Hamas wajibu, Israel miji yapigwa shule na vyuo vyafungwa

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,839
17,437
wa Palestina wajibu mapigo baada ya Israel kumuua shahidi kamanda wa Jihad Islami
Nov 12, 2019 08:07 UTC

Wanamuqawama wa Palestina wametoa jibu kali baada ya jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel kumuua shahidi kamanda wa ngazi za juu wa Harakati ya Jihadul-Islam ya Palestina katika Ukanda wa Gaza.

Katika taarifa, tawi la kijeshi la harakati hiyo ya muqawama imesema Baha Abu al-Ata, kamanda wa Kikosi cha al-Quds aliyekuwa na umri wa miaka 42, ameuawa katika shambulizi la anga la jeshi la Israel dhidi ya makazi yake katika Ukanda wa Gaza mapema leo Jumanne.

Taarifa hiyo imesema mke wa al-Ata ameuawa shahidi pia katika shambulizi hilo la kinyama dhidi ya nyumba ya kamanda huyo katika eneo la Shejaiya, huku watu watatu wakijeruhiwa.

Muda mfupi baada ya mauaji hayo, wanamuqawama wa Palestina wameanzisha mashambulizi ya ulipizaji kisasa kwa kuvurumisha maroketi dhidi ya Israel, ambayo yamelenga miji ya Tel Aviv, Sderot na Ashdod.

Utawala haramu wa Israel umetiwa kiwewe na mashambulizi hayo ya ulipizaji kisasi, na umewataka wanafunzi na wanachuo wasiripoti shuleni na vyuoni katika mji mkuu Tel Aviv na miji mingine mikubwa, sawa na wafanyakazi 'wasio wa dharura'.

Aidha utawala huo batili umetoa tahadhari ya mijumuiko na mikusanyiko katika maeneo ya umma.

Wakati huohuo, Harakati ya Muqawama ya Palestina (Hamas) imesema utawala wa Kizayuni wa Israel utabeba dhima ya matokeo mabaya ya kuwasha moto wasioweza kuuzima, huku ikiapa kulipiza kisasa cha damu ya al-Ata.

Tags
ISRAEL GaZA
4bsnf5b0a0208c1j9r9_800C450.jpeg
4bsn198e655ffa1j9qw_800C450.jpeg
 
Hizi rockets za Wapalestina hazina shabaha ndo maana zinakosa kuleta athari kubwa.Zinaleta hofu zaidi. Mpaka sasa waliothibitika kufa sijaona. Lakini pia tumejua tu Iron Dome ya Israel ni dhaifu mno ikikutana na rockets kama za Iran haifui dafu
 
Hamas ni wachumba tu hapo wangekuwa wamechokozwa Hezbollah kornet zingekuwa zimeshavunja deraya kadhaa za idf
Hezbollah waliionya Israel ikitaka kutaabika imuue mkuu wa kundi hilo. Ni mara kadhaa makamanda wa IDF wanataka kumuua Hassan Nasrallah tokea miaka ya 1990s hadi leo wanasita. Huyu aliyekufa kundi lake dogo na halina nguvu sana
 
Usahihi wa taarifa yako upo kwenye kuuawankwa huyo Kamanda wenu. Hayo mambo ya kuvurumusha bila malengo ni uwendawazimu uliozoeleka na sasa umekuwa sehemu ya masisha yao ya kila siku. Ndani ya Tel Aviv na kwingineko kote ndani ya Israel maisha yanaendelea kama kawaida na watalii ni wa kumwaga tu, sana sana ni ving'ora vya tahadhari au wakati makimbora yanadunguliwa kitu ambacho pia ni utalii wa kijeshi.
 
wa Palestina wajibu mapigo baada ya Israel kumuua shahidi kamanda wa Jihad Islami
Nov 12, 2019 08:07 UTC
Wanamuqawama wa Palestina wametoa jibu kali baada ya jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel kumuua shahidi kamanda wa ngazi za juu wa Harakati ya Jihadul-Islam ya Palestina katika Ukanda wa Gaza.
Katika taarifa, tawi la kijeshi la harakati hiyo ya muqawama imesema Baha Abu al-Ata, kamanda wa Kikosi cha al-Quds aliyekuwa na umri wa miaka 42, ameuawa katika shambulizi la anga la jeshi la Israel dhidi ya makazi yake katika Ukanda wa Gaza mapema leo Jumanne.
Taarifa hiyo imesema mke wa al-Ata ameuawa shahidi pia katika shambulizi hilo la kinyama dhidi ya nyumba ya kamanda huyo katika eneo la Shejaiya, huku watu watatu wakijeruhiwa.
Muda mfupi baada ya mauaji hayo, wanamuqawama wa Palestina wameanzisha mashambulizi ya ulipizaji kisasa kwa kuvurumisha maroketi dhidi ya Israel, ambayo yamelenga miji ya Tel Aviv, Sderot na Ashdod.
Utawala haramu wa Israel umetiwa kiwewe na mashambulizi hayo ya ulipizaji kisasi, na umewataka wanafunzi na wanachuo wasiripoti shuleni na vyuoni katika mji mkuu Tel Aviv na miji mingine mikubwa, sawa na wafanyakazi 'wasio wa dharura'.
Aidha utawala huo batili umetoa tahadhari ya mijumuiko na mikusanyiko katika maeneo ya umma.
Wakati huohuo, Harakati ya Muqawama ya Palestina (Hamas) imesema utawala wa Kizayuni wa Israel utabeba dhima ya matokeo mabaya ya kuwasha moto wasioweza kuuzima, huku ikiapa kulipiza kisasa cha damu ya al-Ata.
Tags
ISRAEL GaZAView attachment 1261718View attachment 1261719

Umetafsiri ww au nani?

Umesema Hamas? au umekunywa kidogo? Maana Hamas wamesema wanafikilia kuwaunga mkono Islamic Jihad endapo mashambulizi hayatositishwa... Kuna uwezekano kuwa Hamas wametoa Ushirikiano kwa Israel kisiri maana huyo Gaidi alikuwa anawasumbua pia Hamas na inawezekana baada ya Bomu la kutegwa linalosadikiwa lilitegwa na kundi hilo na kuwaua Makamanda wa Hamas kisha Islamic Jihad wakawasingizia Israel hamas hawakukubali wakachunguza Wakapata Majibu kuwa ni Islamic Jihad na kiongozi wao ndio huyo Dogo aliyedanjishwa na Israel. so kuna bifu kali sana kati ya Islamic Jihad dhidi ya Hamas
 
Wanamuqawama ni wadau ambao walimgomea Nuhu kujenga safina ambao bado wanaishi mpaka sasa huko Palestinian
Sasa walisave vipi wakati waliangamia kwa gharika? Japo walikuwa mafundi wa kuogelea lakini lango la safina Nuhu hakujua jinsi ya kulifungua kwani PIN za kufungulia alikuwa nazo mwenyewe Muumba, wakati huo akitoa kipigo kikari kwa wafwasi wa shetwain
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom