Habari zenu wapendwa, Jamani naomba mnisaidie nina tatizo dogo tu ambalo kadri siku zinavoenda naona linanikwaza, mume wangu kila nikirudi home kutoka job au popote tu lazima atavizia handbag yangu ataipekua, nimeshamkutia karibia mara 15 sikumuuliza wala sikuchukia, juzi nimemkutia tena na hafanyi hivo mbele yangu anapekua kwa usiri hivo ata kumkutia inakuwa ni bahati tu, hiyo ya juzi nilikuwa nimetoka chuo nikaenda kuweka handbag room, nimerudi sitting room nimekaa kama dakika 5 tu akaja nayeye alikuwa chumbani, akachungulia pale sitting room kaniona niko busy na mtoto akarudi tena chumbani, namie hapohapo nikaingia chumbani nikamkuta tena busy anachambua handbag yangu, jamani ata kama kuna kitu anatafuta kwa mara hizo zote angekuwa ameshakipata, mimi binafsi nachukia na nilishawai kumwambia karibuni tu kama mara ya 13 hivi kuwa kwanini unapenda kufungua handbag yangu, unatafuta nin nikamuuliza vipi mimi nikiwa nakagua mifuko yako ya suruali kila ukirudi utajisikiaje maana wanaume hawabebi handbag, nikamwambia naomba uwe na imani na mimi hili jambo kwakweli linanikwaza, tangia nimemwambia hiyo juzi kaninunia mpaka leo hii eid imepita kimyakimya tu, jamani nisaidieni nifanye nini ili huyu mtu awe na imani namm au anatafuta sababu?