Happy Valentine H.E Jakaya Mrisho Kikwete!

Inabidi ifike wakati tukubali kwamba ili mtu aweze kuzielewa baadhi ya nyuzi za humu JF basi ni ama awe amebalehe enzi za utawala wa Mwalimu au Mzee Mwinyi....na amechelewa sana labda awe amepata baleghe enzi za Mkapa! Lakini kama ni balehe za enzi za JK, nyuzi za JF ni ngumu kueleweka unless uwe REAL GREATEST THINKER!!!

Mkuu hawa wanafikiri ni fb ambapo watu huandika mistari miwili tu !
 
Hapa ni Jukwaa la Greatest Thinkers, nasikitika wewe si mmoja wao na ndio maana umeshindwa kuelewa na kuishia kubwabwaja!! Read btn lines, otherwise potezea!

Great Thinkers hawana muda wa kusoma utumbo! Hit the point!
 
Inabidi ifike wakati tukubali kwamba ili mtu aweze kuzielewa baadhi ya nyuzi za humu JF basi ni ama awe amebalehe enzi za utawala wa Mwalimu au Mzee Mwinyi....na amechelewa sana labda awe amepata baleghe enzi za Mkapa! Lakini kama ni balehe za enzi za JK, nyuzi za JF ni ngumu kueleweka unless uwe REAL GREATEST THINKER!!!

you are very right mkuu, watu wamezoe zile za 'like' au niko ... Nakula nyama choma, ambazo wanaandika kule FB na Twita!
 
Great Thinkers hawana muda wa kusoma utumbo! Hit the point!

Umejuaje kwamba ni utumbo wakati hujasoma?! Hakuna Greatest Thinker aliye mvivu wa kusoma unless kama ni greatest thinker wa facebook!!!
 
  • Thanks
Reactions: Taz
happy valentine mwanaasha jakaya kikwete.......japo shule imekuwa ngumu, waweza jaribu hii...
 
Mkuu ujumbe umefika hata asipo usoma mh basi walio comet negative watamfikishia tu kwani imewauma

"ukitaka kuwaficha kitu watanzania kiweke kwenye maandishi " wanaolalamika ni ujumbe mrefu mno wapo gizani japokua ni mchana

mkuu you are a great thinker, mtu hovyo hovyo hawezi kuulewa ujumbe huu hata kidogo
 
Pamoja na kuwapo kwa ugumu wa maisha na kuwa kama tuliochanganyikiwa lakini sijafikia kiwango cha kusahau kukutumia salama zangu za wapendanao (au za wapendao?) leo hii, bila kusubiri “mwaisha bora” uliyotuahidi! Si wewe peke yako, bali na chama chama chako Chama Cha Mapinduzi a.k.a CCM!

Happy Valentine H.E. Honarable Jakaya Mrisho Kikwete!

Pamoja na yote hayo bado kuna jambo linanishangaza Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu! Wakati naandika salamu zangu kwako taratibu najikuta nikibubujikwa na machozi! Kwanini? Najiuliza kwa haraka haraka kisa cha chozi langu kati kati ya salamu zangu za upendo kwako! Hata hivyo, nakosa jibu! Nafahamu, wengi wapendao hujikuta wakibubujikwa na machozi pale wanapozielezea hisia zao! Hapo ndipo ninapozinduka na kuukumbuka wimbo wa mwanamuziki wa kizazi kipya, Hamisi Mwijuma au Mwana FA uitwao Hawajui Tulikotoka! Je, Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu huwa unapata muda wa kuwasikiliza hawa vijana? Usiwasikilize wale wasioupenda muziki huu kwamba hamna chochote wanachoimba! Kuna kijana mwingine, kwa kupitia muziki huu huu amemtuma Ridhiwan eti aje kuongea na wewe! Sitaki kuamini kwamba vijana hawa wamefikia hatua ya kuamini kwamba wakikueleza wewe moja kwa moja hutawasikiliza hata waamue kumtumia kijana wako Ridhiwan! Nakupenda Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu hivyo sipendi kuona wala kusikia watu wakikusema vibaya! Hivyo basi, endapo ni kweli pamejengwa ukuta katikati yako na wananchi basi ni heri ukuta huo ukabomolewa mapema na kujengwa daraja kama njia moja wapo ya kusikiliza ushauri wa Mjomba Mrisho Mpoto aliyewahi kukueleza kabla kwamba “heri kujengwa daraja kuliko ukuta....”

Salale! Inawezekana hivi sasa naelekea kuchanganyikiwa kwani tayari nilishasahau ni nini hasa nilipanga kukueleza hapo juu! Kama nilivyokueleza hapo juu kwamba baada ya kuzinduka ndipo nikagundua kwamba huenda chozi langu linafanana na yale ambayo Mwana FA alipata kuyaongea kwenye wimbo wake. Mtu anapenda huku akiteswa vikali na ampendae! Utakosa vipi kumwaga machozi wakati unapomtumia Salamu za Wapendanao!?

Eti Wamachinga na Wandengereko nao walikuwa na mpango wa kumtuma Mama Salma eti aje kukupa ujumbe kama alivyoagizwa Ridhiwani! Nikawapoza, nikawaambia ujumbe wao kwako nitaweza kuuleta hata mimi! Wametamka bayana kwamba hili la kuongeza posho za wabunge kwa malaki katu halikubaliki hata chembe! Nami naungana nao, isitoshe sina namna kwani tayari wameshanibebesha msalaba ili nikufikishie ujumbe huo. Ni kweli, pamoja na upendo wangu kwako Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu, kwa hili la hapana!

Hata hivyo, wakati nikisisitiza kwamba suala hilo halikubaliki, bado kuna lingine linaendelea kuelelea akilini mwangu! Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu, hivi ilikuwaje kuhusu mkanganyiko wa posho uliokuwa umejitokeza hivi majuzi katikati ya mgomo wa madaktari?! Mheshimiwa Rais wangu, kumbuka kwamba nakupenda kwa dhati! Hivi una habari kwamba wale wenye vijiba vya roho wanakuita msanii? Yaani Rais wa nchi awe msanii; hapana! Sitaki kuamini, na isitoshe tayari katiba mbovu iliyopo inanilazimisha kumtii rais wa JMT! Mimi ni raia mzalendo niliyekata shauri la kuilinda katiba yetu hata kama nyie mliyeapa kufanya hivyo mnakwenda kinyume na viapo vyenu! Hivyo basi, kwangu mimi kumwita rais ni msanii ni kuvunja katiba kwani hiyo katu haiwezi kuwa utii! Pamoja na hayo, jaribu kukanusha japo kidogo.

Je, ni kweli, Mheshimiwa Rais wangu wewe binafsi na serikali yako ni wasanii?! Hebu fikiria, katikatika ya mgomo wa madaktari Mheshimiwa Waziri Mkuu akatangaza kwamba posho za wabunge zimepanda toka Sh.70,000/= hadi Sh.200,000/=! Papo hapo, Spika wa Bunge nae akathibitisha kwamba Mheshimiwa Rais wangu, nikupendae umeridhia kupanda kwa posho hizo! Ghafla, kijana wako Salva Rweymamu akaja na taarifa kwamba katu hujaridhia kupanda kwa posho hizo na kwamba ulichokuwa umeagiza ni kutumika kwa busara katika kushughulia suala hilo la posho!!! Haya sasa, Mheshimiwa Rais wangu nikupendae; naomba unisaidie katika hili ili upendo wangu kwako usiwe na doa. Kama kweli uliagiza busara itumike katika kushughulikia posho za wabunge; je, Waziri Mkuu alitumia busara gani kutangaza kupanda kwa posho wakati madaktari wakiwa katikati ya mgomo wa kudai maslahi zaidi?! Huoni kama alikuwa anakuchonganisha na madaktari pamoja na wananchi ili uonekane unajali maslahi ya wabunge wachache na kuwadharau madaktari na ulifanya hivyo huku wapiga kura wako wakiwa wanakufa kwa kukosa huduma?! Mheshimiwa Raisi wangu, hivi huoni kwamba Mheshimiwa Waziri Mkuu na Spika wa Bunge waliamua kukuhujumu kwa makusudi ili uchukiwe na wananchi?!

Mheshimiwa Rais wangu, sipendi niwe mnafiki! Kwa mara ya kwanza, nilianza kujenga chuki dhidi yako pale niliposikia kwamba umeridhia uongezaji wa posho za wabunge wakati wananchi wakiwa wanakufa kwa kukosa huduma za madaktari! Sasa Mheshimiwa Rais wangu; ikiwa mie nikupendae tayari nilishaanza kujenga chuki dhidi yako; je wale ambao tangu hapo hawakupendi?! Usisahau Mheshimiwa rais wangu kwamba, nazitoa salamu zangu hizi za Valentine kwako wakati bado nabubujikwa na machozi! Ni kweli uliwaambia waheshimiwa wenzako kwamba watumie busara? Na kama ni kweli, mbona waliamua kukuhujumu?! Vipi unaikumbatia hujuma kubwa kama hiyo toka kwa watendaji wako wakuu? Na kama kweli uliwaagiza watumie busara, mbona walidai kwamba uliridhia Mheshimiwa rais wangu? Ina maana waliamua kuudanganya umma uliokupigia kura na kukupa ridhaa ya uongozi?! Inakuwaje basi bado unaendelea kufanya kazi na viongozi ambao ama ni waongo na wazushi wakubwa au wahujumu wakubwa wa uongozi wako?! Nijuavyo, kama ni kweli uliwaagiza watumie busara, basi Mheshimiwa Waziri Mkuu na Spika wa Bunge ni wahujumu wakubwa waliokusudia kukuhujumu wewe binafsi na vile vile ni waongo na wazushi wakubwa waliokusudia kuwadanganya watanzania. Yote kwa yote, hizo ni sifa mbaya kabisa ambazo katu kiongozi awe wa umma au vinginevyo, hastahili kuwa nazo! Sasa Mheshimiwa Rais wangu mbona bado unaendelea kufanya nao kazi?!

Mheshimwa Rais wangu Mpendwa, au ni Salva? Ni kijana wako Salva Rweymamu ndiye muongo? Je, ni kweli uliridhia kupandishwa kwa posho za wabunge lakini ni Salva ndie muongo aliyesema kwamba hukuridhia? Kama muongo ni huyo Salva, ni kwanini basi aliamua kuwadhalilisha Mheshimiwa Waziri Mkuu na Spika wa Bunge hata waonekane ni wazushi wakati ukweli ni kwamba ulisharidhia? Ni wapi Salva alipata ujasiri wa kuwadhalilisha viongozi wakuu wa nchi hii kwa kuwaonesha mbele ya jamii kwamba ni waongo?! Na ni wapi Salva alipata ujasiri wa kukuzushia bosi wake uongo? Kama kweli uliridhia, halafu Salva anasema hukuridhia; basi hapo maana yake ni kwamba anakuzushia uongo! Sasa, Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu; inakuwaje unaendelea kufanya kazi na Salva muongo, mzushi na mchonganishi?! Kama Salva ni muongo, mzushi na mchinganishi kiasi hicho; ni kwanini basi usimfute kazi mara moja?! Au ni kweli Mheshimiwa Rais wangu wewe ni legelege?! Haiwezekani; yaani Luteni wa jeshi awe legelege?! Sasa mbona huchukui maamjuzi dhidi ya huyu Salva muongo?!

Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu. Lengo langu si kusutana, bali ni kukutakia Salamu za Wapendanao....Happy Valentine H.E. Honorable Presdient Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete. Hata hivyo, bado unanichanganya Mheshimiwa rais wangu! Au lile suala la kupanda kwa posho lilikuwa ni “danganya toto kula kunde mbichi” ili wananchi waache kujadili suala la mgomo wa madaktari na wageukie suala la posho za wabunge? Ilikuwa ni mchezo uliopikwa ili kuwapumbaza Watanzania? Ina maana Ikulu na bunge waliamua kwa makusudi kuudanganya umma?! Je, inawezekana Ikulu kupitia Salva, Waziri Mkuu na Bunge waaamue kwa makusudi kuudanganya umma bila wewe kujua?! Ina maana uliridhia umma wako uliokuweka madarakani kudanganywa kwa makusudi? Au ndio ule usanii unaosemwa upo kwenye serikali yako? Kama sio usanii, tuite nini basi?

Pamoja na kukutakia Salamu za Wapendanao, katu jambo hili halikubaliki hata kidogo katika dunia ya waungwana! Kwa jinsi inavyoonekana, ni ama Waziri Mkuu na Spika wa bunge walidanganya, au Salva alidanganya; au wote kwa ujumla wenu mlidanganya! Kama ambavyo Mheshimiwa Lowassa alipewa nafasi ya kutafakari kwa makini kwenye lile suala tata la Richmond kisha ndipo achukue maamuzi; basi bila shaka katika hili la kizungumkuti cha posho mnatakiwa kulitafakari kwa makini kisha mchukue maamuzi!

Pamoja na yote hayo bado naendelea kukupenda Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu!? Lakini bado nina kila sababu ya kububujikwa na machozi! Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu; nashindwa kuiona busara ya serikali yako ya kuamua kuudanganya umma kwa lengo la kufunika kombe ili mwanaharamu apite! Pamoja na upendo nilionao kwako, lakini hili halikubaliki si tu duniani bali hadi ahera!

Pamoja na yote hayo, ingawaje bado naendelea kububujikwa na machozi, bado ningependa kusema kwamba Happy Valentine, my Beloved H.E. Honarable Jakaya Mrisho Kikwete!

Mmh haya
 
Mkuu, umetisha kwa salamu zako za valentine day kwa baba mwanaasha, pia naimani ujumbe utamfikia.

kuanzia ile siku JK alipoamua kupretend kwamba mgomo wa drs hauna maana na kukazania kwenda kwenye misiba, mie nilikamilisha kumpa divisheni sawa kabisa na ya binti mmoja almaaruf katika majibu ya fom four

TO ME I REGARD MYSELF KWAMBA SINA RAIS TENA!!
 
kuanzia ile siku JK alipoamua kupretend kwamba mgomo wa drs hauna maana na kukazania kwenda kwenye misiba, mie nilikamilisha kumpa divisheni sawa kabisa na ya binti mmoja almaaruf katika majibu ya fom four

TO BE I REGARD MYSELF KWAMBA SINA RAIS TENA!!
Lakini umesahau "tradition" ya Watanzania, wanamjali mfu zaidi ya mtu aliye mzima, mgonjwa mwenye uwezekano wa kutibiwa na kupona?
Kwa taarifa yake na serikali yake, hakuna rangi wataacha kuona kama madai ya madaktari watayapuuza na kudhani ni business as usual!
 
Pamoja na kuwapo kwa ugumu wa maisha na kuwa kama tuliochanganyikiwa lakini sijafikia kiwango cha kusahau kukutumia salama zangu za wapendanao (au za wapendao?) leo hii, bila kusubiri "mwaisha bora" uliyotuahidi! Si wewe peke yako, bali na chama chama chako Chama Cha Mapinduzi a.k.a CCM!

Happy Valentine H.E. Honarable Jakaya Mrisho Kikwete!

Pamoja na yote hayo bado kuna jambo linanishangaza Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu! Wakati naandika salamu zangu kwako taratibu najikuta nikibubujikwa na machozi! Kwanini? Najiuliza kwa haraka haraka kisa cha chozi langu kati kati ya salamu zangu za upendo kwako! Hata hivyo, nakosa jibu! Nafahamu, wengi wapendao hujikuta wakibubujikwa na machozi pale wanapozielezea hisia zao! Hapo ndipo ninapozinduka na kuukumbuka wimbo wa mwanamuziki wa kizazi kipya, Hamisi Mwijuma au Mwana FA uitwao Hawajui Tulikotoka! Je, Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu huwa unapata muda wa kuwasikiliza hawa vijana? Usiwasikilize wale wasioupenda muziki huu kwamba hamna chochote wanachoimba! Kuna kijana mwingine, kwa kupitia muziki huu huu amemtuma Ridhiwan eti aje kuongea na wewe! Sitaki kuamini kwamba vijana hawa wamefikia hatua ya kuamini kwamba wakikueleza wewe moja kwa moja hutawasikiliza hata waamue kumtumia kijana wako Ridhiwan! Nakupenda Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu hivyo sipendi kuona wala kusikia watu wakikusema vibaya! Hivyo basi, endapo ni kweli pamejengwa ukuta katikati yako na wananchi basi ni heri ukuta huo ukabomolewa mapema na kujengwa daraja kama njia moja wapo ya kusikiliza ushauri wa Mjomba Mrisho Mpoto aliyewahi kukueleza kabla kwamba "heri kujengwa daraja kuliko ukuta...."

Salale! Inawezekana hivi sasa naelekea kuchanganyikiwa kwani tayari nilishasahau ni nini hasa nilipanga kukueleza hapo juu! Kama nilivyokueleza hapo juu kwamba baada ya kuzinduka ndipo nikagundua kwamba huenda chozi langu linafanana na yale ambayo Mwana FA alipata kuyaongea kwenye wimbo wake. Mtu anapenda huku akiteswa vikali na ampendae! Utakosa vipi kumwaga machozi wakati unapomtumia Salamu za Wapendanao!?

Eti Wamachinga na Wandengereko nao walikuwa na mpango wa kumtuma Mama Salma eti aje kukupa ujumbe kama alivyoagizwa Ridhiwani! Nikawapoza, nikawaambia ujumbe wao kwako nitaweza kuuleta hata mimi! Wametamka bayana kwamba hili la kuongeza posho za wabunge kwa malaki katu halikubaliki hata chembe! Nami naungana nao, isitoshe sina namna kwani tayari wameshanibebesha msalaba ili nikufikishie ujumbe huo. Ni kweli, pamoja na upendo wangu kwako Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu, kwa hili la hapana!

Hata hivyo, wakati nikisisitiza kwamba suala hilo halikubaliki, bado kuna lingine linaendelea kuelelea akilini mwangu! Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu, hivi ilikuwaje kuhusu mkanganyiko wa posho uliokuwa umejitokeza hivi majuzi katikati ya mgomo wa madaktari?! Mheshimiwa Rais wangu, kumbuka kwamba nakupenda kwa dhati! Hivi una habari kwamba wale wenye vijiba vya roho wanakuita msanii? Yaani Rais wa nchi awe msanii; hapana! Sitaki kuamini, na isitoshe tayari katiba mbovu iliyopo inanilazimisha kumtii rais wa JMT! Mimi ni raia mzalendo niliyekata shauri la kuilinda katiba yetu hata kama nyie mliyeapa kufanya hivyo mnakwenda kinyume na viapo vyenu! Hivyo basi, kwangu mimi kumwita rais ni msanii ni kuvunja katiba kwani hiyo katu haiwezi kuwa utii! Pamoja na hayo, jaribu kukanusha japo kidogo.

Je, ni kweli, Mheshimiwa Rais wangu wewe binafsi na serikali yako ni wasanii?! Hebu fikiria, katikatika ya mgomo wa madaktari Mheshimiwa Waziri Mkuu akatangaza kwamba posho za wabunge zimepanda toka Sh.70,000/= hadi Sh.200,000/=! Papo hapo, Spika wa Bunge nae akathibitisha kwamba Mheshimiwa Rais wangu, nikupendae umeridhia kupanda kwa posho hizo! Ghafla, kijana wako Salva Rweymamu akaja na taarifa kwamba katu hujaridhia kupanda kwa posho hizo na kwamba ulichokuwa umeagiza ni kutumika kwa busara katika kushughulia suala hilo la posho!!! Haya sasa, Mheshimiwa Rais wangu nikupendae; naomba unisaidie katika hili ili upendo wangu kwako usiwe na doa. Kama kweli uliagiza busara itumike katika kushughulikia posho za wabunge; je, Waziri Mkuu alitumia busara gani kutangaza kupanda kwa posho wakati madaktari wakiwa katikati ya mgomo wa kudai maslahi zaidi?! Huoni kama alikuwa anakuchonganisha na madaktari pamoja na wananchi ili uonekane unajali maslahi ya wabunge wachache na kuwadharau madaktari na ulifanya hivyo huku wapiga kura wako wakiwa wanakufa kwa kukosa huduma?! Mheshimiwa Raisi wangu, hivi huoni kwamba Mheshimiwa Waziri Mkuu na Spika wa Bunge waliamua kukuhujumu kwa makusudi ili uchukiwe na wananchi?!

Mheshimiwa Rais wangu, sipendi niwe mnafiki! Kwa mara ya kwanza, nilianza kujenga chuki dhidi yako pale niliposikia kwamba umeridhia uongezaji wa posho za wabunge wakati wananchi wakiwa wanakufa kwa kukosa huduma za madaktari! Sasa Mheshimiwa Rais wangu; ikiwa mie nikupendae tayari nilishaanza kujenga chuki dhidi yako; je wale ambao tangu hapo hawakupendi?! Usisahau Mheshimiwa rais wangu kwamba, nazitoa salamu zangu hizi za Valentine kwako wakati bado nabubujikwa na machozi! Ni kweli uliwaambia waheshimiwa wenzako kwamba watumie busara? Na kama ni kweli, mbona waliamua kukuhujumu?! Vipi unaikumbatia hujuma kubwa kama hiyo toka kwa watendaji wako wakuu? Na kama kweli uliwaagiza watumie busara, mbona walidai kwamba uliridhia Mheshimiwa rais wangu? Ina maana waliamua kuudanganya umma uliokupigia kura na kukupa ridhaa ya uongozi?! Inakuwaje basi bado unaendelea kufanya kazi na viongozi ambao ama ni waongo na wazushi wakubwa au wahujumu wakubwa wa uongozi wako?! Nijuavyo, kama ni kweli uliwaagiza watumie busara, basi Mheshimiwa Waziri Mkuu na Spika wa Bunge ni wahujumu wakubwa waliokusudia kukuhujumu wewe binafsi na vile vile ni waongo na wazushi wakubwa waliokusudia kuwadanganya watanzania. Yote kwa yote, hizo ni sifa mbaya kabisa ambazo katu kiongozi awe wa umma au vinginevyo, hastahili kuwa nazo! Sasa Mheshimiwa Rais wangu mbona bado unaendelea kufanya nao kazi?!

Mheshimwa Rais wangu Mpendwa, au ni Salva? Ni kijana wako Salva Rweymamu ndiye muongo? Je, ni kweli uliridhia kupandishwa kwa posho za wabunge lakini ni Salva ndie muongo aliyesema kwamba hukuridhia? Kama muongo ni huyo Salva, ni kwanini basi aliamua kuwadhalilisha Mheshimiwa Waziri Mkuu na Spika wa Bunge hata waonekane ni wazushi wakati ukweli ni kwamba ulisharidhia? Ni wapi Salva alipata ujasiri wa kuwadhalilisha viongozi wakuu wa nchi hii kwa kuwaonesha mbele ya jamii kwamba ni waongo?! Na ni wapi Salva alipata ujasiri wa kukuzushia bosi wake uongo? Kama kweli uliridhia, halafu Salva anasema hukuridhia; basi hapo maana yake ni kwamba anakuzushia uongo! Sasa, Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu; inakuwaje unaendelea kufanya kazi na Salva muongo, mzushi na mchonganishi?! Kama Salva ni muongo, mzushi na mchinganishi kiasi hicho; ni kwanini basi usimfute kazi mara moja?! Au ni kweli Mheshimiwa Rais wangu wewe ni legelege?! Haiwezekani; yaani Luteni wa jeshi awe legelege?! Sasa mbona huchukui maamjuzi dhidi ya huyu Salva muongo?!

Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu. Lengo langu si kusutana, bali ni kukutakia Salamu za Wapendanao....Happy Valentine H.E. Honorable Presdient Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete. Hata hivyo, bado unanichanganya Mheshimiwa rais wangu! Au lile suala la kupanda kwa posho lilikuwa ni "danganya toto kula kunde mbichi" ili wananchi waache kujadili suala la mgomo wa madaktari na wageukie suala la posho za wabunge? Ilikuwa ni mchezo uliopikwa ili kuwapumbaza Watanzania? Ina maana Ikulu na bunge waliamua kwa makusudi kuudanganya umma?! Je, inawezekana Ikulu kupitia Salva, Waziri Mkuu na Bunge waaamue kwa makusudi kuudanganya umma bila wewe kujua?! Ina maana uliridhia umma wako uliokuweka madarakani kudanganywa kwa makusudi? Au ndio ule usanii unaosemwa upo kwenye serikali yako? Kama sio usanii, tuite nini basi?

Pamoja na kukutakia Salamu za Wapendanao, katu jambo hili halikubaliki hata kidogo katika dunia ya waungwana! Kwa jinsi inavyoonekana, ni ama Waziri Mkuu na Spika wa bunge walidanganya, au Salva alidanganya; au wote kwa ujumla wenu mlidanganya! Kama ambavyo Mheshimiwa Lowassa alipewa nafasi ya kutafakari kwa makini kwenye lile suala tata la Richmond kisha ndipo achukue maamuzi; basi bila shaka katika hili la kizungumkuti cha posho mnatakiwa kulitafakari kwa makini kisha mchukue maamuzi!

Pamoja na yote hayo bado naendelea kukupenda Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu!? Lakini bado nina kila sababu ya kububujikwa na machozi! Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu; nashindwa kuiona busara ya serikali yako ya kuamua kuudanganya umma kwa lengo la kufunika kombe ili mwanaharamu apite! Pamoja na upendo nilionao kwako, lakini hili halikubaliki si tu duniani bali hadi ahera!

Pamoja na yote hayo, ingawaje bado naendelea kububujikwa na machozi, bado ningependa kusema kwamba Happy Valentine, my Beloved H.E. Honarable Jakaya Mrisho Kikwete!

Mpelekee salamu na Bi. Mwanaasha Jakaya Kikwete!!!
 
Back
Top Bottom