Happy Valentine H.E Jakaya Mrisho Kikwete! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Happy Valentine H.E Jakaya Mrisho Kikwete!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NasDaz, Feb 14, 2012.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kuwapo kwa ugumu wa maisha na kuwa kama tuliochanganyikiwa lakini sijafikia kiwango cha kusahau kukutumia salama zangu za wapendanao (au za wapendao?) leo hii, bila kusubiri "mwaisha bora" uliyotuahidi! Si wewe peke yako, bali na chama chama chako Chama Cha Mapinduzi a.k.a CCM!

  Happy Valentine H.E. Honarable Jakaya Mrisho Kikwete!

  Pamoja na yote hayo bado kuna jambo linanishangaza Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu! Wakati naandika salamu zangu kwako taratibu najikuta nikibubujikwa na machozi! Kwanini? Najiuliza kwa haraka haraka kisa cha chozi langu kati kati ya salamu zangu za upendo kwako! Hata hivyo, nakosa jibu! Nafahamu, wengi wapendao hujikuta wakibubujikwa na machozi pale wanapozielezea hisia zao! Hapo ndipo ninapozinduka na kuukumbuka wimbo wa mwanamuziki wa kizazi kipya, Hamisi Mwijuma au Mwana FA uitwao Hawajui Tulikotoka! Je, Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu huwa unapata muda wa kuwasikiliza hawa vijana? Usiwasikilize wale wasioupenda muziki huu kwamba hamna chochote wanachoimba! Kuna kijana mwingine, kwa kupitia muziki huu huu amemtuma Ridhiwan eti aje kuongea na wewe! Sitaki kuamini kwamba vijana hawa wamefikia hatua ya kuamini kwamba wakikueleza wewe moja kwa moja hutawasikiliza hata waamue kumtumia kijana wako Ridhiwan! Nakupenda Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu hivyo sipendi kuona wala kusikia watu wakikusema vibaya! Hivyo basi, endapo ni kweli pamejengwa ukuta katikati yako na wananchi basi ni heri ukuta huo ukabomolewa mapema na kujengwa daraja kama njia moja wapo ya kusikiliza ushauri wa Mjomba Mrisho Mpoto aliyewahi kukueleza kabla kwamba "heri kujengwa daraja kuliko ukuta...."

  Salale! Inawezekana hivi sasa naelekea kuchanganyikiwa kwani tayari nilishasahau ni nini hasa nilipanga kukueleza hapo juu! Kama nilivyokueleza hapo juu kwamba baada ya kuzinduka ndipo nikagundua kwamba huenda chozi langu linafanana na yale ambayo Mwana FA alipata kuyaongea kwenye wimbo wake. Mtu anapenda huku akiteswa vikali na ampendae! Utakosa vipi kumwaga machozi wakati unapomtumia Salamu za Wapendanao!?

  Eti Wamachinga na Wandengereko nao walikuwa na mpango wa kumtuma Mama Salma eti aje kukupa ujumbe kama alivyoagizwa Ridhiwani! Nikawapoza, nikawaambia ujumbe wao kwako nitaweza kuuleta hata mimi! Wametamka bayana kwamba hili la kuongeza posho za wabunge kwa malaki katu halikubaliki hata chembe! Nami naungana nao, isitoshe sina namna kwani tayari wameshanibebesha msalaba ili nikufikishie ujumbe huo. Ni kweli, pamoja na upendo wangu kwako Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu, kwa hili la hapana!

  Hata hivyo, wakati nikisisitiza kwamba suala hilo halikubaliki, bado kuna lingine linaendelea kuelelea akilini mwangu! Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu, hivi ilikuwaje kuhusu mkanganyiko wa posho uliokuwa umejitokeza hivi majuzi katikati ya mgomo wa madaktari?! Mheshimiwa Rais wangu, kumbuka kwamba nakupenda kwa dhati! Hivi una habari kwamba wale wenye vijiba vya roho wanakuita msanii? Yaani Rais wa nchi awe msanii; hapana! Sitaki kuamini, na isitoshe tayari katiba mbovu iliyopo inanilazimisha kumtii rais wa JMT! Mimi ni raia mzalendo niliyekata shauri la kuilinda katiba yetu hata kama nyie mliyeapa kufanya hivyo mnakwenda kinyume na viapo vyenu! Hivyo basi, kwangu mimi kumwita rais ni msanii ni kuvunja katiba kwani hiyo katu haiwezi kuwa utii! Pamoja na hayo, jaribu kukanusha japo kidogo.

  Je, ni kweli, Mheshimiwa Rais wangu wewe binafsi na serikali yako ni wasanii?! Hebu fikiria, katikatika ya mgomo wa madaktari Mheshimiwa Waziri Mkuu akatangaza kwamba posho za wabunge zimepanda toka Sh.70,000/= hadi Sh.200,000/=! Papo hapo, Spika wa Bunge nae akathibitisha kwamba Mheshimiwa Rais wangu, nikupendae umeridhia kupanda kwa posho hizo! Ghafla, kijana wako Salva Rweymamu akaja na taarifa kwamba katu hujaridhia kupanda kwa posho hizo na kwamba ulichokuwa umeagiza ni kutumika kwa busara katika kushughulia suala hilo la posho!!! Haya sasa, Mheshimiwa Rais wangu nikupendae; naomba unisaidie katika hili ili upendo wangu kwako usiwe na doa. Kama kweli uliagiza busara itumike katika kushughulikia posho za wabunge; je, Waziri Mkuu alitumia busara gani kutangaza kupanda kwa posho wakati madaktari wakiwa katikati ya mgomo wa kudai maslahi zaidi?! Huoni kama alikuwa anakuchonganisha na madaktari pamoja na wananchi ili uonekane unajali maslahi ya wabunge wachache na kuwadharau madaktari na ulifanya hivyo huku wapiga kura wako wakiwa wanakufa kwa kukosa huduma?! Mheshimiwa Raisi wangu, hivi huoni kwamba Mheshimiwa Waziri Mkuu na Spika wa Bunge waliamua kukuhujumu kwa makusudi ili uchukiwe na wananchi?!

  Mheshimiwa Rais wangu, sipendi niwe mnafiki! Kwa mara ya kwanza, nilianza kujenga chuki dhidi yako pale niliposikia kwamba umeridhia uongezaji wa posho za wabunge wakati wananchi wakiwa wanakufa kwa kukosa huduma za madaktari! Sasa Mheshimiwa Rais wangu; ikiwa mie nikupendae tayari nilishaanza kujenga chuki dhidi yako; je wale ambao tangu hapo hawakupendi?! Usisahau Mheshimiwa rais wangu kwamba, nazitoa salamu zangu hizi za Valentine kwako wakati bado nabubujikwa na machozi! Ni kweli uliwaambia waheshimiwa wenzako kwamba watumie busara? Na kama ni kweli, mbona waliamua kukuhujumu?! Vipi unaikumbatia hujuma kubwa kama hiyo toka kwa watendaji wako wakuu? Na kama kweli uliwaagiza watumie busara, mbona walidai kwamba uliridhia Mheshimiwa rais wangu? Ina maana waliamua kuudanganya umma uliokupigia kura na kukupa ridhaa ya uongozi?! Inakuwaje basi bado unaendelea kufanya kazi na viongozi ambao ama ni waongo na wazushi wakubwa au wahujumu wakubwa wa uongozi wako?! Nijuavyo, kama ni kweli uliwaagiza watumie busara, basi Mheshimiwa Waziri Mkuu na Spika wa Bunge ni wahujumu wakubwa waliokusudia kukuhujumu wewe binafsi na vile vile ni waongo na wazushi wakubwa waliokusudia kuwadanganya watanzania. Yote kwa yote, hizo ni sifa mbaya kabisa ambazo katu kiongozi awe wa umma au vinginevyo, hastahili kuwa nazo! Sasa Mheshimiwa Rais wangu mbona bado unaendelea kufanya nao kazi?!

  Mheshimwa Rais wangu Mpendwa, au ni Salva? Ni kijana wako Salva Rweymamu ndiye muongo? Je, ni kweli uliridhia kupandishwa kwa posho za wabunge lakini ni Salva ndie muongo aliyesema kwamba hukuridhia? Kama muongo ni huyo Salva, ni kwanini basi aliamua kuwadhalilisha Mheshimiwa Waziri Mkuu na Spika wa Bunge hata waonekane ni wazushi wakati ukweli ni kwamba ulisharidhia? Ni wapi Salva alipata ujasiri wa kuwadhalilisha viongozi wakuu wa nchi hii kwa kuwaonesha mbele ya jamii kwamba ni waongo?! Na ni wapi Salva alipata ujasiri wa kukuzushia bosi wake uongo? Kama kweli uliridhia, halafu Salva anasema hukuridhia; basi hapo maana yake ni kwamba anakuzushia uongo! Sasa, Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu; inakuwaje unaendelea kufanya kazi na Salva muongo, mzushi na mchonganishi?! Kama Salva ni muongo, mzushi na mchinganishi kiasi hicho; ni kwanini basi usimfute kazi mara moja?! Au ni kweli Mheshimiwa Rais wangu wewe ni legelege?! Haiwezekani; yaani Luteni wa jeshi awe legelege?! Sasa mbona huchukui maamjuzi dhidi ya huyu Salva muongo?!

  Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu. Lengo langu si kusutana, bali ni kukutakia Salamu za Wapendanao....Happy Valentine H.E. Honorable Presdient Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete. Hata hivyo, bado unanichanganya Mheshimiwa rais wangu! Au lile suala la kupanda kwa posho lilikuwa ni "danganya toto kula kunde mbichi" ili wananchi waache kujadili suala la mgomo wa madaktari na wageukie suala la posho za wabunge? Ilikuwa ni mchezo uliopikwa ili kuwapumbaza Watanzania? Ina maana Ikulu na bunge waliamua kwa makusudi kuudanganya umma?! Je, inawezekana Ikulu kupitia Salva, Waziri Mkuu na Bunge waaamue kwa makusudi kuudanganya umma bila wewe kujua?! Ina maana uliridhia umma wako uliokuweka madarakani kudanganywa kwa makusudi? Au ndio ule usanii unaosemwa upo kwenye serikali yako? Kama sio usanii, tuite nini basi?

  Pamoja na kukutakia Salamu za Wapendanao, katu jambo hili halikubaliki hata kidogo katika dunia ya waungwana! Kwa jinsi inavyoonekana, ni ama Waziri Mkuu na Spika wa bunge walidanganya, au Salva alidanganya; au wote kwa ujumla wenu mlidanganya! Kama ambavyo Mheshimiwa Lowassa alipewa nafasi ya kutafakari kwa makini kwenye lile suala tata la Richmond kisha ndipo achukue maamuzi; basi bila shaka katika hili la kizungumkuti cha posho mnatakiwa kulitafakari kwa makini kisha mchukue maamuzi!

  Pamoja na yote hayo bado naendelea kukupenda Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu!? Lakini bado nina kila sababu ya kububujikwa na machozi! Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu; nashindwa kuiona busara ya serikali yako ya kuamua kuudanganya umma kwa lengo la kufunika kombe ili mwanaharamu apite! Pamoja na upendo nilionao kwako, lakini hili halikubaliki si tu duniani bali hadi ahera!

  Pamoja na yote hayo, ingawaje bado naendelea kububujikwa na machozi, bado ningependa kusema kwamba Happy Valentine, my Beloved H.E. Honarable Jakaya Mrisho Kikwete!
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Yaani unatarajia great thinkers tupoteze muda wetu kusoma ***** wote huu?
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hivi huwa hamna kazi kwa kuandika mihabari mireeeefu?
   
 4. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Na wewe huna kazi ku-comment mada ambayo hujaisoma?!
   
 5. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Yaani nawe unajiita ni Greatest Thinker?!
   
 6. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  Mi nimesoma ... wapo wengine watakao soma pia
   
 7. chubulunge

  chubulunge Senior Member

  #7
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  i dought
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  Naona kama nimepotea njia moja kwa moja.
   
 9. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sizani hapo ndo mwisho wako wa kufikiri.
   
 10. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  ndefu sana na unarudia yale yale! huna wa kumpenda katika familia yako au ndo kujipendekeza? hacha umwanaasha wewe! ukute hata mkeo au mmeo au babako au mamayako haujawatakia hata iyo v. day njema unaangaika na mtu asiyekujua! ambae hata ukifa hawezi hata kukuzika! ndo maana nkakwambia hacha umwanaasha!
   
 11. samito

  samito JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 621
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nimesoma ila nimeishia ktkt. ni nzur umepanga vizur inavutia kusoma naamin hata baba mwanaasha atasomewa endapo ataona uvivu kusoma.
   
 12. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280

  Hapa ni Jukwaa la Greatest Thinkers, nasikitika wewe si mmoja wao na ndio maana umeshindwa kuelewa na kuishia kubwabwaja!! Read btn lines, otherwise potezea!
   
 13. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Mwaaisha jk,be my vaalentine.
   
 14. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Aagh Baba mwanaasha umetisha!!
   
 15. gwankaja

  gwankaja JF-Expert Member

  #15
  Feb 14, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 1,950
  Likes Received: 1,586
  Trophy Points: 280
  aaaaaaaah aaaaaaah nimecheka sana eti u-mwanaasha
   
 16. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Umefanya vema kuonyesha hisia zako. Hata kama hakujui, ujumbe umefika!
   
 17. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #17
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Haka kajamaa kanafiki kweli haya ndo mahaba ya msimu anayosema Ole sendeka, sioni mantiki ya kumpondea kutokana na udhaifu wa serikali yake then unasema unampenda. Unampenda kwa lipi??? Unafiki mkubwa, huna tofauti na wale wanaosena Mh spika awali ya yote naunga mkono hoja 100% lakini...........................
   
 18. n

  ngokowalwa Senior Member

  #18
  Feb 14, 2012
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kweli kabisa huna haja ku comment mada ambayo hujisoma , binafsi baada ya kupitia mstari kwa mstari nimeona mwandishi wa mada ametoa ujumbe mzito sana wenye kugusa jamii yetu ya kitz kwa ujumla .
   
 19. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #19
  Feb 14, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280

  Inabidi ifike wakati tukubali kwamba ili mtu aweze kuzielewa baadhi ya nyuzi za humu JF basi ni ama awe amebalehe enzi za utawala wa Mwalimu au Mzee Mwinyi....na amechelewa sana labda awe amepata baleghe enzi za Mkapa! Lakini kama ni balehe za enzi za JK, nyuzi za JF ni ngumu kueleweka unless uwe REAL GREATEST THINKER!!!
   
 20. MANI

  MANI Platinum Member

  #20
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jasusi bila kusoma utajuaje mambo? Kusoma ndio mwanzo wa uelewa. @Nasdaz ujumbe wako murua mwenye masikio na asikie!
   
Loading...