nadhani heading yako ilitakiwa kuwa hiviii mpinzani halisi vs. Mamluki
Tuangalie kwa mtazamo wa taifa zaidi,chadema imejikita bara na imespread maeneo tofauti imepata wabunge huku ccm ikichukua sehemu kubwa zaidi,CUF ZNZ tena Pemba tu,ccm Unguja.sasa nafikiri CUF itazamwe kama ya upande fulani ambao imepata umaarufu wa mkumbo mkumbo tu.Ni kweli wapemba wengi kwa akili zao na fikra huru wamekubaliana na mustakabali wa CUF?au Unguja wengi wao CCM? Je hapa haitupi mashaka kidogo kuwa kinachopiganiwa ZNZ sio siasa tunazozijua bali ni ushindani wa makundi kwa itikadi wa sehemu wanazotoka na si itikadi za vyama kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla?ukiwasikiliza CUF na CDM vizuri katika swala la kuunda kambi ya upinzani bungeni,kama unapendelea upinzani ueendelee kukua sidhani kama utakubaliana na CDM kuishirikisha CUF achilia vyama vingine ambavyo vilishaonyesha wazi kuegemea upande wa ccm.
Kwa vile maamuzi ya muungano wa upinzani bungeni ni wa hiari kwa CDM kuwashirikisha wengine tuwaache waamue kwa utashi wao,na CUF wasilalamike kwani CDM wanayo haki ya kisheria na wao CUF hawawezi kuidai popote nafasi hiyo.Wasubiri uchaguzi ujao kama watabahatika tena kuipata nafasi hiyo.
Mbowe ni mtoto mdogo tu katika historia ya Zanzibar
Chadema musitulilie sisi bali lilieni na bunge la tanzania ambalo limewakosesha haki zenu za kupiga kura,na haki nyengine za msingi,sisi zanzibar tunalilia na baradha letu la wawakilishi kwani ndio lenye maamuzi yote wakisema tuitishe kura ya maoni juu ya muungano tukisema noo basi tumeuvunja,tukisema serikali tatu basi tutahakikisha serikali tatu zimekuwa au tumevunjaa muungano.
Tafuta magazeti mengine zaidi ya MwanaHalisi halafu ndiyo utajua kuwa CUF ina wabunge kutoka mikoa gani kabla ya kuandika madai ya utumbo ya hapo juu. Umefunga milango ya akili yako ndiyo maana ufahamu wako wa mambo ya siasa yamejifunga kiasi cha kutoa madai ya utumbo!
Nilifuatilia kwa makini saana mdahalo ulowakutanisha mbunge wa wawi mh hamad rashid kiongozi wa kambi ya upinzani isiyo rasmi na mbunge wa hai mh freeman mbowe ambaya ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni.Ukiacha ushabiki wa vyana Hamad Rashid alionesha uelewa mkubwa mno wa kile alichokuwa akikieleza zaidi ya mwenzake mbowe ambaye alikuwa akizungumza hoja ambazo hakuelewa nini msingi wake au amelishwa.Ni kama mtu aliyekaririshwa halafu akakuta kitu tofauti.Hamad alijibu maswali kitaalamu na kiufundi ambapo mbowe alikuwa akilalamikia cuf juu ya katiba(kama vile wameiweka wao) na kuuliza maswali ya jf yasiyo na kichwa wala miguu.Hakuonesha umakini ila udhaifu na kiasi cha kuzua naswali mengi namna kambi ya upinzaji chini ya uongozi wake hali itakuwaje.
Ukweli mbowe siasa bado,aendelee kujifunza kwa wanasiasa wakongwe.
Mdahalo umeonyesha Hamad Rashid usiku ule alikuwa kama mlima kilimanjaro na freeman mbowe kama kichuguu,kiasi ilimfanya mwenyekiti wa mdahalo awe anaingilia kati kumnusuru mbowe kiasi kilichopelekea mashabiki wa cuf waingilie kati kiasi cha kutaka kupelekea mdahalo uvunjike.
Ilikuwa kama watu walioandaa mechi katika uwanja wao,refa wao,kikombe chao, mwisho wanapigwa mabao na wanabaki na mshangao.
ni mtazamo tu
Nilijua wanaccm humu jf watasema ninayo yasikia lakini ukweli ni kwamba mbowe alimfunika vibaya mamuluki kwa point zifuatazo.
1. Kwa kanuni za bunge chadema inaruhusiwa kuunda kambi ya upinzani bila kutishwa wala kuingiliwa na mamluki yeyote
2. Kwa cuf kuwa nusu serikali nusu upinzani siyo rahisi kukurupuka kuwahusisha kwenye kambi ya upinzani
3. Cuf walisusia serikali ya zanzibar 1995, 2000, 2005 yet waliunda kambi ya upinzani anashangaa nini chadema kuunda
4. Kususia hotuba ya rais chadema hawajavunja kanuni yoyote ya bunge wala shria yoyete ya tanzania ila walicheza krata yao vizuri kuibua mjadala wa katiba mpya, na tume huru ambavyo cuf wameshindwa kuvitekeleza.
5. Ilikuwa aibu na uelewa mdogo kwa hamad kuleta mambo ya udini kwenye mdahalo eti niliongea na ndesamburo akaniambia eti cuf sisi wadin bullllllllllllshit hamadi
6. Inaonesha wazi kuwa hamadi ameumia million 200 alizokuwa akipatiwa kama kiongozi bungeni
7. Hamadi alishindwa kufafanua ikiwa cuf inalenga serikali ya umoja wa kitaifa mbona hawajashirikisha vyama vyote zanzibar katika ndoa yao?
8.hamadi alishindwa kufafanua atawezaje kuwa mpinzani wakati yeye ni sehem ya serikali
9. Hamdi amaeshindwa kuelewa kuwa mabadiliko ndani ya bunge hayawezikani bila pressure ya umma nje ya bunge -kwakuwa ndani ccm imejaza mbumbumbu wapiga makofi
10. Kwa ujumla mbowe was cool and hamdi alikuwa na hasira saana hadi pale walipoitwa ccm wakataka kupiga ngumi
hongera rosemary mwakitwange
kwenye ushabiki elimu haifui dafu ila ukweli rashidi alionyesha upeo kuliko freeman.......
alionyesha upeo gani, anajisifia kuua watu zanzbar, wameshirikishwa singo na ccm wanadhani albam ni yao. sera na ilani zinazotekelezwa na serikali ni za ccm cuf wamewachuuza wazenji wakafa, wanachofia madaraka kwa maalim seif. ovyoo!