Halotel wanawaibia wateja

Halotel wanawaibia wateja

Nawe unafikiri ni vichaa?kagua vizuri una deni au umeshajiunga na pata Salio automatically, Fanya HV,tuma SMS OFF,Kwenda,14963
 
Yaani hapa nimetoka kununua line ya mtandao mwingine yenye 4G

The good thing ni kwamba huwa natumia halotel kwa Internet tu ila whtsup namba inayo apper ni ya kampuni nyingine ambayo haioko vizuri upande wa net

Sasa jana Nilijiunga kifuruchi cha mwanachuo cha halotel kila nikibrowse hamna kitu kucheki salio la kifuruchi ziro yaani ni kitendo cha dakika hiyo hiyo
Nikasema poa watuwanalalamikaga kuhusu huu mtandao labda leo zamu yangu kuibiwa nikaona mia tano sio issue nikajiunga tena vilevile

Nikachomoa li laini sijui nimelitupa wapi na nilikua nachat niko katikati ya maongezi sijamind vi mia tano namaindi usumbufu
SITAKI KUSIKIA IYO KITU-HALOTEL
Hamuulizi mawakala wenu jinsi ya kujiunga vifulushi,pia internet ya baadhi ya siyo automatic, so INA bidi uzijue access point, zake
 
Halotel waliniibia kifurushi changu cha internet kisicho na kikomo cha mwezi, eti baada ya Siku 4 naambiwa kimeisha. Kimeishaje wakati hakina limit ya mb? Mwisho wake ni siku 30. Niliwasha moto mpaka kikarudishwa. Na sitaki tena kusikia kitu inaitwa halotel.
 
Ni Mara kadhaa Sasa nikiingiza Salio kuanzia 1000 na kuendelea wanakata Salio langu na kusema limelipwa deni. Wakati sijawahi kukopa hata siku moja ktk mtandao wa halotel.
Leo nimeingiza Salio la 1500 nimekatwa Nasema hawa jamaa hawako makini na kazi zao wasidhani huu ni ulimwengu ule kipindi mtandao ya simu inaanza.
Nitaambatanisha hapa SMS zao walizokata pesa wanaonesha muda niliokopa ni usiku wakati simu Yangu automatically inajizima SAA tano kamili usiku na kujifungua SAA kumi na mbili kamili asubuhi kila siku. Ndio maana Nasema hai ni wezi maana huo muda Mimi nakuwa tayari nilisha lala.

SMS zao ni hizo ;

(PATASALIO)
Akiba yako imekatwa kiasi cha Tsh 500 kwa malipo ya mkopo, tarehe 2017/02/04 00:43:35. Deni ni Tsh 600. Ahsante!

(PATASALIO)
Akiba yako imekatwa kiasi cha Tsh 51 kwa malipo ya mkopo, tarehe 2017/02/04 00:43:35. Deni ni Tsh 549. Ahsante!

Labda wanawaibia ili waweze kupata Pesa za kuendeshea Kesi yao inayowakabili baada ya Mabosi wao kukamatwa.
 
mmetumwa na mitandao mengne nyny si bure

Well said mkuu, WaVietNam watakuwa na shida gani kuwaiibia waswahili - tusitake kuwasingia bila sababu - Watanzania wakati mwingine tunakuwa wazushi sana - mfano mwezi uliopita watu walidai eti haloTel imefunga mitambo ya kupwepa kulipa kodi stahiki eti Mkurugenzi mkuu wa Halotel alishirikiana na Wapakistani kutekeleza wizi huo - baadae ikaja gudurika kwamba HaloTel ahusiki a ujinga huo ni kampuni nyingine kabisa ndiyo ilikuwa inatumia SIM cards za haloTel kufanya udanganyifu.
 
Labda wanawaibia ili waweze kupata Pesa za kuendeshea Kesi yao inayowakabili baada ya Mabosi wao kukamatwa.

Mkuu HaloTel hawana kesi yoyote mahakamani, watuhumiwa wanatoka Kampuni nyingine kabisa - kampuni hiyo ya kitapeli ndiyo ilikuwa inatumia SIM cards za HaloTel kufanya udanganyifu.
 
Mkuu HaloTel hawana kesi yoyote mahakamani, watuhumiwa wanatoka Kampuni nyingine kabisa - kampuni hiyo ya kitapeli ndiyo ilikuwa inatumia SIM cards za HaloTel kufanya udanganyifu.

Wanakulipa Tsh ngapi kuwatetea na kupindisha ukweli uliopo juu ya Utapeli wa HALOTEL? Kwahiyo zile taarifa zote za Media za Tanzania hadi na tukaonyeshwa na Video zao walivyokuwa wanapelekwa Mahakamani sisi Watanzania tulilishwa matango pori?
 
Watakuwa wamefundishwa wizi na waliowakuta ktk soko, mwanzoni walikuwa honest, sasa wamegeuka genge la wahuni.
 
Hamuulizi mawakala wenu jinsi ya kujiunga vifulushi,pia internet ya baadhi ya siyo automatic, so INA bidi uzijue access point, zake
Laini natumia kila siku sio kwamba ni mpya
ok let us say ni line mpya utashindwaje kujua kujiunga kifurushi wakati unapata confirmation inayokwambia umejiunga na kifurushi kadha wa kadha umepata mb kadha mpaka tarehe kadha

Na huwezi kupata kupata Internet bila APN mbona ni hata ya mwanzo kabisa kama simu ni mpya?
Hamuulizi mawakala wenu jinsi ya kujiunga vifulushi,pia internet ya baadhi ya siyo automatic, so INA bidi uzijue access point, zake
 
Back
Top Bottom