Natafuta Ajira
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 4,425
- 9,822
Ulifata mkondo wa wazazi /ndugu, ulivutiwa na mchezaji wa timu husika, kuna tukio la kufurahisha au kuuzunisha lililikufanya uipende timu yako?
Binafsi nimeanza kufatilia mpira nikiwa na miaka 6 mwaka 1998 kipindi cha world cup. Kabla ya hapo sikua shabiki wa kuangalia mpira ingawa nilikua naucheza na marafiki mtaani na shuleni. Ule mkusanyiko wa watu na vibe wakati wa mechi nami nikawa najumuika ndipo nakaanza kuwa shabiki wa soka
Baada ya world cup kuisha nikawa nafuatilia zaidi ligi ya uingereza kwa kipindi hicho ilikua inaoneshwa majumbani nimesahau chanel gani ila ni DTV au CTN, nilikua nawafatilia zaidi wachezaji waliokuwepo kwenye world cup kama beckham, owen, henry, berkamp n.k.
Wachezaji waliovuma world cup ila hawachezi ligi ya uingereza kama Ronaldo de lima, Zidane, Rivaldo n.k nilikua nawafatilia kupitia uefa champions league kwa kipindi hicho ilikua inaoneshwa ITV. Timu ninazoshabia kwa sasa ni Yanga na Manchester United. Nilianzaje kuzipenda izo timu?
YANGA: Miaka ya 90 mwishoni kuelekea 2000 kuna binamu yangu alitoka kijijini kuja dar tukawa tunaishi nae nyumbani, alikua anaipenda sana simba kila mechi ya simba au yanga lazima asikilize redioni kila siku jioni anasikiliza kipindi cha michezo redio 1 kilikua kinatangazwa na Maulid Kitenge. Kipindi kinaanza na kibwagizo utasikia "maulid baraka wa kitenge jezi nambari 9 mgongoni alalalala goooooo".
Nikajenga mazoea ya kusikiliza nae mpira redioni katika mechi za yanga nilikua nasikia sana jina la Lunyamila kuashiria anawapeleka puta mabeki uko uwanjani, ilifika hatua nikawa nasikiliza mechi za Yanga nisikie tu namna anavyowatesa wapinzani. Lunyamila ndie alinifanya niipende Yanga ingawa nilikua namsikia redioni tu sikua namjua hata kwa muonekano, azam tv haikuwepo kipindi hicho
MANCHESTER UNITED: Ilikuaje nikaanza kuipenda hii timu? Usiku wa fainali ya champions league msimu wa 1998/1999 kati ya bayern Munich vs Man u. Mpaka kufikia hii siku sikua shabiki wa timu yoyote ulaya, bayern walitangulia kupata goli, tukiwa tumekusanyika mtaa mzima nyumbani kwa jirani yetu tunaangalia iyo game sebure nzima kulikua na huzuni kubwa sana nakumbuka wachezaji wa bayern kule benchi walishainuka wamepanga mstari huku wamekumbatiana mabegani kujiandaa na shangwe la ubingwa, furaha ilirudi pale sebureni baada ya Sosha kuchomoa goli dakika za mwisho kila mtu akijua game inaenda 120, Sosha akaweka cha pili. Nakumbuka refa alikua Collina muitary fulani hivi ananyoa kipara, nakumbuka beki wa bayern munich kufor alivyokua analia huku akipiga ngumi uwanja. Lile shangwe pale sebureni kwa jirani na mtaani baada ya mechi kuisha sitakuja kulisahau na ndio siku niliyoanza kuipenda manchester united.