dos santos
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 256
- 128
Nilifuatilia kwa makini saana mdahalo ulowakutanisha mbunge wa wawi mh hamad rashid kiongozi wa kambi ya upinzani isiyo rasmi na mbunge wa hai mh freeman mbowe ambaya ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni.Ukiacha ushabiki wa vyana Hamad Rashid alionesha uelewa mkubwa mno wa kile alichokuwa akikieleza zaidi ya mwenzake mbowe ambaye alikuwa akizungumza hoja ambazo hakuelewa nini msingi wake au amelishwa.Ni kama mtu aliyekaririshwa halafu akakuta kitu tofauti.Hamad alijibu maswali kitaalamu na kiufundi ambapo mbowe alikuwa akilalamikia cuf juu ya katiba(kama vile wameiweka wao) na kuuliza maswali ya jf yasiyo na kichwa wala miguu.Hakuonesha umakini ila udhaifu na kiasi cha kuzua naswali mengi namna kambi ya upinzaji chini ya uongozi wake hali itakuwaje.
Ukweli mbowe siasa bado,aendelee kujifunza kwa wanasiasa wakongwe.
Mdahalo umeonyesha Hamad Rashid usiku ule alikuwa kama mlima kilimanjaro na freeman mbowe kama kichuguu,kiasi ilimfanya mwenyekiti wa mdahalo awe anaingilia kati kumnusuru mbowe kiasi kilichopelekea mashabiki wa cuf waingilie kati kiasi cha kutaka kupelekea mdahalo uvunjike.
Ilikuwa kama watu walioandaa mechi katika uwanja wao,refa wao,kikombe chao, mwisho wanapigwa mabao na wanabaki na mshangao.
ni mtazamo tu