Hard working woman

Hard working woman

mimi sikubishii, naomba tu niseme labda sababu haya hayajanikuta ndo maana sielewi inakuwaje mpaka mwingine awe power tiller wakati wote mna kipato kizuri... labda hii mtu mzima mwenzangu Dark City asaidie kunielewesha

Hata mimi bado sijamwelewa teacha gfsonwin,

Na ndiyo maana nikasema kuwa, labda anaongelea uzoefu wa nyumbani kwao...ambao pia kama mtoto anaweza kuwa aliuvaa mkenge. Kwa sababu si rahisi mtoto akajua mipangilio yote ya wazazi ambayo wanaipangia chumbani...

Kwa kweli mama wa namna hiyo anahitaji maombi zaidi kuliko mwanamume!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
babu mpaka nasema hapa haya nina uhakika kabisa na hili. mbona hata mama alikua nasema wazi kamba baba yenu hapndi shida?? na huwez kuamini tulikua tunakwenda KIA kulima mama anaingia kaazini anajiiba natufwata shamba anapanda maharage kisha anarudi tena ofcn na kutuacha tunapanda kweye lile jua la KIA hadi kumsababishia mama kupata melanoma.

muda wote huo baba yuko kivulini na ilifika mahali tulimwuliza mama kwann haya mama akasema namjua mume wangu hapendi shida na akija huku ataumwa. ila uzuri wa baba mkirudi home mnakuta hata menu karekebisha fresh na maji katenga ya kuoga jikoni kwa jinsi alivyokuwa na upendo. nilikuja ku conclude kwamba baba yangu amezaliwa mtu wa aina hiyo so hawez kubadilika na sio kwamba anapenda ila ndo yuko ivyo.
hapa umezungumzia kazi ya aina fulani.....
hilo linaeleweka kabisa, kuna mtu hapendi kazi hii lakini ana bidii na kazi nyingine.
mimi pia wakati tupo kwa wazazi ilikuwa mwendo wa shamba, na mimi nilionekana kabisa sipendi kazi za shamba...
ndugu zangu wote walikuwa wanaomba mimi nisiende shamba maana nitawatia uvivu, mara nimeona nyoka, mara kichwa kinauma, basi hiyo siku watu hawafanyi kazi inavyopaswa.
ila wakiniacha nyumbani, wanakuta mambo safi kabisa, yaani wakirudi ni kuoga, kula, na kulala, kila kitu poa kabisa....
na nilipoona siwezi mambo ya shamba nikakazana kwa ninayoyaweza ili maisha yangu yasiishie kwenye kazi nisiyoiweza.....
hayo ni kawaida kabisa rafiki.
 
Hata mimi bado sijamwelewa teacha gfsonwin,

Na ndiyo maana nikasema kuwa, labda anaongelea uzoefu wa nyumbani kwao...ambao pia kama mtoto anaweza kuwa aliuvaa mkenge. Kwa sababu si rahisi mtoto akajua mipangilio yote ya wazazi ambayo wanaipangia chumbani...

Kwa kweli mama wa namna hiyo anahitaji maombi zaidi kuliko mwanamume!!

Babu DC!!
ni kweli kabisa ni ngumu kujua mipangilio ya wazazi.....
mimi huwa nacheka sana na wanangu, nikitoka nao kwenda sehemu huwa hawanidai kununua vitu, wameshajua mama hana hela, ila wakitoka na baba hawawezi rudi mikono mitupu...... ni kweli mama hana hela?
na kuna siku baba alipokuwa kwenye safari zake wakamwomba awanunulie games....... baba kweli alijisahau tu hakununua, aliporudi akaomba msamaha kuwa hakupata atawanunulia siku nyingine, mmoja akamwambia usijali mama akisafiri atatununulia maana anakoendaga kuna games nyingi sana.....:confused2:
mawazo ya watoto wakati mwingine yanakuwa tofauti na uhalisia wa wazazi
 
sijaeleweka wapi?? hapa babu nasema jambo ambalo liko wazi kabisa na nilikuwa naona jinsi ambavyo hata ndugu zake bba wakiugua wanakuja kutbiwa nyumban na mama likuwa natuambia of course baada ya kukua kwamba mumewe anajipenda zaid kuliko kazi hivyo mama hakuoana sababu ya kuumiza moyo wake ilihali ndo kesha kuwa huzzy wake.

alichofanya alichapa kazi baba akabaki kuwa ni msemaji tu. binafsi nilifika mahali nikasema sitaolewa na mwanaume wa kimachame kwasababu wao ni watanashati wanajipenda wao kuliko kazi. mpaka leo ukienda mtaani kwetu watu humtania baba kwa sababu ya usafi na utanashati wake.

lakini hawajui njinsi ambavyo mama anaumia kwaajili ya kuyafanya hayo yatookee. nashindwa kuelewa kwann mnaona kama sikuelewa vyema.

babu nimezaliwa hapa nimekulia hapa miaka yangu yote hata kama leo niko kwangu, na uzuri kazi tulikuwa tunafanya na mama so nilijua ni wapi mama anapita kwa wakati huo.

baba alikuwa nafanya kazi coffee curing ila hakuna siku aliwah kuja na kairoba cha sukari home, ila mama akitoka job amepita shamba kuangalia shamba na anarudi na furush la bidhaa.
 
ni kweli kabisa ni ngumu kujua mipangilio ya wazazi.....
mimi huwa nacheka sana na wanangu, nikitoka nao kwenda sehemu huwa hawanidai kununua vitu, wameshajua mama hana hela, ila wakitoka na baba hawawezi rudi mikono mitupu...... ni kweli mama hana hela?
na kuna siku baba alipokuwa kwenye safari zake wakamwomba awanunulie games....... baba kweli alijisahau tu hakununua, aliporudi akaomba msamaha kuwa hakupata atawanunulia siku nyingine, mmoja akamwambia usijali mama akisafiri atatununulia maana anakoendaga kuna games nyingi sana.....:confused2:
mawazo ya watoto wakati mwingine yanakuwa tofauti na uhalisia wa wazazi

FP umri wa mm kuweza kupanda maharage ama kauchuma kahawa haukuwa mdogo kiasi cha kushindwa kuelewa bana. ninyi mtakataa uhalisia ila ukweli kabisa kuna wababa ambao wameumbwa wazuri kenye kila kitu ila tu sio wawezeshaji. yaani hapa ninauhakika kabisa
 
hapa umezungumzia kazi ya aina fulani.....
hilo linaeleweka kabisa, kuna mtu hapendi kazi hii lakini ana bidii na kazi nyingine.
mimi pia wakati tupo kwa wazazi ilikuwa mwendo wa shamba, na mimi nilionekana kabisa sipendi kazi za shamba...
ndugu zangu wote walikuwa wanaomba mimi nisiende shamba maana nitawatia uvivu, mara nimeona nyoka, mara kichwa kinauma, basi hiyo siku watu hawafanyi kazi inavyopaswa.
ila wakiniacha nyumbani, wanakuta mambo safi kabisa, yaani wakirudi ni kuoga, kula, na kulala, kila kitu poa kabisa....
na nilipoona siwezi mambo ya shamba nikakazana kwa ninayoyaweza ili maisha yangu yasiishie kwenye kazi nisiyoiweza.....
hayo ni kawaida kabisa rafiki.

hilo sikatai rafiki ila amini tu kwamba kuna watu ambao hua wanaweza kuwezesha na kuna wengine sio kabisaaa.

tena unakuta mama wa aina hii akisafiri chumvi ikiisha ndani baba atampigia simu chumvi hakuna sasa hapo sijui mama atailetaje na yuko mbali
 
Sometimes inategemea na mwanamke ni rahisi gani ku-raise hiyo hela mnayotegeana

Unaweza kuta ada ya mtoto 1m kwa mwaka, hii nayo hadi mkimbizane weee

Unaweza kuta kwa mwezi mke anaingiza 3m

So inategemea, ila kama mke anaingiza let say laki 3 kwa mwezi afu ada 1m, inaweza mwia ngumu ku-raise hiyo amaount

Hakuna jibu la moja kwa moja hapa

Me im with my mother 100% kwanini ujitese wakati wote uwezo wa kucover majukumu mnao! Ili mumeo akuone unampenda sanaaaa? Ah wapi!

Wanaume wanatakiwa wawe responsible sio kutegea wake zao.

Kama mtu hatoi measures zifanyike awe anatoa banaaaa!
 
lara 1 sio rahisi kujikausha kununua chakula au kulipa ada ya watoto eti kwa sababu mume hanunui au halipi. Siku ukiwa na watoto/familia utalielewa hilo. Kina mama wanaojitambua au walio wengi wanapenda waone watoto wao au familia zao zina maisha mazuri wakati wote au zinapata mahitaji muhimu so to speak. Hii husababisha kina mama wa aina hiyo kufanya kazi ya kutafuta pesa kwa bidii zaidi maana hawako tayari kuona watoto wakikosa mahitaji muhimu. Pia mke/mama anayejitambua huwa hayuko tayari kuona mume wake au familia yake ikiaibika kwa chochote kile. Hivyo lazima ajitahidi kufukia mashimo.
gfsonwin binafsi sipendi kuomba omba pesa iwe kwa ajili ya mambo madogo madogo au hata ya shughuli za maendeleo. Mie huamini kuwa mume anatakiwa kujua wajibu wake na hatakiwi kusubiri aombwe. Mie mtu akijikausha atashangaa kuona ninaendelea kukamilisha tulichopanga au ninachotaka bila kuomba omba yaan kama hayupo vile! Kama mwanaume ana akili atajua anatakiwa kufanya nini.

Kikubwa kinachoniudhi sana, unakuta mwanamke umejishughulisha lets say kwenye ujenzi kisha ndugu wa mume wakiona wanaanza kumpongeza ndugu yao as if wanahakika hicho wanachokiona kimefanywa na ndugu yao. Mtu mko pamoja badala hata ya kuwapongeza kwa ujumla wenu, utasikia "flani (jina la mume) hongera sana umejenga nyumba nzuri sana..."! Hapo ndio mtu unaishia kutukana kimoyo moyo!
 
Last edited by a moderator:
Sometimes inategemea na mwanamke ni rahisi gani ku-raise hiyo hela mnayotegeana

Unaweza kuta ada ya mtoto 1m kwa mwaka, hii nayo hadi mkimbizane weee

Unaweza kuta kwa mwezi mke anaingiza 3m

So inategemea, ila kama mke anaingiza let say laki 3 kwa mwezi afu ada 1m, inaweza mwia ngumu ku-raise hiyo amaount

Hakuna jibu la moja kwa moja hapa

Swala sio ability ya kurais the funds! Noooooo! THE ISSUE IS OUT OF PRINCIPLES TU NI WAJIBU WAKE!

Hata kama mumu unaraise 3M na mumeo 2M, je Mwanaume hiyo 2M nanapeleka wapi???????? Atoe hiyo 2M ionekane then aseme amekwama coz ni impossible yeye kutoa zaidi coz kipato chake ndo kimeishia hapo, then mwanamke akimsapoti its okay!

Ila mambo ya mtu unapata 3m zoote unudumia familia, Mr. 2M afu yote ananywea bia, supu, kitimoto, michemsho na kuhonga! Aaaaaaaaaawapi!
 
lara 1 sio rahisi kujikausha kununua chakula au kulipa ada ya watoto eti kwa sababu mume hanunui au halipi. Siku ukiwa na watoto/familia utalielewa hilo. Kina mama wanaojitambua au walio wengi wanapenda waone watoto wao au familia zao zina maisha mazuri wakati wote au zinapata mahitaji muhimu so to speak. Hii husababisha kina mama wa aina hiyo kufanya kazi ya kutafuta pesa kwa bidii zaidi maana hawako tayari kuona watoto wakikosa mahitaji muhimu. Pia mke/mama anayejitambua huwa hayuko tayari kuona mume wake au familia yake ikiaibika kwa chochote kile. Hivyo lazima ajitahidi kufukia mashimo.
gfsonwin binafsi sipendi kuomba omba pesa iwe kwa ajili ya mambo madogo madogo au hata ya shughuli za maendeleo. Mie huamini kuwa mume anatakiwa kujua wajibu wake na hatakiwi kusubiri aombwe. Mie mtu akijikausha atashangaa kuona ninaendelea kukamilisha tulichopanga au ninachotaka bila kuomba omba yaan kama hayupo vile! Kama mwanaume ana akili atajua anatakiwa kufanya nini.

Kikubwa kinachoniudhi sana, unakuta mwanamke umejishughulisha lets say kwenye ujenzi kisha ndugu wa mume wakiona wanaanza kumpongeza ndugu yao as if wanahakika hicho wanachokiona kimefanywa na ndugu yao. Mtu mko pamoja badala hata ya kuwapongeza kwa ujumla wenu, utasikia "flani (jina la mume) hongera sana umejenga nyumba nzuri sana..."! Hapo ndio mtu unaishia kutukana kimoyo moyo!
aisee hapa ngoja nimwite snowhite,

sasa kasheshe mwali inakuja umefanya kitu wewe peke yako ila ukweni sifa zote analundikiwa yeye asante sana kwa msaada wako yaani kwakweli u mwanaume.............halafu wewe hata ile asante ya mdomo hupewi na hao ndugu zake
 
Last edited by a moderator:
Sometimes inategemea na mwanamke ni rahisi gani ku-raise hiyo hela mnayotegeana

Unaweza kuta ada ya mtoto 1m kwa mwaka, hii nayo hadi mkimbizane weee

Unaweza kuta kwa mwezi mke anaingiza 3m

So inategemea, ila kama mke anaingiza let say laki 3 kwa mwezi afu ada 1m, inaweza mwia ngumu ku-raise hiyo amaount

Hakuna jibu la moja kwa moja hapa

ishu hapa Kongosho una address jambo gumu kwa lugha ngumu sana.

lkn ukweli wa ndani ya kuta 4 upo ndani mwa wawili laiti mapaa yangeezuliwa tuone ama tuskie hapa kila mtu angeongea tofauti kabisaaa.

mie niko hivi as long as napata amani na raha ndani mwangu basi mengine sitoyajali period. manake ningepewa huyu wa kunipa kila kitu bado nisingemuweza
 
Last edited by a moderator:
ni kweli japo mara nyingi wababa watabisha. lakini ukiwa na strategy, unakuwa hardworking and you push your man to work hard too.
tatizo analipata mdogo wangu (baby dont read this, lol), she is hard working na anabarikiwa haswa. mume yuko busy na competition ila in a good way. mwisho wa siku wanaendelea.
ndio maana nasemaga hapa, baba aangalie familia yake entirely! alipe bills, alipe ada etc. Mama atachip in kwenye maendeleo. Kama mkitaka kununua gari na kujenga nyumba, haidhuru kama mama akatoa hela hata zaidi ya baba. kuna rafiki yake Paw aliwahi kusema ameandikisha kila kilicho chake kwa mkewe. kwa sababu ana uhakika siku mkewe akifa hakuna atakaemsumbua, ila yeye akifa anajua mkewe atasumbuliwa. na anakiri yeye na mkewe wanasaidiana maendeleo.

Haya tunayapenda sana kwa wake zetu ila baadhi yenu mbona mkishajua mali mmeandikiwa mnaanza kitim tim ili man ukileta za kuleta unafungashiwa nguo...Dada ni jambo jema ila mara nyingi halijaleta mwisho mzuri.
 
lara 1 sio rahisi kujikausha kununua chakula au kulipa ada ya watoto eti kwa sababu mume hanunui au halipi. Siku ukiwa na watoto/familia utalielewa hilo. Kina mama wanaojitambua au walio wengi wanapenda waone watoto wao au familia zao zina maisha mazuri wakati wote au zinapata mahitaji muhimu so to speak. Hii husababisha kina mama wa aina hiyo kufanya kazi ya kutafuta pesa kwa bidii zaidi maana hawako tayari kuona watoto wakikosa mahitaji muhimu. Pia mke/mama anayejitambua huwa hayuko tayari kuona mume wake au familia yake ikiaibika kwa chochote kile. Hivyo lazima ajitahidi kufukia mashimo.
gfsonwin binafsi sipendi kuomba omba pesa iwe kwa ajili ya mambo madogo madogo au hata ya shughuli za maendeleo. Mie huamini kuwa mume anatakiwa kujua wajibu wake na hatakiwi kusubiri aombwe. Mie mtu akijikausha atashangaa kuona ninaendelea kukamilisha tulichopanga au ninachotaka bila kuomba omba yaan kama hayupo vile! Kama mwanaume ana akili atajua anatakiwa kufanya nini.

Kikubwa kinachoniudhi sana, unakuta mwanamke umejishughulisha lets say kwenye ujenzi kisha ndugu wa mume wakiona wanaanza kumpongeza ndugu yao as if wanahakika hicho wanachokiona kimefanywa na ndugu yao. Mtu mko pamoja badala hata ya kuwapongeza kwa ujumla wenu, utasikia "flani (jina la mume) hongera sana umejenga nyumba nzuri sana..."! Hapo ndio mtu unaishia kutukana kimoyo moyo!

Mwa J mimi nimesema hapo juu as long as mdingi yuko home, Maza hatoi pesaaaa! Ndio maisha niliokulia mimi. Na ada nimerudishwa kama mara 5 hivi dingi hajalipa ada, na maza HATOIII!!!!

Maza wangu sio mchoyo, hela za kujinafasi ananipa sanaaa, sijui trip za shle zote lazima niende hata kama sitaki, sijui fashion imeingia ananipa hela, anything i want.

Ila swala la kuwa mnyonge wa mdingi hakunaga! Kama ni jukumu la mdingi ajibalaguzeeee, ajivuteeee, ajizungusheee mwisho lazima alimalize hilo jukumu. Hamuulizi wala halifanyi! Katuuuuu! Hadi mdingi mwenyewe kachemka! Anamwambiaga wewe kwanini hauko kama wanawake wenzio kujituma kuhudumia familia? Anamwambia na wewe kwanini haupo kama warabu uniachishe kazi nikae hapa unimwagie midhahabu?

Mwanaume anajifanya nunda kukupima tu, ukikomaaa kufa na kupona anatoa.

Kuna kipindi mdingi aligomaaa kama wiki hivi kutoa ada, akamwambia ikifika kesho kutwa hela hujatoa nakuja kwa bosi wako na ustawi wa jamii kublock mshahara! Usinitanie kabisaaa. Kesho akatoa! Kumbe alikuwa nazo basi tu.

Mwanamke unatesekaaa ukichunguza hela za huyo mume zinaenda wapi utshangaa na roho yako! Hakuna la maana analofanya zaidi ya kunywa bia!
 
aisee hapa ngoja nimwite snowhite,

sasa kasheshe mwali inakuja umefanya kitu wewe peke yako ila ukweni sifa zote analundikiwa yeye asante sana kwa msaada wako yaani kwakweli u mwanaume.............halafu wewe hata ile asante ya mdomo hupewi na hao ndugu zake

Kwa kweli mie huwa nakereka sana na hiyo tabia labda kwa vile mie huwa natambua sana wayafanyayo wifi zangu upande wa kaka zangu. Nadhani tatizo ni mfumo dume kwa baadhi ya jamii. Wao hata mwanamke afanya nini huwa hawaoni na huamini kuwa kilichofanyika ni juhudi za kijana wao wa kiume.
 
NDO MANAKE!OH!
mpango wa kazi kwa mama mpango wa sifa kwa baba!
 
Wanawake hardworking uangalie mahali anakotoka kama Rombo mashati au Rombo tarakeea huko! Sisi wanawake wa pwani asili yetu ni kujipaka hina na kushinda barazani ikauke.

Hata tusome vipi uvivu na kulalamika kazini kuacha mwiko, hata promotion inabidi tutumie shortcut ambapo ndo the only sector we are best at.

Afu wanaume wa siku hizi kauzu zaidi ya dagaaa, ukijifanya hardworking kidogo na mtoaji mbona majukumu yote anakutelekezea hapo. Utalipa ada zote, utalisha familia, utajenga, yaani ukija kustuka you are alredy 50yrs, More than 20yrs of your life umefujwa fujwa tu.

Mwenzangu ukiona mtu hatoi na wewe jikaushe kau! Kama hajigusi kujenga we jenga kwa siri, kama chakula hanunui na wewe jikaushe kau! Ada jikaushe hivohivo hata watoto wakirudishwa poa tu, mbona atalipa. Hii inakuwaga mnyonge mnyongeni! @ Mama lara kuku zikipitishwa ofisini lazima amuulize baba lara achukue ngapi na pesa yake atarudishiwa lini?

Ila kuna EXTREME CASES! za wanawake too much is harmfull

1.Wamama wa pwani! Jamani tupunguze, wajiremba wewe tu, kujishindilia midhahahabu tuuuuu, na make up za ghali sanaaa! Midera ya laki 3, miguo kabati ya milango 4 haifungi, ila kila siku wapika maharage! Wanao rafurafu. Ukipata hata mia wawekeza kwa sonara au botique.

2.Wamama wachaga! Kila senti wawekezaaa tu! Kutwa kutuma hela nyumbani kwenu. Kila siku wajenga tuuuu! Nani ataishi humo mijumba yote hiyo? Huli kwa rahaaa na kujinafasi, Hujipendezeshi, hujitreat! Kutwaaa wewe kusave na kusave tu. Kujenga kwenue, sijui nini! Khaaaaaaaa! Wanao na mumeo hawafaidi kisa unainvest!

3. Wamama Wanyamwezi na wamanyema! Kutwaaa pesa yote kusaidia nduguzo. Hata hamuendelei wewe ndo umejitwisha familia yenu mazimaaaa! Haihusu kabisaaaa. Pesa zote watuma nymbani!!!
mmmh lara wee,hiyo no.1 mimi mtu wa pwani na siko hivyo.i'm working hard,ila kwa wengine wa pwani ninaowafahamu,kujipamba kwao,wanawapambia waume zao kwani ndivyo walivyofundishwa.mwanamke ndani ni pambo la nyumba.na wengine hawaruhusiwi kabisa kufanya kazi na waume zao.
 
Kuna rafiki yangu huu uzi wako utakuwa umemgonga kumoyo... ipo siku ntakuonyesha i wish.... wanaume wa namna hiyo si ndio hao tunawaita Mariooo, wanaume wa namna hiyo lazima kisaikolojia uwe tayari kuishi nao la sivyoo ngumu sana.

Kwakweli huyo shemeji yangu inafika mahali anachanganyikiwa ada za watoto,kodi ya nyumba, chakula na mavazi anahangaika yeye mwenyewe. jamaa yeye viti virefu na misele kibao akijifanya yuko bussy... jamani tujitahidi malezi ya watoto wetu wasijefanya haya makosa yetu
 
Kwa kweli mie huwa nakereka sana na hiyo tabia labda kwa vile mie huwa natambua sana wayafanyayo wifi zangu upande wa kaka zangu. Nadhani tatizo ni mfumo dume kwa baadhi ya jamii. Wao hata mwanamke afanya nini huwa hawaoni na huamini kuwa kilichofanyika ni juhudi za kijana wao wa kiume.

kiukweli binafsi napenda sana kumsifia mtu akifanya jambo zuri, na huwez kaumini wifi yanu akifanya jambo zuri huwa nasifia yeye na kumsuta kaka kwamba uchangamke kumtia moyo mkeo tena bila kificho.

sasa inapokuja huku kwingine ndo balaa, yaani sifa zinakwend aambako hazistahili kabisaa.
 
Mwa J mimi nimesema hapo juu as long as mdingi yuko home, Maza hatoi pesaaaa! Ndio maisha niliokulia mimi. Na ada nimerudishwa kama mara 5 hivi dingi hajalipa ada, na maza HATOIII!!!!

Maza wangu sio mchoyo, hela za kujinafasi ananipa sanaaa, sijui trip za shle zote lazima niende hata kama sitaki, sijui fashion imeingia ananipa hela, anything i want.

Ila swala la kuwa mnyonge wa mdingi hakunaga! Kama ni jukumu la mdingi ajibalaguzeeee, ajivuteeee, ajizungusheee mwisho lazima alimalize hilo jukumu. Hamuulizi wala halifanyi! Katuuuuu! Hadi mdingi mwenyewe kachemka! Anamwambiaga wewe kwanini hauko kama wanawake wenzio kujituma kuhudumia familia? Anamwambia na wewe kwanini haupo kama warabu uniachishe kazi nikae hapa unimwagie midhahabu?

Mwanaume anajifanya nunda kukupima tu, ukikomaaa kufa na kupona anatoa.

Kuna kipindi mdingi aligomaaa kama wiki hivi kutoa ada, akamwambia ikifika kesho kutwa hela hujatoa nakuja kwa bosi wako na ustawi wa jamii kublock mshahara! Usinitanie kabisaaa. Kesho akatoa! Kumbe alikuwa nazo basi tu.

Mwanamke unatesekaaa ukichunguza hela za huyo mume zinaenda wapi utshangaa na roho yako! Hakuna la maana analofanya zaidi ya kunywa bia!

Uzuri baba yangu alikuwa analijua jukumu lake la kulipa ada kama sala vile! Siku ya kwanza ya kufungua shule lazima mtoto aende na ada mkononi (enzi hizo ada tunalipia shule). Mambo mengine aliweza kujikausha lakini mama alikuwa mstari wa mbele kuona kila kitu kinaenda sawa. K

wa kweli binafsi nitaona aibu mtoto akirudishwa home eti kwa vile hatujalipa ada ili hali uwezo wa kufanya hivyo upo. Sitapenda kuona mtoto anakuwa mnyonge sababu ya mvutano wa wazazi kutegeana kulipa ada. Nitalipa kisha ntajua namna baba atakavyozirudisha wakati mwingine bila hata yeye kujua!
 
Back
Top Bottom