Baada ya uchaguzi huu wa Mwenyekiti wenu wa ccm na makamu wake tumeshuhudia vilio toka kwa wanaccm wenyewe wakilia kuchezewa rafu, kuibiwa kura zao, kuchakachuliwa matokeo ya kura zao.
Wameelezea kwamba makamu mwenyekiti bara alipata kura 50 za hapana na makamu mwenyekiti zanzibar alipata kura za hapana 48. Kama hiyo haitoshi tumeambiwa mwenyekiti aliponea chupuchupu kung'olewa kwani hadi nusu ya kura zilizokuwa zimehesabiwa kura za ndio na hapana zilikuwa zinakwenda sambamba hadi matson chizii alipotoka ndani ya chumba cha kuhesabia kura akaenda kusikojulikana na baadae akarudi na usalama wa taifa na green guard, wakawatoa nje wajumbe wote waliokuwa wanahesabu kura na wao wakafanya kazi hiyo.
Katika matukio mengine ya uchaguzi wa ndani ya ccm ambapo wanaccm wenyewe wamekuwa wakilalamika kuchakachuliwa ni dhahiri kwamba ccm ni mafundi wa kuchakachua na ukweli wa kura za uraisi kuchakachuliwa katika uchaguzi mkuu wa 2010 uko dhahiri, na hata majimboni katika nafasi za ubunge, udiwani, umeya na uenyekiti wa halmashauri mchezo ni huo huo.
Kwahiyo anachoandika Mchambuzi ni mawazo yake ambayo ukiyatazama kwa kina utaona yana ukweli kwa sehemu kubwa sana, na si suala la kuogopa ama kutafuta support ya wanaJF.
kwa nini wewe na mashabiki wenzako hamkuingia mtaani kupinga matokeo mkawaacha mbowe na slaa peke yao kulalamika? nakumbuka hata zitto na viongozi wengine wa cdm hawakuona umuhimu wa kumkataa JK kwa sababu hawakuamini kama slaa alipata kura zaidi ya mil 4.5 kati ya zile mil 8 zilizopigwa. Nikuelimishe zaidi kaka, uchaguzi wa kimabadiliko uonekana toka mwanzo kwa kujitokeza kwa wapiga kura wapya wengi na upigaji kura uwa mkubwa (hapa ujue mabadiliko utokea) ila kwa number za 2010 ingekua miujiza kwa Slaa kushinda na numbers kama zile.