Hapa kuna msaada wa kisheria? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hapa kuna msaada wa kisheria?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Kana-Ka-Nsungu, Jan 13, 2009.

 1. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu wenye upeo mkubwa kwenye mambo ya kisheria, naomba mawazo yenu kwenye hii scenario hapa chini:

  Hapo zamani la kale baba yako kabla ya kufariki analikujulisha kwamba anashare kwenye shamba la ekari tano la urithi aliloachiwa yeye pamoja na nduguze wawili. Kutokana na kutingwa na majukumu unashindwa kabisa kutembelea lilipo shamba hilo kwa muda mrefu lakini unapopata akili ya kulifuatia unagundua kuwa ndugu wa marehemu baba yako walishaliuza na kugawana kimyakimya bila kukushirikisha. Ugumu wa kuwabana unatokana na sababu kwamba baba yako hakuwa na kitu chochote kwenye maandishi kuhusu umiliki wake wa shamba hilo, shamba lenyewe lilikuwa halina hati ya umiliki na ndugu za baba yako ukiwauliza wanakuambia- baba yako hakuwa na share!
  Unaanzia wapi hapa kudai haki yako?
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,090
  Trophy Points: 280
  KKN, mimi si mwanasheria lakini ili kupata haki yako inabidi kufungua kesi mahakamani na inabidi kuwa na hati miliki, bila kuwa na hati miliki hii itakuwa ni kesi ngumu mno kwako na utaishia kupoteza muda na pesa, lakini labda wanasheria kama wapo hapa wanaweza kuwa na mtazamo tofauti na wangu.
   
 3. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,517
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Mkuu kwa vyovyote vile, ni wazi kuwa shamba hilo lilikuwa likimilikiwa kwa mujibu wa sheria za kimila. Ili kuweza kupata haki yako, consult Sheria zenu za kimila kwanza kabla ya kufanya chochote. Tafuta wazee wa kimila uwadodose ili wakupe abc ya sheria za kimila za kabila lenu. Anza na hilo kwanza mkuu.
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Naungana mkono na ChiefmTz kuwa hilo shamba lilikuwa lamilikiwa kimila. Na ndio mashamba na mali nyingi hasa za vijijini, hata baadhi ya majumba mijini hayana hati, bali tu inajulikana ni ya mtu fulani.

  Cha kufanya ni kutafuta ndugu wanaolifahamu hilo, hapa waweza kuwa wajomba, shangazi, bibi, babu. Pia majirani, manake majirani ndio wanajua historia kuwa huyo muhusika alikuwa akimiliki hilo shamba tokea kwa nani. Na unapotafuta majirani, wenye umri mkubwa walioishi na huyo mzee watakuwa muhimu. Ukishawapata watu wataokuwa tayari kulitolea hilo shamba ushahidi, nenda kwa serikali ya kijiji anza process ya kudai haki, hao jamaa wataitwa ili kutoa ushahidi kuwa marehemu alikuwa mmoja wa wamiliki wa hilo shamba. Usuluhishi na madai yataanza katika serikali ya kijiji, wakishindwa watatoa ruhusa kufungua kesi ya kudai haki hiyo mahakamani.
   
 5. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nenda kwenye mabalaza ya ardhi ya kijiji. hawa ndio watakao toa uamuzi wa nani anamiliki nini hapo, wakishindwa wataenda kwenye mabalaza ya ardhi ya kata, then kama wakishindwa wataenda mbele. ila kwa kifupi kama walivyosema wenzangu, hiyo kitu inaangukia kwenye sheria za ardhi kimila. inadondokea kwenye sheria ya ardhi ya vijiji mwaka 1999. nenda web ya parliament chukua hiyo sheria isome.

  Ninasikitika kukutaarifu kuwa, kama huo muda ulioitelekeza iyo ardhi umepita miaka kumi na miwili, haki yako ya kumiliki ardhi imepotea kisheria, na anayeikalia ardhi hiyo kwa sasa kimila na kwa halali, ni yake. kwa kawaida, umiliki ardhi kimila unaisha baada ya miaka kumi na miwili kupita kama umeitelekeza iyo ardhi. kama alishaenda kuitumia na kuweka identity yako pale katikati ya iyo miaka, basi mabaraza ya ardhi ya kijiji yataamua iyo kesi. ila kama ulitelekeza ukapenda mjini bongo daslam bila hata kwenda kusalimia kijijini mzee umeliwa. upo hapo? sijui uko fungu gani.

  na wale ambao wanayo maeneo ya ardhi vijijini, mnatakiwa mwende mkaipatie hati. wanatoa hati za kumiliki ardhi kimila siku hizi. hiyo itakusaidia sana kuchukulia hata mkopo. pia, ni program ya selikali, inataka in ten years to come, iwe imewamilikisha watz ardhi yote, ili tuondokane na huu mgogoro wa ardhi na majirani zetu kwenye mambo ya ushirikiano. tuchangamke, tununue ardhi vijijini na tuchukue hati mapema. si muda hiyo ardhi tunayoidharau itakuwa na value kubwa sana kama ile ya kenya.

  tafadhali, naombeni maswali ya ardhi, benk, inheritence yaani ugawaji mirathi, wills, company laws, na sheria kama hizo. swali lolote lile la ndoa, ni chai kwangu, lileteni and criminal offense yoyote ni ile.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,325
  Trophy Points: 280
  Naungana na Mwana wa Mungu, kwa kuongezea, kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi Namba 4 ya Mwaka 1999 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba 5 ya Mwaka 1999, mikataba mingine yoyote inaweza kuwa ya mdomo, lakini mauziano ya Ardhi, lazima yawe na maandishi, kama hakuna maandishi yoyote ya umiliki wa Mzee wako kwenye Ardhi tajwa, ni sawa na hakuna umiliki unless anaishi kwenye eneo husika kwa zaidi ya miaka 12, ama kuwe na uthibitisho wa makaburi/mahame kama viashiria vya milki ya ardhi ya kimila na kuthibitishwe na wazee walio hai.
  Kinyume cha hapo, you have no any legal remwdies. Just consider the land lost.

  However, kuna sheria ya asili ambayo haina maandishi, inaitwa 'Law of the Karma'. Kila anayefanya dhuluma hapa duniani, malipo ni hapa hapa duniani. Just sit and watch hao waliomdhulumu marehemu watakavyo 'perish one after the other on horrible deaths' ama maisha yao 'its a living hell'
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Natatizika kuamini kuhusu the so called "Law of the Karma" - mbona dhuluma zimekithiri duniani? Hapa Tanzania tu tukiangalia dhuluma katika ngazi mbalimbali tutashangaa na kuuliza when does law of the karma start operating.
  Ninachoamini ni kuwa, hata Kama una haki, ukiikalia ujue utakapoihitaji itakuwa haipo.Kwenye hili la ardhi kanuni za sheria ziko wazi (tukiachilia mbali vifungu vilivyotajwa na wachangiaji waliotangulia).Ardhi ni nyenzo muhimu sana kwa maisha ya mtu wa kawaida Tz na hata sheria zetu zimetungwa kwa kuzingatia hilo.Kama kweli unaihitaji basi huwezi ukawa umeitelekeza kwa kipindi chote hicho.Kutelekeza ardhi ni moja ya mambo yanayozuiliwa na sheria na ndiyo maana hata kama haupo, sheria inakuta uache angalau kitu cha kuthibitisha kuwa utarudi ( animus revetendi).
   
Loading...