VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Sasa niko Dodoma 'kikazi' kwa shughuli za chama yaani CCM. Hapa Dodoma,pamoja na kufuatilia nyendo za Wabunge wa CCM,lakini pia tunazifuatilia nyendo za Wabunge wa upinzani hasa wa CHADEMA. Tumearifiwa hapa kuwa Wakili Msomi Tundu Antipas Mughway Lissu(Mbunge) ametua Dodoma na nyaraka mbalimbali zinazogusa 'skendo' za wenye nchi.
Katika pitapita zetu na kupitia taarifa na nyaraka,tumegundua kuwa Ofisi ya Spika wa Bunge haina amani na Wabunge wa CHADEMA. Hivyobasi,Ofisi ya Spika imeomba msaada wa Serikali-hasa wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali-Jaji na Wakili Msomi Fredrick Mwita Werema na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Uratibu na Bunge)-Ndugu William Lukuvi kudhibiti kombora lolote la CHADEMA. Pia,wabunge wengine wa upinzani wasiotokana na CHADEMA wanaandaliwa zawadi kama wakitoa msaada wa kiudhibiti.
Hapa Dodoma,habari kuu ni kuwafunga midomo Wabunge wa CHADEMA na wanaofanana nao,ili kulinda taswira ya Serikali ya CCM. Sifa kemkem zinamwagwa kwa Spika Anne Makinda na uongozi wa Bunge kwa ujumla kwa kupitisha kanuni mpya zitakazopunguza presha kwa kiti cha Spika na Serikali wakati wa kujadilina kupitisha Bajeti ya Serikali.Kimsingi,wapinzani wamejipanga na kupangika.Vivyo hivyo kwa Serikali na Wabunge wa chama tawala. Patakuwa padogo hapa Dodoma.Stay tuned!
Crazy observation: Wabunge wengi vijana hasa wa upinzani wanakunywa sana pombe jamani.Wajirekebishe.Wasipofanya hivyo,nitawaweka hapa majina na picha zao wakiwa chakari. Niko hapa karibu yao wakiwa wamelewa sana. Not good at all!
Kila kitu kitakachojiri hapa ambacho watanzania watapaswa kukijua,watakijua tena kwa haraka sana. Usiku mwema!
VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba Dar es Salaam(sasa Dodoma)