Hanje: Wabunge Vijana hawana michango yenye tija kwa Watanzania

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,468
9,208
Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum, Nusrat Hanje amesema wabunge vijana wanashindwa kulisaidia Taifa kwa kuwa michango yao bungeni haina tija na haiwezi kuwapeleka mbele Watanzania.

Ameeleza hayo Februari 10, 2021 bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa Mpango wa Serikali unaoonyesha mwelekeo wa bajeti 2021/22 na kuibua hali ya sintofahamu kutokana na baadhi ya wabunge kuwasha vipaza sauti na kumjibu bila kufuata utaratibu.

Kauli hiyo iliwakwaza wawakilishi hao wa wananchi akiwemo Naibu Spika, Dk Tulia Akson aliyewatuliza kiaina wabunge akisema kauli ya Hanje haina ukweli na kumtaka mbunge huyo kujikita kuchangia mjadala husika.

Akiendelea na mchango wake, Hanje amesema hakuna tupu iliyo tupu kabisa, na kwamba inawezekana wapo waliotoa michango ya maana.

Kauli hiyo ilimnyanyua tena Dk Tulia safari hii akitoa ufafanuzi juu ya kauli hiyo huku wabunge wengi wakipiga kelele, baadhi wakidai ufungwa umemchanganya Hanje na kwamba anawaza kufukuzwa uanachama Chadema.

Baadhi ya wabunge waliosimama na kumpa taarifa Hanje ni Jacqueline Msongozi, Ndaisaba Ruhoro, Patrobas Katambi na Hussein Nasoro wakidai Hanje amevunja kanuni kwa kusema uongo bungeni.

Katika ufafanuzi wake kuhusu taarifa hizo, Dk Tulia amesema michango ya wabunge vijana katika Bunge hilo la 12 ni mkubwa, akisisitiza kuwa wabunge bado wanajifunza.

Kabla ya kuapishwa kuwa mbunge wa Viti Maalum Novemba mwaka 2020, Hanje alitokea mahabusu alikokaa kwa siku 133 baada ya yeye na wenzake kupata msamaha wa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Biswalo Mganga.

Nusrat alikuwa mmoja wa makada 19 walioibua utata baada ya kujitokeza kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum Chadema, wakati chama chao kikisema hakijapeleka majina ya mapendekezo kwa ajili ya uteuzi na kikituhumu kuwepo kwa njama dhidi yake.

Chama kinachopata zaidi ya asilimia tano za kura za ubunge katika Uchaguzi Mkuu, hupata nafasi za viti maalum kulingana na idadi ya kura.

Mbunge huyo na wenzake walikuwa gerezani wakishtakiwa kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usio halali, kudhihaki wimbo wa Taifa, kujaribu kuvujisha siri za halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida na kutoa lugha za kuudhi.
 
Hivi wale wanaosema jamaa aongezewe muda ni vijana au wazee?

Hawa covid wawe makini huko bungeni, ni kama wanalazimisha kusema chochote ili warudishe imani kwa wale waliowakosea bila kujali athari za maneno yao kwa hao wanaowasema.

Mpaka watakapotubu dhambi zao kwa waliowakosea ndio watakuwa na amani, vinginevyo watajikuta wanaharibu na kuchukiwa hata na marafiki zao wa CCM.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom