Hangary: Hatutoafikiana na EU kuweka vikwazo dhidi ya mafuta na gesi ya Russia, 90% ya waHungary watapata dhiki kubwa na uchumi wetu utaanguka

Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban, ametangaza kuwa nchi yake (Hungary) ipo dhidi ya vikwazo vyovyote vitavyowekwa na umoja wa Ulaya juu ya Russia kuuza mafuta na gas ktk nchi za Umoja huo.

Kufuatia mkutano uliofanyika London uliowahusisha mawaziri wakuu wa nchi kadhaa zikiwemo Hungary, Poland, the Czech Republic, Slovakia na Uingereza, Orban alisema kuwa pamoja na kuwa Hungary imesikitishwa na Russia kuanzisha vita nchini Ukraine, lakini serikali ya Hungary hapo tayari kuruhusu familia za waHungary kufanywa kafara (kuadhibiwa) la vita hiyo (“to be made to pay the price of war”).

Akinoti kuwa vikwazo vinavyoweka dhidi ya Russia vinaziumiza nchi zote za Ulaya, Waziri Mkuu huyo akasema kuongezea vikwazo ktk sekta ya nishati ya Russia (mafuta na gesi asilia) vitaiathiri Hungary vibaya zaidi. Waziri Muu huyo akadokeza kuwa karibia kiasi chote cha mafuta na gesi asilia kinachotumika Hungary hununuliwa toka Russia, na 90% ya familia za waHungary hupasha joto makazi yao kwa kutumia gesi hiyo ya Russia, akaongezea kuwa uchumi wa nchi ya Hungary hauwezi kusimama pasi na mafuta na gesi za Russia.

===========

Hungary will not support sanctions on Russia covering oil, gas imports: Premier

Hungary buys most of its oil and natural gas from Russia, says Viktor Orban​

Mehmet Yılmaz |09.03.2022

Hungary will not support sanctions on Russia covering oil, gas imports: Premier

BUDAPEST

Hungarian Prime Minister Viktor Orban announced Tuesday that his country is against possible sanctions on Russia that would cover imports of its oil and natural gas.

Following a meeting in London with his counterparts from fellow Visegrad Group countries Poland, the Czech Republic and Slovakia along with British Prime Minister Boris Johnson, Orban said in a statement that Hungary condemns Russia’s launch of a war on Ukraine but would not allow Hungarian families “to be made to pay the price of war.”

He said it is in everyone's interest to end the war as soon as possible and his country will make every effort to do so.

Noting that the sanctions imposed on Russia affect all countries in Europe, he said the expansion of sanctions to Russia’s energy sector will affect Hungary "very seriously."

Orban said Hungary buys most of its oil and natural gas from Russia and 90% of Hungarian families heat their homes with gas, adding the Hungarian economy could not function without oil and gas.

Russia's war on Ukraine, which began on Feb. 24, has drawn international condemnation, led to financial sanctions on Moscow and spurred an exodus of global firms from Russia.

At least 474 civilians have been killed and 861 injured in Ukraine since the beginning of the war, according to the UN, which noted that conditions on the ground make it difficult to verify the true number.
Some 2 million people have also fled to neighboring countries, said the UN Refugee Agency.

Nilitegemea wangefika huko kutokubaliana, lakini sikutegemea kama ingekuwa mapema hivi
 
EU ni AU ilichangamka,ina uchumi mzuri, ina teknolojia, lakini nao ni mandezi kama AU tu, marekani hana nia nzuri na wao,anafanya yoote kwa manufaa yake.
Watashangaa vita inaisha ndumilakuwili USA anawafungulia vikwazo RUSSIA na kuendelea na biashara zao kama awali kwa ile filosofi yao ya kutokuwa na Rafiki wala Adui wa kudumu
 
Uingereza mimi hua namchukulia ni mke halali wa Marekani, yeye yuko bega kwa bega kumsapoti mume wake, ila hawa wengine ndio hua nashindwa kuwaelewa yaani nawafananisha na michepuko isiyokua na misimamo, bwana wao Marekani akiwakazia wanatoa mpaka ndogo.
nchi yenyewe inaongozwa na Bibi ,ambaye ni KE .kuolewa ni obviously
 
wengi mnajadili tu ila hamjui kwanini EU inasimama na USA na kumsikiliza..

Mkasome vizuri WW2, ndio mtafahamu kwanini mataifa ya ulaya magharibi yanasujudu kwa USA.?
 
Marekani ni muhuni sana, lengo lake ni kuidhoofisha Europian Union, alianza na kampeni ya BREXIT akafanikiwa, sasa hivi kawaingiza mkenge kwenye hili sakata la Ukraine nao wakanaingia kichwa kichwa, nashangazwa jinsi Germany na France yalivyokua mandezi badala ya kusimama imara kupambania umoja wao.
Muhuni kama muhuni, anataka Europe imuinamie yeye US, alianzisha chokochoko za trade war tariffs, mara 5G, akawamimd kumpa Huawei kazi, basi he is a bully!
Kila kitu security Yao tyuu, na siyo wenzake!

Pole SANA Europe Kwa kuzidiwa akili!
 
Ngoja waingie mkenge wa waone watakavyoumia
Natizama habari mda huu UTV, Evona Kamutu amuhoji mmoja wa watanzania anayeishi Alabama, anadai bei ya mafuta Marekani imepanda karibia mara mbili.

Huyo US kishaanza kuumia je wao wenye uchumi wa kuungaunga, bora wafikirie kwa kutumia vichwa vyao kuna na hali yao na si kuendeshwa huku ukimfurahisha UE na kumuumiza mwananchi wa kawaida.
 
Katika kitu ambacho Baiden ali kurupuka ni kwenye vikwazo vya mafuta na hawezi kuvifuta maana akithubutu itakuwa ni aibu ya mwaka.

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
 
Kinachofuata ni Uchumi wa russia kuporomoka, raia wataingia mtaani kuandamana.
Putin kupinduliwa.
Itabaki story, maisha yatarudi kua kawaida.
Vikwazo vya namna hii iliwekewa Iran mwaka 2018 na utawala wa Trump watu wakawa wanasema eti utawala wa Ayatullah unaanguka ndani ya mwaka lakini mpaka sasa hakuna kilicho tokea.

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
 
Kuna maamuzi EU wanafanya sasa hivi hadi mtu unakosa jibu kama wapo timamu au lah? Mfano, uamuzi wa Ujerumani kusitisha nordstream 2 wakati bado wanaingiza gesi kupitia nordstream 1 lakini pia kampuni za ulaya zimewekeza kwenye nordstream 2.

Ulaya kwa sasa wamekuwa watumwa wa Marekani, huu ni ukweli usiopingika.
Tunasitisha Nordstream mbele ya camera na mapichapicha, behind the scenes mambo ni kama kawaida Nordstream inaendelea! Bila Nordstream wanajua wanarudi nyuma! Na uchumi wa nchi nyingi ulitetereka na COVID,
 
Natizama habari mda huu UTV, Evona Kamutu amuhoji mmoja wa watanzania anayeishi Alabama, anadai bei ya mafuta Marekani imepanda karibia mara mbili.

Huyo US kishaanza kuumia je wao wenye uchumi wa kuungaunga, bora wafikirie kwa kutumia vichwa vyao kuna na hali yao na si kuendeshwa huku ukimfurahisha UE na kumuumiza mwananchi wa kawaida.
ila hili lakupanda kwamafuta hata yule mpuuzi BIDEN alilisema ila akawaambia raia wake kwamba inabidi waumie sasa kwabaadae yao iliobora
acha tuone
 
ila hili lakupanda kwamafuta hata yule mpuuzi BIDEN alilisema ila akawaambia raia wake kwamba inabidi waumie sasa kwabaadae yao iliobora
acha tuone
Baadaye ipi??
Hili chaka la miiba na misiba,
UN Kura zilivyopigwa US hakutegemea,
Juzi Kati UAE na Saudi, ma king, wamechomoa kupokea simu za Biden!
Aibu tupu!

Watu imefikia mahali tumewachoka, ni bully of the playground. Nafikiri anaelewa dunia inavyojisikiaga. Anavyokuwaga anamkingia Kifua Israel kwenye issue ya Palestine!
 
hakika
 
Back
Top Bottom