Happy born day PIERLUIGI COLLINA

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,904
PIERLUIGI COLLINA kitu ambacho hatasahau zaidi kwenye kazi yake u referee: "Tulikuwa katika dakika mbili za mwisho za fainali ya Ligi ya Mabingwa na niliwaona wachezaji wa Bayern wakiwa kwenye benchi tayari kusherehekea ubingwa wao. Mashabiki walikuwa wanaekumbatiana kwenye viti kiwanjani wakisubiri filimbi yangu,ya mwisho.

Ghafla, Manchester United wanafunga mabao mawili ndani ya dakika mbili na Kubadili matokeo. Sitasahau furaha ya wachezaji na benchi la Manchester united, walionekana kama simba wanaounguruma, kabla ya ukimya mkubwa upande wa Bayern. wachezaji wa United walikimbia kama wazimu kwenye nyasi, huku nikimwona mchezaji wa Bayern amelala akilia, bila tumaini, na kukata tamaa sana.

- Nilimkaribia, lakini sikuweza kufikiria kitu kingine chochote cha kumwambia zaidi ya kumwambia "Simama na upambane , bado una sekunde 20! lakini wakati huo niliona sura halisi ya soka, ambapo wachezaji walijitolea maisha yao yote uwanjani, huku watu wakipiga kelele za furaha na wengine wakiwa na roho zilizochubuka.”

-SIKU NJEMA YA KUZALIWA KWA MWAMUZI PEKEE AMBAYE VAR IMEUNGANISHWA KATIKA MUONEKANO WAKE: PIERLUIGI COLLINA,Happy birthday Mwamuzi Bora Wa muda wote
IMG-20240220-WA0009.jpg
 
PIERLUIGI COLLINA kitu ambacho hatasahau zaidi kwenye kazi yake u referee: "Tulikuwa katika dakika mbili za mwisho za fainali ya Ligi ya Mabingwa na niliwaona wachezaji wa Bayern wakiwa kwenye benchi tayari kusherehekea ubingwa wao. Mashabiki walikuwa wanaekumbatiana kwenye viti kiwanjani wakisubiri filimbi yangu,ya mwisho.

Ghafla, Manchester United wanafunga mabao mawili ndani ya dakika mbili na Kubadili matokeo. Sitasahau furaha ya wachezaji na benchi la Manchester united, walionekana kama simba wanaounguruma, kabla ya ukimya mkubwa upande wa Bayern. wachezaji wa United walikimbia kama wazimu kwenye nyasi, huku nikimwona mchezaji wa Bayern amelala akilia, bila tumaini, na kukata tamaa sana.

- Nilimkaribia, lakini sikuweza kufikiria kitu kingine chochote cha kumwambia zaidi ya kumwambia "Simama na upambane , bado una sekunde 20! lakini wakati huo niliona sura halisi ya soka, ambapo wachezaji walijitolea maisha yao yote uwanjani, huku watu wakipiga kelele za furaha na wengine wakiwa na roho zilizochubuka.”

-SIKU NJEMA YA KUZALIWA KWA MWAMUZI PEKEE AMBAYE VAR IMEUNGANISHWA KATIKA MUONEKANO WAKE: PIERLUIGI COLLINA,Happy birthday Mwamuzi Bora Wa muda woteView attachment 2909702
Linapokuja suala la uamuzi,hakika huyu alikuwa mwamba
 
99 hii uefa champions league, samuel kuffor alilia kama mtoto mdogo, wakati mwingine soka lina matokeo ya kikatili saana, maumivu haya huwa wanapata wabetiji, mtu anasubiri milioni 40 halafu jiooooni mambo yanabadilika,

Mtu aliyeweza kumudu game ya kubeti, aliyeipenda arsenal ile ya wenger mwishoni na hapa katikati huyo yupo certified kuingia kwenye NDOA 🤣😂
 
Sammy Kuffor huyu mwamba sidhani kama atakuja kuisahau hiyo game....Sometimes mpira una matokeo ya kikatili nakumbuka Moscow final 2008 Man Utd vS Chelsea pale captain John Tery anakosa penalty na kuwakosesha the blues fursa ya kubeba Champions league kwa mara ya kwanza
 
99 hii uefa champions league, samuel kuffor alilia kama mtoto mdogo, wakati mwingine soka lina matokeo ya kikatili saana, maumivu haya huwa wanapata wabetiji, mtu anasubiri milioni 40 halafu jiooooni mambo yanabadilika,

Mtu aliyeweza kumudu game ya kubeti, aliyeipenda arsenal ile ya wenger mwishoni na hapa katikati huyo yupo certified kuingia kwenye NDOA
Solskajaer anatokea benchi anafunga goli la pili biashara inaishia hapo...

Wenger kutokubeba hili kombe nilimuona hana maana kabisa, ushindani ulikuwa mdogo wakati ule tofauti na sasa, ajabu akafika fainali moja tu aliyopigwa na Barca Ufaransa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Mpira una mambo ya kikatili.

Niliwahi kusikia kuna mchezaji alidaka makusudi mpira uliokuwa unaingia golini, huyo mchezaji akapata red card halafu jamaa wakapata penalt ili wafunge goli lao.

Bahati mbaya wakaikosa hiyo bahati na huyo mchezaji aliyedaka mpira kwa makusudi akawa shujaa kwa kuwaokoa.
 
Siyo yule mla watu suarez?
 
Ushindani haujawahi kuwa mdogo.
Wenger timu yake bora kabisa ilikuwa ndio hiyo kuanzia 2000 hivi mpaka 2006, baada ya hapo hakuwa na timu ya maana
 
Hii ni 2010 pale kwa Madiba South, mchezaji alikua Suarez kima yule
 
Ushindani haujawahi kuwa mdogo.
Wenger timu yake bora kabisa ilikuwa ndio hiyo kuanzia 2000 hivi mpaka 2006, baada ya hapo hakuwa na timu ya maana
Naamini ushidani ulikuwa mdogo, wakati ule ukiondoa Bayern Munich, Man Utd, na Barca, hapakuwepo na timu nyingine ngumu kama ilivyo sasa. Hata R. Madrid ya wakati ule haikuwa moto.

Angalia leo, kuna Man City, R. Madrid, Atletico Madrid, Inter Milan, Bayern, na nyingine kibao hapo timu inaweza kutolewa na nyingine yoyote.. sijawaweka kina Dortmund, PSG, kubeba UEFA siku hizi ni mtihani mara mbili ya ule wa enzi zile..

Mbona unawatoa kina ac Milan, juventus n.k hao walikuwa moto pia
Huku huku kwenye hizi timu bora madrid kabeba mara 3 mfululizo tofauti na enzi hizo ambazo unasema timu zilikuwa mdebwedo
 
Mpira una mambo ya kikatili.

Niliwahi kusikia kuna mchezaji alidaka makusudi mpira uliokuwa unaingia golini, huyo mchezaji akapata red card halafu jamaa wakapata penalt ili wafunge goli lao.

Bahati mbaya wakaikosa hiyo bahati na huyo mchezaji aliyedaka mpira kwa makusudi akawa shujaa kwa kuwaokoa.
mchezaji alikua luis suarez, world cup ya 2010 south africa!nusu final vs Ghana!Asamoah Gyan anakosa penalt
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom