tafuta namna ya kumfanya akuamini. kuna kitu lazima.Habari zenu wapendwa, Jamani naomba mnisaidie nina tatizo dogo tu ambalo kadri siku zinavoenda naona linanikwaza, mume wangu kila nikirudi home kutoka job au popote tu lazima atavizia handbag yangu ataipekua, nimeshamkutia karibia mara 15 sikumuuliza wala sikuchukia, juzi nimemkutia tena na hafanyi hivo mbele yangu anapekua kwa usiri hivo ata kumkutia inakuwa ni bahati tu, hiyo ya juzi nilikuwa nimetoka chuo nikaenda kuweka handbag room, nimerudi sitting room nimekaa kama dakika 5 tu akaja nayeye alikuwa chumbani, akachungulia pale sitting room kaniona niko busy na mtoto akarudi tena chumbani, namie hapohapo nikaingia chumbani nikamkuta tena busy anachambua handbag yangu, jamani ata kama kuna kitu anatafuta kwa mara hizo zote angekuwa ameshakipata, mimi binafsi nachukia na nilishawai kumwambia karibuni tu kama mara ya 13 hivi kuwa kwanini unapenda kufungua handbag yangu, unatafuta nin nikamuuliza vipi mimi nikiwa nakagua mifuko yako ya suruali kila ukirudi utajisikiaje maana wanaume hawabebi handbag, nikamwambia naomba uwe na imani na mimi hili jambo kwakweli linanikwaza, tangia nimemwambia hiyo juzi kaninunia mpaka leo hii eid imepita kimyakimya tu, jamani nisaidieni nifanye nini ili huyu mtu awe na imani namm au anatafuta sababu?
ukute kashauriwa na waganga wa kienyeji.............maana siku hizi kuna upuuzi mwingi wa kuleta utajiri. wee unaona bora kipi, akubali kukutoa wewe sadaka, aambiwe asilale kitandani au awe anakagua pochi yako kila siku?Habari zenu wapendwa, Jamani naomba mnisaidie nina tatizo dogo tu ambalo kadri siku zinavoenda naona linanikwaza, mume wangu kila nikirudi home kutoka job au popote tu lazima atavizia handbag yangu ataipekua, nimeshamkutia karibia mara 15 sikumuuliza wala sikuchukia, juzi nimemkutia tena na hafanyi hivo mbele yangu anapekua kwa usiri hivo ata kumkutia inakuwa ni bahati tu, hiyo ya juzi nilikuwa nimetoka chuo nikaenda kuweka handbag room, nimerudi sitting room nimekaa kama dakika 5 tu akaja nayeye alikuwa chumbani, akachungulia pale sitting room kaniona niko busy na mtoto akarudi tena chumbani, namie hapohapo nikaingia chumbani nikamkuta tena busy anachambua handbag yangu, jamani ata kama kuna kitu anatafuta kwa mara hizo zote angekuwa ameshakipata, mimi binafsi nachukia na nilishawai kumwambia karibuni tu kama mara ya 13 hivi kuwa kwanini unapenda kufungua handbag yangu, unatafuta nin nikamuuliza vipi mimi nikiwa nakagua mifuko yako ya suruali kila ukirudi utajisikiaje maana wanaume hawabebi handbag, nikamwambia naomba uwe na imani na mimi hili jambo kwakweli linanikwaza, tangia nimemwambia hiyo juzi kaninunia mpaka leo hii eid imepita kimyakimya tu, jamani nisaidieni nifanye nini ili huyu mtu awe na imani namm au anatafuta sababu?
Shosti huyo hajiamini kama yuko peke yake.lakini kwakweli nitabia mbaya sana mwanamme kufungua Handbag ya mkewe
malezi gani hayo alolelewa? tena usimcheke bora ajue kama hupendi na usichoke kusema,ama sivyo ukimuachia atataka akupekua mpaka kwenye chupi ajue kama umelala namwengine au laa.
Pole N. Ni bora akague na kuondoka kuliko akuibie. Kuna mtu mmoja yeye alimsachi mkewe akitafuta vito vyake vya thamani na akaviiba akenda kuuza na kugawia wanawake mahawara ili awaonyeshe kuwa ana hela. Mkewe alivyostuka ikabidi ahamishe vitu afungie sandukuni tena kwa kofuli na akahamishia chumba cha wageni lile sanduku. Kumbe mwanaume yule akatafuta tena vile vitu vya thamani hakuvipata na siku moja alipoona sanduku lina kofulu basi akasubiri usiku wamelala akaamka na akaenda kuvunja lile kofuli la sanduku na kuiba vile vito vya mke wake pamoja na vitu vya thamani. Kesi hii ilitua kwangu na kwa tathmini ya haraka haraka ilionekana alichukua vitu vya zaidi ya milion 60 vya huyu mkewe. Nilisuluhisha but kwa kweli hadi ninapoandika hapa ile ndoa ni gumzo. Hakuna amani kabisa na mke alikuwa ni mama wa familia kwa kujitoa sana kumsaidia mume kwa kuwa mume ni the so called wafanyabiashara wasio na ofisi mujini!!!
Ni jambo la fedheha kumkagua mwenzako hasa kama mwenzi huyo hana tabia za kutia wasiwasi. Na mbaya zaidi kumwibia!!! Yaani hadi leo nikikumbuka kisa hiki huwa natema mate kisikumbe kizazi changu. Mume kumuibia mke ni laana ambayo haina kipimo, mbaya sana.
Asante kaka, naona wengi kweli wamenishauri nimpatie kabisa mkoba nitakuwa nafanya hivo
ni sawa tu na kupekua sms na phonebook ya simu zako,sasa fanya hivi we ukirudi tu toka job mpelekee pochi mwambie sachi dia
Hiyo red dah imenigusa mie hutendwa hivyo kila mara mpaka siku hizi vitu vyangu naweka ofisini naacha huko kabisa na hata pesa natembea na ya kutumia siku hiyo hiyo tu
Hivi unamaanisha? Nikajua unatania aisee! Kwangu hata maid asie muaminifu simuwezi, bora kahaba! Nina colleague anafungiaga hela ofisini ama anatupa tumuwekee. Ila yeye mumewe haibi, anazipangia matumizi! Unakaaje na mwanaume mwizi!!!! Uwiiii! Si unaishi kama stendi!