kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,000
- 17,909
wa Palestina wajibu mapigo baada ya Israel kumuua shahidi kamanda wa Jihad Islami
Nov 12, 2019 08:07 UTC
Wanamuqawama wa Palestina wametoa jibu kali baada ya jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel kumuua shahidi kamanda wa ngazi za juu wa Harakati ya Jihadul-Islam ya Palestina katika Ukanda wa Gaza.
Katika taarifa, tawi la kijeshi la harakati hiyo ya muqawama imesema Baha Abu al-Ata, kamanda wa Kikosi cha al-Quds aliyekuwa na umri wa miaka 42, ameuawa katika shambulizi la anga la jeshi la Israel dhidi ya makazi yake katika Ukanda wa Gaza mapema leo Jumanne.
Taarifa hiyo imesema mke wa al-Ata ameuawa shahidi pia katika shambulizi hilo la kinyama dhidi ya nyumba ya kamanda huyo katika eneo la Shejaiya, huku watu watatu wakijeruhiwa.
Muda mfupi baada ya mauaji hayo, wanamuqawama wa Palestina wameanzisha mashambulizi ya ulipizaji kisasa kwa kuvurumisha maroketi dhidi ya Israel, ambayo yamelenga miji ya Tel Aviv, Sderot na Ashdod.
Utawala haramu wa Israel umetiwa kiwewe na mashambulizi hayo ya ulipizaji kisasi, na umewataka wanafunzi na wanachuo wasiripoti shuleni na vyuoni katika mji mkuu Tel Aviv na miji mingine mikubwa, sawa na wafanyakazi 'wasio wa dharura'.
Aidha utawala huo batili umetoa tahadhari ya mijumuiko na mikusanyiko katika maeneo ya umma.
Wakati huohuo, Harakati ya Muqawama ya Palestina (Hamas) imesema utawala wa Kizayuni wa Israel utabeba dhima ya matokeo mabaya ya kuwasha moto wasioweza kuuzima, huku ikiapa kulipiza kisasa cha damu ya al-Ata.
Tags
ISRAEL GaZA