Hapa Lowassa hatoki...

Hapa Lowassa hatoki...

Tatizo kubwa tulilonalo Ni chuki na fitina zilizojaa mioyoni mwetu,Hatumkubali mtu hata kama kafanya vizuri kwa viwango Gani! Napenda tu nimsihi mchingiaji anayewaita watu wanavichwa vya nazi kuwa yeye ndiye mwenye kichwa hicho,na ameshindwa hata kulink hoja yenyewe,badala yake unaeneza siasa za chuki USIENDESHWE NA HISIA ZA CHAMA CHAKO BALI ANAGALI UTAIFA KWANZA.Wachangiaji wengine WA mada tajwa hapo juu wapo sahihi na makini sana.Uwe unasikiliza mambo kwa umakini kisha balance ukweli na hujuma.Pengine Ungeitwa leo hii mahakamani kutoa ushaidi wa Edo,ungetoroka nchi kabla ya ya ushahidi wako,maana tunauhakika huna hata chembe zaidi ya siasa za chuki binafsi.Tafadhali Usichangie hoja kama Konda wadalala ambeye yeye huacha kichwa nje na makalio hubaki ndani.
 
Hakuna jipya, ni haohao, mambo yao hayohayo NA 2015 hawatoki.
 
Edo Edo Edo Edo ...... vichwa vya nazi kujadili fisadi lililokubuhu katika utumishi wa umma. What significant acheivements can he bring in our country more than increasing grand corruptions and damaging the future of this nation? Where and when did he proved to be the best candidate in the CCM if you guys are not part of the corrupt tanzanians who does not wish the best to prevail in the future generation of our people. Records exist which shows that, from his early age after college was employed as public servant, how comes he demonstrates such huge accumulated wealth? when and how did he dedicated his time as business man to earn such a wealth if he neither plundered public funds nor used public office for personal gains?

Lets discuss possibility of getting right people for the presidency who have demonstarted high integrity in the public service of our country and stop this EDO thing out. He has no clean hands for the majority of Tanzanians but he has clean hands for very few of Tanzanians who are the beneficiary of his mis conducts.

Bora Fisadi alyeiba na akawekeza hapa TZ na tunaona mali zake kuliko Mafisadi waliotuibia na hatujui waliko peleka hizo mali zetu! Is it enough??
 
Uteuzi wa Nchemba kuwa Naibu Katibu Mkuu umeniacha hoi; Sielewi CCM huwa wanatumia performance indicators gani kumpandisha mtu cheo; Naibu katibu Mkuu wa Chama ni mtu mzito sana na Nchemba ni mtu mwepesi sana kubeba uzito huu; Iwapo CCM ilitaka Kijana ashike nafasi hii na atoke miongoni mwa Vijana waliopo mle tayari, ni bora nafasi hii angepewa Nape au Makamba Junior;

Kama wakuu wa chama walikuwa serious waliposema wanaunda timu ya ushindi kuelekea 2015, nadhani likija suala la kura za vijana, timu hii inaelekea zaidi kuwa timu ya kifo cha chama, sio ushindi, kwani hoja mbovu mbovu za nchemba zitakimbiza vijana wengi zaidi kutoka CCM; CCM isidanganyike na umati mkubwa wa vijana huko vijijini kwenye mikutano yake tena nyakati za kazi kwani umati huu huwa ni mkubwa kwa sababu vijana hawana kazi; Kwahiyo mara nyingine huwa ni outing kwenda kusikiliza vituko vya wanasiasa makujwaani;

Kwa kweli inasikitisha kugundua kwamba utumbo aliokuwa anaufanya Nchemba ambao umekuwa unatufukuzia vijana wengi kutoka CCM, utumbo huu huu umempatia madaraka zaidi ndani ya Chama; Nchemba Naibu wa Kinana? Nani alifanya uamuzi huu? Kweli kazi ipo na ndio maana awali nilisema kwamba mabadiliko yaliyotokea kwenye mwili huu wa CCM ni ya KICHWA, lakini SHINGO ambayo ndio hugeuza kichwa kulia na kushoto imebakia kuwa ni ile ile;

mwenyekiti wa chama chao amesema aliweza kukanyaga bajeti ya upinzani bungeni hivyo alionyesha kupambana na chadema inavyotakiwa. Huyo ndio aina ya mwenyekiti na rais kwa hiyo madudu yote yanayotokea tanzania ni kutokana na uelewa mdogo wa rais yani ameshindwa kung'amua kuwa kitendo cha mchemba kutupa bajeti ya upinzani kwenye chombo kikubwa km bunge ni utovu mkubwa wa nidhamu kwa watanzania
 
Naona fisadi mmoja aliyeficha mabilioni uswis hiki chama ni aibu tupu
 
Uteuzi wa Nchemba kuwa Naibu Katibu Mkuu umeniacha hoi; Sielewi CCM huwa wanatumia performance indicators gani kumpandisha mtu cheo; Naibu katibu Mkuu wa Chama ni mtu mzito sana na Nchemba ni mtu mwepesi sana kubeba uzito huu; Iwapo CCM ilitaka Kijana ashike nafasi hii na atoke miongoni mwa Vijana waliopo mle tayari, ni bora nafasi hii angepewa Nape au Makamba Junior;

Kama wakuu wa chama walikuwa serious waliposema wanaunda timu ya ushindi kuelekea 2015, nadhani likija suala la kura za vijana, timu hii inaelekea zaidi kuwa timu ya kifo cha chama, sio ushindi, kwani hoja mbovu mbovu za nchemba zitakimbiza vijana wengi zaidi kutoka CCM; CCM isidanganyike na umati mkubwa wa vijana huko vijijini kwenye mikutano yake tena nyakati za kazi kwani umati huu huwa ni mkubwa kwa sababu vijana hawana kazi; Kwahiyo mara nyingine huwa ni outing kwenda kusikiliza vituko vya wanasiasa makujwaani;

Kwa kweli inasikitisha kugundua kwamba utumbo aliokuwa anaufanya Nchemba ambao umekuwa unatufukuzia vijana wengi kutoka CCM, utumbo huu huu umempatia madaraka zaidi ndani ya Chama; Nchemba Naibu wa Kinana? Nani alifanya uamuzi huu? Kweli kazi ipo na ndio maana awali nilisema kwamba mabadiliko yaliyotokea kwenye mwili huu wa CCM ni ya KICHWA, lakini SHINGO ambayo ndio hugeuza kichwa kulia na kushoto imebakia kuwa ni ile ile;

Hata mimi nakubaliana na wewe, Nchemba kuwa promoted kwa hiyo level kweli nashindwa kuelewa. Hata hivyo tukumbuke kuwa kwa wale wakristo wanaamini kuwa wakati mwingine Mungu huwa anaruhusu mambo mengine yatokee ili agano lipite. Wakristo wanaamini Mungu aliruhusu Yesu apitie mateso na kufa ili agano lake la kumkomboa mwanadamu litimie.

Kwa Nchemba; huyu mlipukaji imebidi awe kwenye hiyo timu tena kwenye level hiyo ili aendelee kufanya madudu ambayo ni rahisi kutambulika kwa watu wasiojua ulipukaji wake. Hakuna mtu wa kuzuia mageuzi na dalili ndizo hizo tumeziona.
 
Hii ni sekretarieti lakini, sio CC; tulichonacho so far ni wajumbe saba wa sekretarieti ambao automatically wanaingia kwenye CC; Kwahiyo hawa ni wajumbe wa mwanzo wa CC i.e. wajumbe saba kati ya jumla ya wajumbe ishirini, which makes it only one third of the total so far; Ni muhimu tusubiri uteuzi wa wajumbe 13 waliobakia ili tujue ni kina nani, then ndio tuingie katika analysis husika;

wajumbe wengine wanaoingia kwa nafasi zao ni pamoja na waziri mkuu, rais wa tz, rais wa zenj, wale makamu wawili jumla sasa wanakuwa tisa, bado 11 tu. sasa huyu jk anashindwa kujua amteue nani, na amwache nani, hasa kutoka kwenye yale makundiyake
 
Sababu za kutojaza nafasi za Kamati Kuu zilizobaki JK hajazisema. Kwa kawaida anateua majina mengi tu miongoni mwa wajumbe wa NEC halafu wanapigiwa kura na NEC hiyohiyo. Kuahirisha kuwateua sasa ni pungufu na dhaifu jingine la Kikwete. Wengi tulimtarajia kama alivyofanya kwenye secretariet angeachana na walioko serikalini na hata BUNGENI labda kama mbunge ni wa kiti maalum kama alivyo mama Zakhia Meghji.

JK afikirie pia watu muhimu kama SAS kuwemo kwenye chombo hiki nyeti cha CCM. Kamati Kuu ya CCM isiposukwa vizuri tutampata mgombea URAIS wa ajabu sana mwaka 2015. Mwaka 1995 wakati Mwalimu akiwa hai majina kama ya akina Lowasa yalimalizwa na Kamati Kuu.
 
Kwa kweli khs kumu-undermine Mwigulu namna hiyo nafikiri unakosea sana, umechambua vizuri ila hapo umekosea sana kwa sababu huyo bwana anachukiwa na upinzani kwa ajili ya kuwapa vidonge vyao sio kila mtu anaona Mwigulu anaongea pumba, kawasome vizuri wapiga kura kaka.

Kama CCM inachagua timu ya kutoa vidonge then ntakubaliana na wewe; lakini kama CCM inaandaa timu ya kuongoza nchi na kuleta matumaini na maisha bora, then Mchambuzi yuko right 100%

Mimi nalinganisha Mwigulu na Lusinde, na kibaya zaidi Mwigulu amesoma shule.... Mwigulu is synonymous na kubwabwaja

CCM CAN DO BETTER THAN M-BWABWAJAJI
 
Katika hili kikwete anastahili pongezi , Kinana c mchezo , si mtu wa kupelekwa pelekwa na ndio maana alikaa pembeni kama wadau wanavyosema hapo juu watakuwa wamemshawishi sana kukubali hiyo nafasi, so far mi naona vichwa vya ccm vinavyoweza kusaidia ni nape,kinana na mangula wengine hao mhhhh !!

Siku taarifa ya Kinana kung'atuka CCM ilipokuja hapa JF kwa mara ya kwanza, nilikuwa wa kwanza kusema huku nikinukuu kauli ya Kikwete kuwa "viwanda vya uongo viko kazini". Uteuzi huu wa Kinana kuwa Katibu mkuu haujatokea kwa bahati mbaya...uteuzi huu unaenda sambamba na kung'atuka siasa alikotangaza Kinana yapata miezi sita iliyopita. Ndio maana amerejea huku akiahidi kuwa Watanzania watamwelewa tu...Napata hisia kuwa CCM wanafanya maigizo ya kisiasa,na hakuna la maana wanalokusudia kufanya kwa ustawi wa nchi yetu na watu wake. Niwasisitize Watanzania wenzangu wenye nia ya kuikomboa nchi, waachane na hizi siasa za maigizo za CCM, tuungane tuikatae CCM ya maigizo ambayo haina hata hoja moja inayoisimamia kwa dhati zaidi ya sanaa za maigizo zisizovutia zaidi ya mipasho na vijembe.
 
Kwa kweli khs kumu-undermine Mwigulu namna hiyo nafikiri unakosea sana, umechambua vizuri ila hapo umekosea sana kwa sababu huyo bwana anachukiwa na upinzani kwa ajili ya kuwapa vidonge vyao sio kila mtu anaona Mwigulu anaongea pumba, kawasome vizuri wapiga kura kaka.

Kaka hapa wewe nadhani ndiye unaekosea , mwigulu thinks after speaking. To me and perhsps to a majority of us Mwigulu has never provided poltically influential speeches.

Mwigulu ana shule kubwa kuliko Nape lkn Nape anauwezo mkubwa wa kupambanua nyakati za siasa na kuzitolea speech kwa mujibu wa nyakati hizo. Mwigulu is not of that type. Mchambuzi is right kwa mtazamo wangu.lkn nawewe huo ni mtazamo wako kwa hiyo tuendelee
 
mchezo uliochezwa na namna ulivyochezwa ni lazima kuufahamu....inshalah nikimaliza kazi mapema leo tutajulishana.
 
Hatred yako kwa CCM ipo justified kabisa, na ni mwehu tu ndio atakuwa na mapenzi na CCM ya sasa bila ya kuikosoa; vinginevyo kuhusu Lowassa na CC, ni mapema kujadili hilo as a final analysis kwani ni mapema mno kujua iwapo Lowassa is a political asset au a political liability KWA CCM, tutajua hilo Mwanzoni mwa 2015, hasa pale market forces zitakapo kick in; So far ni direct interventions ndio zinaendelea to determine whether he is an asset or a liability;

Vinginevyo kwa sasa, kama nilivyokwisha sema elsewhere, uteuzi wa Kinana, Mangula ni jambo zuri kwa CCM ya sasa, lakini ni muhimu tujue tu kwamba katika mwili wa lijitu hili linaloitwa CCM, kilichotokea ni mabadiliko kidogo katika Kichwa lakini Shingo imebakia kuwa ni ile ile;

Nadhanu pia utakubaliana na mimi kwamba Shingo (sio kichwa) ndio hufanya kichwa kigeuke kulia, kushoto, kitazame juu, kitazame chini, kilalie mto, kisilalie mto, kiitikie ndio au hapana kwa kutikisa kichwa n.k; Kichwa hakifanyi haya kwa maamuzi yake bali kwa maamuzi na nguvu ya shingo;

Hii ndio changamoto kubwa inayokikabili Kichwa (Kinana, Mangula) kwani Shingo ni ile ile;

He is already a liability na old phasing out product....The consumers have tested on this product called EL and there is no way you can change their preference so good kwa jinsi life ilivyo tight na kuwa tied up na attributes alizo kuwa tied up with-Ufisadi ambao CCM wenyewe waliusaidia kuu promote kwenye market kama one of his quality.....

Let me be sincere with you guys ndani ya CCM...Hao individuals wote hakuna mwenye interest na sijui imani itikadi ooh whasoever ya chama kinachowaweka waendelee kuwa members ni interest zao na hasa investiments walizonazo so the main objective is power consolidation. Wana monopolise power kwakutumia governance yaani policies zinazo exclude potential entrant ambao wata wa out compete kukiwa na free entry na exit ndani ya chama (democracy)..Ndiyo maana ya hii re-cycling otherwise siyo kwamba hawajui nini kitawaokoa ili waendelee kuwepo....One issue remains un-resolved je tukiingiza new members kwenye inner circle how would they react towards our interests? How powerful would we remain to make sure that we can influence their decisions?

So ndiyo unaona watoto wanapelekwa front, ndugu, jamaa, watu wenye same qualities (mafisadi) kwakujua kuwa na wao wana interest kuendlea kuilinda hiyo dola to safe guard the interest...Hao wengine associate ni wale waliopewa makombo ambao nao wanajua wazi hawa lords wakiondoka they have no enough muscles to compete with tough and competent excluded Tanzanians especially youths!

Bahati ya CDM ni kuwa imebeba hao future potential giants (Youths (male and female) educated, self reliant and competent)....Lakini link kati ya CDM na powerful people ndani ya system ndiyo tatizo kwa sasa...Ila siyo kitu ambacho kinashindikana only the right button needs to be pressed and there you are....Winners!
 
Kaka hapa wewe nadhani ndiye unaekosea , mwigulu thinks after speaking. To me and perhsps to a majority of us Mwigulu has never provided poltically influential speeches.

Mwigulu ana shule kubwa kuliko Nape lkn Nape anauwezo mkubwa wa kupambanua nyakati za siasa na kuzitolea speech kwa mujibu wa nyakati hizo. Mwigulu is not of that type. Mchambuzi is right kwa mtazamo wangu.lkn nawewe huo ni mtazamo wako kwa hiyo tuendelee

Kila kitu kina relative in comparison..When you compare Mwigulu with the rest of youths ndani ya CCM ofcourse he is far better..Lakini compare Mwigulu with youths ndani ya CDM sijui kama hata atasimama na mmoja wapo tena hawa tunaowafahamu ambao wameweza ku-break the ice in 2010 lakini wapo many ambao kwa sasa hawajawa exposed..Then ujue ni jinsi gani CCM iko taabani kama the only hope and the best is Mwigulu ambaye analysis yake kwenye budget ilishindwa kutofautisha finacial analysis na economic analysis when it comes to budgeting. yet the guy is a hero; na ndiyo atakaye isaidia nchi ki-uchumi...

Duuh shuguli ipo tena pevu....Vijana wengi wa umri wa Mwigulu wanauelewa mkubwa kumzidi na wakipewa platform utashangaa jinsi atakavyo pwaya...Tuliona wakati ule wa Tido na mchakato majimboni tena wakati huo bado ice breaking ilikuwa haijafanyika na hesitation kwa abled youth ilikuwa kubwa...Leo itokee tena utashangaa kuona jinsi Tanzania ilivyo kuwa na potential youths ambao wamekuwa excluded na policies zenye kuleta monopolicies katika siasa...

Kazi yangu inanifanya niweze ku-interact na hao vijana so hii si hisia bali nawafahamu vijana wengi sana ambao they can do far better than what guy mwenye certificate ambao imekuwa graded na system mbaya ya elimu Tanzania ambapo hata wasioweza ku-articulate issues wanaweza pata hizo maksi na kuacha wengine ambao wako more deep in matters wakiwa na average marks.
 
Uteuzi wa Nchemba kuwa Naibu Katibu Mkuu umeniacha hoi; Sielewi CCM huwa wanatumia performance indicators gani kumpandisha mtu cheo; Naibu katibu Mkuu wa Chama ni mtu mzito sana na Nchemba ni mtu mwepesi sana kubeba uzito huu; Iwapo CCM ilitaka Kijana ashike nafasi hii na atoke miongoni mwa Vijana waliopo mle tayari, ni bora nafasi hii angepewa Nape au Makamba Junior;

Kama wakuu wa chama walikuwa serious waliposema wanaunda timu ya ushindi kuelekea 2015, nadhani likija suala la kura za vijana, timu hii inaelekea zaidi kuwa timu ya kifo cha chama, sio ushindi, kwani hoja mbovu mbovu za nchemba zitakimbiza vijana wengi zaidi kutoka CCM; CCM isidanganyike na umati mkubwa wa vijana huko vijijini kwenye mikutano yake tena nyakati za kazi kwani umati huu huwa ni mkubwa kwa sababu vijana hawana kazi; Kwahiyo mara nyingine huwa ni outing kwenda kusikiliza vituko vya wanasiasa makujwaani;

Kwa kweli inasikitisha kugundua kwamba utumbo aliokuwa anaufanya Nchemba ambao umekuwa unatufukuzia vijana wengi kutoka CCM, utumbo huu huu umempatia madaraka zaidi ndani ya Chama; Nchemba Naibu wa Kinana? Nani alifanya uamuzi huu? Kweli kazi ipo na ndio maana awali nilisema kwamba mabadiliko yaliyotokea kwenye mwili huu wa CCM ni ya KICHWA, lakini SHINGO ambayo ndio hugeuza kichwa kulia na kushoto imebakia kuwa ni ile ile;

Kwa ulivyomchambua lameck Nchemba nimekupa like, jenerali ulimwengu aliwahi kusema unapowapa madaraka watu washamba malimbukeni kama Nchemba jua umepotoka, kwa hili CCM imechimba kabuli
 
Uteuzi wa Nchemba kuwa Naibu Katibu Mkuu umeniacha hoi; Sielewi CCM huwa wanatumia performance indicators gani kumpandisha mtu cheo; Naibu katibu Mkuu wa Chama ni mtu mzito sana na Nchemba ni mtu mwepesi sana kubeba uzito huu; Iwapo CCM ilitaka Kijana ashike nafasi hii na atoke miongoni mwa Vijana waliopo mle tayari, ni bora nafasi hii angepewa Nape au Makamba Junior;
;
Nakuomba usome maneno yaliyokuwa highlited na Nyekundu upate nataka kumaanisha nini. Nafasi ya Naibu katiibu Mkuu Bara/Zanzibar ni nafasi ya kitendaji, na kwa mujibu wa kanuni za CCM hairuhusiwi kushikwa na mwanachama mwenye wadhifa wa uwaziri katika serikali. Kwa maana hiyo January Makamba ni naibu waziri hivyo hawezi kushika nafasi ya Naibu katibu Mkuu nafasi ambayo ni ya kitendaji itapinganana kanuni za uongozi za CCM.
 
Jamani kwa sasa bado mapema sana me nafkiri tutajua mambo yote tutakapovuka daraja bt what i know lowasa atazidi kujimarisha sana sana.
 
Nakuomba usome maneno yaliyokuwa highlited na Nyekundu upate nataka kumaanisha nini. Nafasi ya Naibu katiibu Mkuu Bara/Zanzibar ni nafasi ya kitendaji, na kwa mujibu wa kanuni za CCM hairuhusiwi kushikwa na mwanachama mwenye wadhifa wa uwaziri katika serikali. Kwa maana hiyo January Makamba ni naibu waziri hivyo hawezi kushika nafasi ya Naibu katibu Mkuu nafasi ambayo ni ya kitendaji itapinganana kanuni za uongozi za CCM.

Hoja yangu ya msingi ilikuwa kwamba January was a better candidate kwa nafasi hiyo kama walitaka kijana, which means angehitajika, angeachia kofia moja per kanuni unayoizungumzia; in short, you are right, lakini ni muhimu pia uelewe msingi wa hoja yangu ilikuwa nini, haikuwa kupendekeza january awe naibu katibu mkuu huku akiwa ni naibu waziri;
 
Kwa ulivyomchambua lameck Nchemba nimekupa like, jenerali ulimwengu aliwahi kusema unapowapa madaraka watu washamba malimbukeni kama Nchemba jua umepotoka, kwa hili CCM imechimba kabuli

Unajua wapo wengi humu ambao wataona kumjadili Nchemba au wengine kama wabovu ni wivu na mambo kama hayo; Wapo sahihi iwapo kwa watu hawa kuteuliwa nafasi kama hizi ni KUULA, kwani magazeti mengi yanaweka vichwa vya habari fulani na fulani WAULA; Kwa mentality kwamba kupewa kazi ya umma ni kwenda kula, basi kupinga hoja zetu kwamba viongozi kama kina nchemba wabovu ni hoja zenye mashiko, lakini hoja zao zitakuwa ni za ovyo iwapo kazi hizi za umma ni za kwenda kutumikia nchi/wananchi, kujenga chama katika mazingira ya ushindani, na mambo kama hayo yenye tija kwa chama na taifa kwa ujumla wake; Kazi za chama, ubunge n.k hizi sio kama kazi za Vodacom au Barclays, lakini kwa bahati mbaya, wengi hawalioni hili;
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom