambayo hata mtu anayefanana hadhi na Mzee Kikwete / Rais / Makamu / Waziri Mkuu aitazame, ila kwangu hii sidhani hata, Viongozi waalikwa watatamani kuuliza video imetoka. (Video haina maadili + Kipindi hichi cha Corona)
.
Nadhani Kwa hili, Harmonize na wasanii wenzake watakua wamejifunza ukiweka Standard ya kitu chako lazima umaintain hadhi yako, hasa kwa Project unayoifanya kwa wakati huo
.
Insta: FB: Twitter: Sangu Joseph
 
Back
Top Bottom