Happy Valentine H.E Jakaya Mrisho Kikwete!

Happy Valentine H.E Jakaya Mrisho Kikwete!

Pamoja na kukutakia Salamu za Wapendanao, katu jambo hili halikubaliki hata kidogo katika dunia ya waungwana! Kwa jinsi inavyoonekana, ni ama Waziri Mkuu na Spika wa bunge walidanganya, au Salva alidanganya; au wote kwa ujumla wenu mlidanganya! Kama ambavyo Mheshimiwa Lowassa alipewa nafasi ya kutafakari kwa makini kwenye lile suala tata la Richmond kisha ndipo achukue maamuzi; basi bila shaka katika hili la kizungumkuti cha posho mnatakiwa kulitafakari kwa makini kisha mchukue maamuzi!

Lakini bado nina kila sababu ya kububujikwa na machozi! Mheshimiwa, Mpendwa Rais wangu; nashindwa kuiona busara ya serikali yako ya kuamua kuudanganya umma kwa lengo la kufunika kombe ili mwanaharamu apite!



Hili anapaswa kulitekeleza haraka sanaaa!!
 
Mpelekee salamu na Bi. Mwanaasha Jakaya Kikwete!!!

Happy Valentine Mpendwa wetu Mwanaasha Jakaya Kikwete!! Achana na hawa mavuvuzela wa JF waliokomalia wewe mpendwa kupata Division Four!! Wanasumbuliwa na husuda tu hawa!! Baba zao waliigusa hata hiyo form four?! Hawana jema hawa, ungepiga Divison One wangesema tu; oh, Mwanaasha alifanyia paper home wakisaidiana na Riz1....!!! Mijitu mingine bana, kwani Division Four kuoneshwa kwenye matokeo ndo lazima cheti nacho kiandikwe Division Four!!! Hawajui hawa kwamba umepiga One ya nguvu, sema kwa kuhofia vidomodomo vyao kwamba paper ulifanyia home, m-sure akaamuru matokeo yaandikwe Div. Four lakini ile One yako kali itaandikwa kwenye cheti chako mwaya na baada ya hapo unaenda kwenye bonge la shule la A-Level!! Mijitu mingine inasubiria kuona eti unaenda kusomea teaching !!!! Yaani hadi leo haijui kwamba ulijifanyisha tu...??!!! Watu wana husuda hadi basi....m-sure presdaa, braza Riz akijihusisha na politics wanasema uongozi wa kurithishana .....sasa mbona wanataka ukasomee teaching wakati madha nae ni teacher?! si ndo kurithishana kulekule wanakopinga?! happy valentine mwaya; see u!!

 
Back
Top Bottom