Hapa Dodoma: Mambo ni moto!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Sasa niko Dodoma 'kikazi' kwa shughuli za chama yaani CCM. Hapa Dodoma,pamoja na kufuatilia nyendo za Wabunge wa CCM,lakini pia tunazifuatilia nyendo za Wabunge wa upinzani hasa wa CHADEMA. Tumearifiwa hapa kuwa Wakili Msomi Tundu Antipas Mughway Lissu(Mbunge) ametua Dodoma na nyaraka mbalimbali zinazogusa 'skendo' za wenye nchi.

Katika pitapita zetu na kupitia taarifa na nyaraka,tumegundua kuwa Ofisi ya Spika wa Bunge haina amani na Wabunge wa CHADEMA. Hivyobasi,Ofisi ya Spika imeomba msaada wa Serikali-hasa wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali-Jaji na Wakili Msomi Fredrick Mwita Werema na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Uratibu na Bunge)-Ndugu William Lukuvi kudhibiti kombora lolote la CHADEMA. Pia,wabunge wengine wa upinzani wasiotokana na CHADEMA wanaandaliwa zawadi kama wakitoa msaada wa kiudhibiti.

Hapa Dodoma,habari kuu ni kuwafunga midomo Wabunge wa CHADEMA na wanaofanana nao,ili kulinda taswira ya Serikali ya CCM. Sifa kemkem zinamwagwa kwa Spika Anne Makinda na uongozi wa Bunge kwa ujumla kwa kupitisha kanuni mpya zitakazopunguza presha kwa kiti cha Spika na Serikali wakati wa kujadilina kupitisha Bajeti ya Serikali.Kimsingi,wapinzani wamejipanga na kupangika.Vivyo hivyo kwa Serikali na Wabunge wa chama tawala. Patakuwa padogo hapa Dodoma.Stay tuned!

Crazy observation: Wabunge wengi vijana hasa wa upinzani wanakunywa sana pombe jamani.Wajirekebishe.Wasipofanya hivyo,nitawaweka hapa majina na picha zao wakiwa chakari. Niko hapa karibu yao wakiwa wamelewa sana. Not good at all!

Kila kitu kitakachojiri hapa ambacho watanzania watapaswa kukijua,watakijua tena kwa haraka sana. Usiku mwema!

VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba Dar es Salaam(sasa Dodoma)
 
pombe na wabunge..
halafu utasikia eti wako katika hatari ya kutekwa na kuwekewa sumu
hii nchi hii...
 
Hao wabunge walevi wa upinzani hapo sugu, lema hawakosi. Hilo ni balaa tupu! Mjiangalie vizuri!
 
Crazy observation: Wabunge wengi vijana hasa wa upinzani wanakunywa sana pombe jamani.Wajirekebishe.Wasipofanya hivyo,nitawaweka hapa majina na picha zao wakiwa chakari. Niko hapa karibu yao wakiwa wamelewa sana. Not good at all!

Ni kweli kabisa. Unywaji wa pombe hasa wa kupitiliza sio mzuri hasa ukiwa unakabiliwa na shughuli nzito ambazo inabidi utumie akili na kujilinda usitamke maneno hovyo hadharani.
 
Sasa niko Dodoma 'kikazi' kwa shughuli za chama yaani CCM. Hapa Dodoma,pamoja na kufuatilia nyendo za Wabunge wa CCM,lakini pia tunazifuatilia nyendo za Wabunge wa upinzani hasa wa CHADEMA. Tumearifiwa hapa kuwa Wakili Msomi Tundu Antipas Mughway Lissu(Mbunge) ametua Dodoma na nyaraka mbalimbali zinazogusa 'skendo' za wenye nchi.

Katika pitapita zetu na kupitia taarifa na nyaraka,tumegundua kuwa Ofisi ya Spika wa Bunge haina amani na Wabunge wa CHADEMA. Hivyobasi,Ofisi ya Spika imeomba msaada wa Serikali-hasa wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali-Jaji na Wakili Msomi Fredrick Mwita Werema na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Uratibu na Bunge)-Ndugu William Lukuvi kudhibiti kombora lolote la CHADEMA. Pia,wabunge wengine wa upinzani wasiotokana na CHADEMA wanaandaliwa zawadi kama wakitoa msaada wa kiudhibiti.

Hapa Dodoma,habari kuu ni kuwafunga midomo Wabunge wa CHADEMA na wanaofanana nao,ili kulinda taswira ya Serikali ya CCM. Sifa kemkem zinamwagwa kwa Spika Anne Makinda na uongozi wa Bunge kwa ujumla kwa kupitisha kanuni mpya zitakazopunguza presha kwa kiti cha Spika na Serikali wakati wa kujadilina kupitisha Bajeti ya Serikali.Kimsingi,wapinzani wamejipanga na kupangika.Vivyo hivyo kwa Serikali na Wabunge wa chama tawala. Patakuwa padogo hapa Dodoma.Stay tuned!

Crazy observation: Wabunge wengi vijana hasa wa upinzani wanakunywa sana pombe jamani.Wajirekebishe.Wasipofanya hivyo,nitawaweka hapa majina na picha zao wakiwa chakari. Niko hapa karibu yao wakiwa wamelewa sana. Not good at all!

Kila kitu kitakachojiri hapa ambacho watanzania watapaswa kukijua,watakijua tena kwa haraka sana. Usiku mwema!

VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba Dar es Salaam(sasa Dodoma)
Mwigulu vipi kazungukwa na machangu wangapi?
 
Nyumba ikichoka pakivuja hapa unaziba kesho panavuja pengine dawa ni kuibomoa na kujenga mpya tu!

CCM ni nyumba iliyochoka haifai hata viraka!!
 
Masikini hii ID ya wapambanaji wa CDM siku hizi inaongea pumba sijui ni voluntia gani wameachiwa?
 
Hao wabunge walevi wa upinzani hapo sugu, lema hawakosi. Hilo ni balaa tupu! Mjiangalie vizuri!

Tunawajua wale wabunge wa CCM ambao hata kuchangia hawawezi hadi wakayatwike maji ya Pansiasi au Ilala. Wakijua tu wamo kwenye list ya wachangiaji wanakimbilia baa kwanza. Mbona wanajulikana hapa Dom. Ndiyo maana huwa wanaitikia ndiyoooo hata kwa vitu wasivyovijua. Mambo mengi huchangia.
 
Back
Top Bottom