Hamisi wa Bongo Star Search uwezo wake mdogo

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
13,576
18,894
Leo niliangalia marudio ya Bongo Star Search ya Jumapili nimeona kabisa huyo Hamisi uwezo wake wa kuimba ni mdogo sana wakati wenzake uwezo wao ni mkubwa. Na amshukuru Mungu kufika hatua ya 10 Bora, hakustahili kufika hatua hiyo.

Ifike kipindi watanzania tuache unafiki pale Bongo Star Search wanaangalia kipaji na si mtu kutia huruma na washiriki wote wameenda kwa ajili ya kutafuta nafasi ya kuonekana na pia kutafuta maisha kupitia vipaji vyao.

Hitimisho: kiukwel Bongo Star Search ya mwaka huu ndio yenye vipaji vikubwa kuliko Bongo Star Search zote kwa mtazamo wangu. Kwa upande wangu nimewakubali hawa watu Frank, Mshaki na Leonard - wanafanya poa sana.
 
yule bwana wa chitohori ali sema ana msign dgo mahaba aya ...sijui alkua ana taka apite na upepo
 
sijapata nafasi ya kufuatilia nashindano haya ila kwa baadhi ya clip nlizozitazama ni kweli Hamisi anapendwa ila habhana kipaji cha kuimba labda kupiga gitaa
 
Huyo Hamis anazingua aende huko akasainiwe na kina mboto kwnye comedy
 
Halafu kwann anacheza vile Hamisi kulala chin na kujinyanyua miguu sio sir mm nilikuwa namuonea huruma sana mpk nikajikuta nimekuwa namfatilia ila nimegundua kuna vipaji mule vikar
 
Kwa ufupi bongo star seach haina majaji, pamoja na kuwepo wote kulipaswa kuwe na mtaalamu wa mziki ambae hajaji tu kwa sikio bali kwa utaalamu. Master J ni producer sawa lakini si mtaalamu wa muziki.

Kuna makosa mengi ya kiufundi wanafanya, na majaji wanayajua ila wanashindwa kuyaeleza kitaalam. Rejea show ya wiki iliopita december 3 kama sikosei. Kuna mshiriki aliimba, J dee aka sense kuna tatizo sehemu flani, akaishia kusema una sauti lakin kuna kitu sijui nini labda Master J anisaidie.

Master J akaishia blah blah, Dully nae aka comment nashindwa kuelewa sijui mikia, na hili neno mikia ndio linaniua zaidi, ya pigo kuwa kamili ndio mikia. sasa kama jaji anashindwa jua tatizo hasa la muimbaji kisauti ana jaji nini?

Kuna mshiriki anaitwa fatuma katika show hiyohiyo ya jumapili, alianza na ufunguo wa chini wimbo wa Nandy, na akawa anaenda off key kila akitaka kupanda. Ila majaji wanaishia tu kusema bado kuna tatizo sehemu.

All in all mwalimu wao wa sauti anapaswa kuongeza juhudi maana karibu waimbaji wote wanakosa voice control, hasa wanapotaka kuhit high notes. Tatizo hili hadi yule muimba na gitaa mwenye vocal nzuri.
 
Leo niliangalia marudio ya Bongo Star Search ya Jumapili nimeona kabisa huyo Hamisi uwezo wake wa kuimba ni mdogo sana wakati wenzake uwezo wao ni mkubwa. Na amshukuru Mungu kufika hatua ya 10 Bora, hakustahili kufika hatua hiyo.

Ifike kipindi watanzania tuache unafiki pale Bongo Star Search wanaangalia kipaji na si mtu kutia huruma na washiriki wote wameenda kwa ajili ya kutafuta nafasi ya kuonekana na pia kutafuta maisha kupitia vipaji vyao.

Hitimisho: kiukwel Bongo Star Search ya mwaka huu ndio yenye vipaji vikubwa kuliko Bongo Star Search zote kwa mtazamo wangu. Kwa upande wangu nimewakubali hawa watu Frank, Mshaki na Leonard - wanafanya poa sana.
Asante kwa kuniwakilisha.
 
Huyo Hamis anazingua aende huko akasainiwe na kina mboto kwnye comedy
hahahaaaa lakini anaweza akafanya mziki wa kwake tofauti cha msingi afanye mazoezi zaidi
ila kwenye mashindano haya hana lolote nnachopenda toka kwake ni upigaji wa gitaa tu na si uimbaji
 
Back
Top Bottom