Hapana: Serikali bado haijampa heshima stahiki Mzee wetu Benjamin Mkapa

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,502
51,098
Rais Mstaafu kafariki, Taifa limetangaziwa msiba huu mzito, kesho yake shughuli za serikali zinaendelea kama kawaida. Hata watoto kwenda shule wakaenda!

Ligi za mpira zinaendelea wakati mwili wa mzee wetu ukiwa umelala katika viwanja vya uwanja pale Uhuru Stadium

Mwili wa Mzee wetu unatolewa hospitalini Lugalo hospital, na ving'ora na gari la kijeshi, unapita mtaani, hakuna muongozo wowote wa serikali kwa wananchi kuwaeleza kuwa mwili utapita barabara zipi na kuwataka wananchi wasimame barabarani kutoa heshima zao kwa mwili huo. Yaani mwili unapita njiani wananchi wachache wachache tu nao kama wamestukizwa tu hawana habar na msafara!

Yaani mtu kama Ruge Mutahaba msiba wake ulikuwa organised na kutangazwa kwa nguvu zaidi, na kuwapa wananchi taarifa za kuwahamasisha kuupokea barabarani zaidi kuliko ilivyofanywa kwa rais wetu mstaafu.

Inakuwa vipi rais mstaafu aliyefanya Makubwa afariki halafu mtaani mambo yawe conducted as if nothing has happened?

Uko wapi uhamasishaji wa vikundi vya kwaya, na watu binafsi kumuimbia mzee wetu nyimbo za kumuaga?

Taasisi inayojihusisha na misiba mikubwa ya Kitaifa, mboba hamjaupa msiba mzito huu hadhi yake?

Mbona Mkapa wakati huo akiwa rais alimzika Mwalimu kwa heshima kubwa sana sana kuliko jinsi msiba wake ulivyokuwa handled?

Mbona mambo makubwa na mazito sana aliyoyafanya Mkapa kwa manufaa ya nchi hii hayatajwi kwa uzito wake sana kuwakumbusha wananchi mzee huyu alivyolitendea taifa?
 
Washamba na malimbukeni tumeshikilia usukani. Unategemea cha maana hapo? Kule kwetu huwa mtu akifariki tunafukia kama mnyama kisha tunaendelea. na shuguli zetu kama kawaida. Huwezi kutubadilisha ukubwani kirahisi.

Kwa taarifa yako tu, madaraka hayaondoi ushamba.
 
Nashauri mzee wetu apelekwe kwa njia ya barabara hadi nyumbani Masasi ili watu wa kusini tupate nafasi ya kumpa heshima za mwisho japo kwa kumpungia barabarani, bila yeye hakuna daraja la Mkapa alilolijenga na kuturahisishia usafiri Wana kusini.
 
Nashauri mzee wetu apelekwe kwa njia ya barabara hadi nyumbani Masasi ili watu wa kusini tupate nafasi ya kumpa heshima za mwisho japo kwa kumpungia barabarani, bila yeye hakuna daraja la Mkapa alilolijenga na kuturahisishia usafiri Wana kusini.
Ile slogan ya HAPA KAZI TU ndio imesababisha hali hii
 
Mimi naona poa2.Msiba mkubwa ni wasting of public money labda kama zitatoka kwenye account yake.
 
Tupo busy na mapokezi ya LISU ww mzee keshafariki nikumuombea tu hakuna kipya hapo
 
Back
Top Bottom