Handbag ya Madam II - Nimepewa talaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Handbag ya Madam II - Nimepewa talaka

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by naima79, Sep 17, 2012.

 1. naima79

  naima79 Senior Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 186
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  H
   
 2. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  huyo alikuwa obsessed na wewe,hakuwa na mapenzi,kumpenda mtu ni pamoja na kumpa uhuru wake binafsi na kumuamini!ni ndoa hiyo lakini kwa minajili hiyo atakusumbua sana kimsingi!pole mwaya ndo ukubwa !
   
 3. naima79

  naima79 Senior Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 186
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Asante my dear
   
 4. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  kuna dalili nyingi sana za mapenzi ya kitesaji mojawapo ni hiyo,huwezi kukipenda usichoamini ni chako!
   
 5. E

  ESAM JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Kwanza pole sana dada Naima79 hayo ni matatizo na matatizo huwapata wanadamu. Sijui nianzie wapi. Tatizo kubwa ninaloliaona kwa huyo mume wako zaidi ni utoto tu unamsumbua na hauwezi kumsaidia. Pia inaonekana yeye ni mbinafsi sana ambaye anajiona yeye tu ndio mwenye haki ya chochote anachotaka na sio mtu mwingine. Sasa mtu akiwa na tabia kama hizo kubadilika sio kitu rahisi. Kwa vyoyote atakuwa over 30 kama ni hivyo inawezekana uzoefu wake katika ndoa sio muda mrefu na hivyo akikaa muda wa kutoka katika ndoa atagundua kwamba hayo anayoyafanya hayasaidia.
  Pia inawezekana tayari moyo wake umetekwa na mwanamke mwingine kwa hiyo anatafuta namna ya kukuondoa ili apate nafasi ya kuwa na huyo ndiyo maana hata kwenye thread umekiri kwamba alikuwa anatafuta sababu ya kukufukuza. Je wewe huna taarifa za yeye kutoka nje ya ndoa? Halafu kusema usirudiane naye inategemea kwani ndoa yenu kama ni ya Kikristo hiyo haifunguki mpaka kifo vinginevyo mtajipeleka katika maisha ya uzinzi. Kama atataka mrudiane naomba usikatae, ila umwekee masharti usikubali kuwa mnyonge tu siku zote vinginevyo utakufa kwa pressure. Masharti: lazima akuheshimu kama mtu ambaye una haki ya kuwasiliana na watu wengine hata kama ni wa jinsia nyingine kwa wewe hukukua kama kisiwa na kukutana na yeye peke yake ya jinsia ya kiume; una uhuru wa kuwa na privacy sio lazima uwe na password za mawasiliano yako labda ukimpa kwa hiari; akutambua kwamba wewe ni mwanadamu unayestahili heshima kama anavyotaka heshima yeye, wewe sio kitu au mali yake, bali mwenza. Akikubali hayo kwa dhati rudiana naye tu na mengine unaweza kuvumilia kwa hakuna mwanadamu aliye mkamilifu. Asante dada yangu, ubarikiwe
   
 6. Eversmilin Gal

  Eversmilin Gal JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 783
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  pole kwa yaliyokukuta mpenzi sababu ameipata na ameitumia ila kuachana siyo rahisi hasa kama ulikua unampenda na sie wanawake tulivyokua na tabia ya kusahau utakuja kuombwa msamaha na utarudiana na mmewe na wale wote kwa njia yeyote ile walitaka uachane nae utawaona wabaya
   
 7. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Achana naye atakuletea magonjwa ya siyo na tiba kama ya moyo.
  Chukua hatua kata shauri maisha ni popote utapata mwingine kama unaamini sna ktk ndoa.
   
 8. s

  sindo Senior Member

  #8
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Pole mwaya, wanaume wengine migogoro tu, Ningekuwa mimi nafikiri ingekuwa basi maana, isije ikawa nenda rundi ndio maisha . huyo sio mume wa kutegemea tafuta mwingine wa kufaa
   
 9. s

  sindo Senior Member

  #9
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  hapo, ukimwi au ugonjwa wa moyo, na kuzeeka haraka sababu ya stress angalia
  PIGA CHINI TU TAFUTA MWINGINE POLEPOLE
   
 10. naima79

  naima79 Senior Member

  #10
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 186
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Asante sana kaka Esam nashukuru kwa ushauri ubarikiwe pia, sisi tulifunga ndoa ya kiislam maana wote sie ni waislam
   
 11. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Peleka tatizo hili kwenye sala (kwa MUNGU)...
  Kama hii ndoa is from heaven, then will never breakup...!!
  Muombe MUNGU aibadilishe ndoa yenu..!!
   
 12. s

  sindo Senior Member

  #12
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Ni kweli kabisa peleka tatizo kwa mungu,
  Ikiwezekana funga kabisa uliombee,
  Lakini kurudiana KWA MATAZAMO WANGU HAPANA
  MUOMBE MUNGU AKUPE MUME MWINGINE ANAYEKUFAA, utapata tu
   
 13. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Pole kwa yaliyokukuta, ndoa saa nyingine zina changamoto zake, ambazo baadhi yake ndiyo kama hizo zilizokukuta. Maelezo uliyoyatoa yanaonyesha wazi kuwa mumeo ni mtu mwenye wivu wa kupindukia, i mean mpaka umepitiliza, kitu ambacho kinakufanya muda mwingi ujikute kana kwamba unawindwa au kutafutiwa sababu ya kuachwa. Katika maelezo yako, sijaona sehemu yeyote ile uliyosema au kuhisi kuwa mumeo ana nyumba ndogo au msichana anayedate naye kitu kinachonifanya niamini kuwa wivu wake inawezakana si sababu ya kukutafutia talaka.

  Jambo hili mi naliangalia kwa mtazamo tofauti kidogo. Pamoja na madhaifu ya mumeo kwenye wivu uliopitiliza, lakini kwa namna moja au nyingine na wewe pia uliteleza kidogo kwa kuendeleza mawasiliano na mtu ambaye tayari alikuonya naye mara kadhaa hata kama mawasiliano yenu yalikuwa si ya kimapenzi (Maana hata ningekuwa mimi mtu nimhisi ana uhusiano na mke wangu, nimuonye mke wangu then nibaini kuwa bado wawasiliana nafikiri ningekuwa mkali maana hiyo ni dalili ya dharau au kutokujali). BF wa rafiki yako ana thamani gani mbele ya ndoa yako? Pamoja na kuwa umejitetea uliwasiliana kwa sababu ya huo msiba wa rafiki yako na taharuki uliyokuwa nayo, kuinusuru ndoa yako either ungefuta namba ya simu baada ya kupiga au kutumia simu yeyote kuwasiliana na huyo kaka maana ndoa kwako ni muhimu zaidi kuliko marafiki na ulikuwa unajuwa wazi kuwa mumeo hukagua simu yako! Kinga huwa ni bora zaidi kuliko tiba!

  Kwa ushauri, sifahamu umedumu kwenye ndoa kwa miaka mingapi na una watoto wangapi ila binafsi sifurahii ndoa kuvunjika kirahisi hivi (na wala si jambo la kufurahia) kwa sababu ya wivu tu, maana huwa siamini kuwa talaka ni suluhu ya migogoro ya ndoa na pia hujui huyo atakayefuata atakuwa wa aina gani, probably mbaya zaidi kuliko uliyenaye. Nakushauri tafuta namna ya kuongea na mumeo kupitia kwa wazee na ndg wa karibu kujaribu kufanya suluhu. Kama suluhu itapatikanika, ni vyema na wewe kufunguka kuyaeleza mambo yote mabaya anayokutendea, na kwa mtindo huo unaweza kujikuta umelinda ndoa yako na pia kwa wakati huo huo pia umemfunza mumeo kwa tabia zake mbaya za wivu uliopitiliza.
   
 14. s

  sindo Senior Member

  #14
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  kuchelewa kurudi nyumbani ni dalili mbaya, saa saba! mh inatisha kuangalia handbag sio mbaya si anataka kujiridhisha, yeye je anakubali kupekuliwa?
   
 15. E

  ESAM JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Inapendeza mtoto kukua akiwa na wazazi wake wote wawili wakiishi pamoja kama mke na mume, hiyo inasaidia kumjenga ili na yeye aige mfano wao. Kwa hiyo sisi wazazi tunaweza kuwa na matatizo yetu lakini cha msingi ni kufanya kila linalowezekana kuishi pamoja na kuandaa kizazi bora cha baadae kupitia watoto wetu. I wish you a lot of success
   
 16. E

  ESAM JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Huo ni utoto kwa mwanaume anayejiamini huwezi kufanya ujinga huu, yaani ili kuishi maisha bora ya ndoa bila pressure lazima kuaminiana, vinginevyo kama humwamini mtu ya nini kuingia naye katika ndoa?
   
 17. naima79

  naima79 Senior Member

  #17
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 186
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kibweka mimi huwa namuomba mungu sana katika sala zangu, na kwa bahati nzuri mimi nasali sala 5, hivo kila sala yangu siachi kumuomba mungu
   
 18. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,250
  Trophy Points: 280
  Kwa sababu mmeachana kwa sababu zisizo na kichwa wala mkia, mtarudiana tu. Lakini mshikishe adabu. Usipopata uhuru wako kipindi hichi hutakaa uupate tena.
  Kwanza badilisha password za accounts zako zote. Kama anakuamini upya then hahitaji kukufanyia monitoring tena. Pili mkubaliane mambo ya msingi. Kama yeye ana marafiki na anaweza kuwasiliana nao basi nawe sawia.
  Haya yote mpeane muda wa kupumua kwanza. Hebu kaa kwa dada yako uone utakavyofurahia stress free life. Usimtegemee kurudi kukutafuta, na wewe usitafute mambo yake ili usiumie. Hilo gereza la ndoa, either utoke ama ujitengenezee utaratibu wa kumudu mazingira. Muonyeshe upo uwezekano wa wewe kumuacha na kuendelea na maisha pia.
   
 19. naima79

  naima79 Senior Member

  #19
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 186
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Asante kwa ushauri kaka na nimekkuelewa vema kabisa na nimekiri kosa pia, ila maoni yako ni muhimu sana kwangu
   
 20. E

  ESAM JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Yaani kaka hiyo paragraph ya pili siwezi kukubaliana na wewe, yaani mtu uache kuwasiliana na watu eti kwa sababu kuna mtu fulani hata kama anaitwa mke au mume anayo mawazo ya kijinga kuhusiana na mawasiliano hayo? Cha muhimu kufanya ni kumfahamisha huyo mtu ni nani na lengo la mawasiliano yenu ni nini? Kwa sababu kumbuka huyo mke ulikutana naye akiwa tayari mtu mzima huwezi hata siku moja kufikiri kwamba hajawahi kuwa na uhusiano na watu wengine shuleni, kazini, nyumbani na kwingineko. Jambo la msingi ni kuaminiana vinginevyo mtu akiamua kutoka nje ya ndoa anaweza akakuomba hata wewe mwenyewe kumsindikiza na ukamsubiri na mkarudi wote kumbe alienda kukutana na mwenzake. NI NGUMU SANA KUFIKIRI KWAMBA UNAWEZA KUMDHIBITI MTU MWENYE KICHWA KIMOJA NA UBONGO MMOJA KAMA WEWE KWA KUTUMIA KICHWA NA UBONGO HUOHUO MMOJA. Poor husbands with such stupid behaviour
   
Loading...