Wabunge Wawili wa Chadema Waunga Mkono Azimilo la Kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,051
49,735
My Take
Chadema wameanza kumuelewa Rais Samia baada ya wabunge wao wawili Nusrati Hanje na Salome Makamba Kupiga Kura ya ndio wakati wa azimio la Kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali.

Kupinga Kila kitu ni Ujinga.
1687773427935.png

======
WABUNGE 354 wakiwemo wa Viti Maalum Nusrati Hanje na Salome Makamba wamepiga kura ya Ndiyo wakati Bunge likiidhinisha Bajeti Kuu ya Mwaka 2023/24 iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba.

Wabunge wengine 20 akiwemo Halima Mdee walipiga kura ya kutokuwa na maamuzi (abstain) huku hakuna aliyepiga kura ya hapana.Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson ametangaza kuwa Bunge limeidhinisha Bajeti ya Serikali kwa asilimia 95 ya Wabunge wote waliopiga kura.
 
Nawaunnga mkono msimamo wa hawa covid-19 wawili. Unasnzaje kupinga mpango wa ubia ktk uendeshaji wa bandari kati ya waarabu wabobezi (ktk uendeshaji wa bandari) na serikali ya Tanzania?

Ktk hili nasimama na rais Samia
 
Onyo la Mwisho : Chadema haina wabunge wa viti maalum kwenye bunge la Tanzania

Mleta Mada jaribu kuwa na heshima na Chadema ili uheshimike , Ukileta uzushi utachafua hali ya hewa muda si mrefu
Wale ni wabunge wa Chama gani? 😂😂
 
My Take
Chadema wameanza kumuelewa Rais Samia baada ya wabunge wao wawili Nusrati Hanje na Salome Makamba Kupiga Kura ya ndio wakati wa azimio la Kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali.

Halima Mdee na Baadhi ya wengine wame abstain.
View attachment 2669286

======
WABUNGE 354 wakiwemo wa Viti Maalum Nusrati Hanje na Salome Makamba wamepiga kura ya Ndiyo wakati Bunge likiidhinisha Bajeti Kuu ya Mwaka 2023/24 iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba.

Wabunge wengine 20 akiwemo Halima Mdee walipiga kura ya kutokuwa na maamuzi (abstain) huku hakuna aliyepiga kura ya hapana.Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson ametangaza kuwa Bunge limeidhinisha Bajeti ya Serikali kwa asilimia 95 ya Wabunge wote waliopiga kura.
Hao wabunge wa Tulia Ackson, chadema ina mbunge mmoja tu jimbo la nkasi, aidan kenan
 
Back
Top Bottom