Harakati za fao la kujitoa

Harakati za fao la kujitoa

Mimi napatwa na hasira sana.
TUCTA wako wapi?mbona suala hili hawalizungumzii wala kulipa uzito wowote.Suala la malipo ya 25%walilupigia kelele sana mpaka wakafanikiwa lakini fao la kujitoa mbona kimya?
Naona hapa kuna ubaguzi mkubwa kutoka TUCTA na wanachama wake,kama kweli wangekuwa wanatetea matatizo ya wanachama basi fao la kujitoa bado lingekuwa agenda kubwa hivi sasa.

Mimi nasema bora nijitoe kwenye vyama vya wafanyakazi kwasababu sioni mchango wao wowote ilihali mchango wangu kika mwezi wanapata.Nasema najitoa kutoka vyama vya wafanyakazi.

#TUPENI_FAO_LETU
#HAKI_YETU_SIYO_HISANI

Vyama vya wafanyakazi ni vyombo vya propaganda kwa serikali ya chama.

Eti baada ya Magu kurudisha kikokotoo cha zamani wakafanya maandamano.

Wahuni sana.
 
Hii mifuko ilipe pesa za watu wote bila ubaguzi walioachishwa ,walioacha ,waliotumbuliwa na Jiwe ,vyeti feki ,wote walipwe ili mradi walichangia pesa yao .Mbona wakubwa wanaziteka tu pesa za wafanyakazi na hawajachangia chochote .
 
Hii mifuko ilipe pesa za watu wote bila ubaguzi walioachishwa ,walioacha ,waliotumbuliwa na Jiwe ,vyeti feki ,wote walipwe ili mradi walichangia pesa yao .Mbona wakubwa wanaziteka tu pesa za wafanyakazi na hawajachangia chochote .

Hao wanajua kuzitungia sheria na matumizi, zao hazipiti huko. Na wakimaliza kazi wanavuta mpunga wao.
 
Amani iwe kwenu wapendwa.

Background: Mifuko ya hii ya NSSF na PPF (siku hizi PSSSF) ilikuwa na utaratibu kwamba unapoacha kazi kwa hiari, kufukuzwa, mkataba kuisha unachukua hela yako maisha yanaendelea.

Around 2014/2015 huo utaratibu ulisitishwa, ukiuliza unaambiwa sheria hairuhusu, ingawa kuna baadhi walikuwa wanapata kwa mikakati maalum.

Mifuko ikaunganishwa, likaja swala la vikokotoo na Fao la Kukosa Ajira.

Tar 28 Dec 2018, Mh Rais alitengua swala la vikokotoo vipya na kusema mambo yawe kama zamani, ni baada ya kufanya kikao na wadau husika SSRA, wawakilishi wa wafanyakazi, wahusika wa taasisi hizo nk. Na tumeona maandamano ya kumpongeza Rais kwa tukio hili.

Bahati mbaya, kinachoonekana ni kwamba swala la Fao la Kujitoa limewekwa kando, tukifatilia tunaambiwa hakuna mwongozo.

Kuna watu kibao wako mtaani na kazi zimekuwa ngumu kupata, kuna walio maofisini wangetamani kuacha wachukue mitaji wafanye mambo yao, kuna walio maofisini muda wowote watakuwa vijiweni nao wanatamani kuwa na uhakika wa hii fedha.

Kama hili swala lisipopatiwa ufumbuzi kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi, tusahau kulipatia ufumbuzi.

Nini cha kufanya:-
Wahanga, na wote ambao ni wazalendo tunatakiwa kwa pamoja tutoe mapendekezo kuhusu hili swala, kama ni kutengeneza petition, kama ni kufanya maandamano kuonana na waziri husika, waziri mkuu au kuelekea SSRA, kama pia ni kufanya utaratibu wa kuonana na Rais, etc.

Kupitia hii thread, tunaweza ku-brainstorm ni njia ipi tunaweza kuitumia kuhakikisha taarifa zinamfikia Rais kwamba kuna watu wanakufa njaa wakati hela zao zipo, haki yao ipo.

Tukumbuke kwamba jinsi tutakavyoonesha wingi wetu, influence yetu ndivyo hivyo hivyo swala letu litachukuliwa serious.

Naomba kuwasilisha.
Petition itengenezwe faster.
 
Tatizo tunapishana uelewa, ile speech hakuna mahali Rais alilifanyia hitimisho swala la Fao la Kujitoa, isipokuwa yalikuwa mapendekezo kwamba waangalie namna ya kufanya.

Swala lililotolewa hitimisho ni kuhusu kikokotoo.
Kuna jamaa niliwahi mueleza kama maelezo yako,tukabishana nikaona isiwe tabu,kuna jamaa waifungua wachukue fao la kujitoa wanadunda
 
Imekwama na unaposikia mtu kalipua kijiji manake mazungumzo hayakufua dafu. Naunga mkono hoja sema ulipuaji ndio mara zote unawakuta wasio na hatia sababu wahusika wanajilinda hatare kukwepa kubeba dhamana ya matendo yao.
Tunatakiwa kutumia njia ambazo ni diplomatic.
 
Back
Top Bottom