Halotel ndio mtandao dhaifu zaidi kwenye huduma ya Internet kwa sasa

Ndio vipo vyenye 4g, mimo na hio band 2600, sema asilimia kubwa sio lte advance, na kuikuta yenye lte advance bei inakua ndefu inaweza fika laki 3.

Kwa experience yangu flagship za zamani Unazipata kwa bei rahisi zaidi kuliko router kali, mfano Google pixel 2 ama Sony Xz1 Unazipata around $60 huko ughaibuni, hii Modem yake ni Gigabit lte, kwa speed tu ya 4g hakuna Router inayofikia. Pia unakuta ina bands zote Duniani Sababu ni flagship hivyo huna haja ya kusumbuka kichwa hata kama ni msafiri wa mara kwa mara.
mkuu hivi vismart vitochi vya voda unavizungumziaje? vina hizo specs ulizotaja?
 
Halotel ambao waliingia kwenye soko na kufanya mapinduzi kwa kutoa kasi kubwa ya Internet sambamba na bei nafuu kuliko watoa huduma wote waliowakuta, hatimaye wameshindwa kuendelea kutoa huduma hiyo kwa ufanisi.

Inawezekana mteja asiye makini akaendelea tu kusema Halotel wana bei nafuu za vifurushi vya Internet kulinganisha na wengine, lakini kwa usahihi si kweli. Unanunua kifurushi bei nafuu lakini hutokitumia mpaka muda wake unaisha sababu ikiwa mtandao wao kutofanya kazi kwa masaa mengi ya siku.

Maoni yangu:
Halotel muachane na ushindani wa bei pekee, ushindani sahihi ni ubora wa huduma. Ni bora muongeze bei za vifurushi huku mkiboresha huduma kiliko kuweka bei rahisi na huduma ikawa duni
Mi nafikir hii mitandao inategemea na eneo ulipo, kwa sababu kuna malalamiko mengine watumiaji wanalalamika lakini ukilinganisha na wew ambaye unatumia huo huoni shida.
 
Sidhani kama ni overload , hawa jamaa baada ya ile kesi ya kuingiza vifaaa kinyemela ni kama walitikisika
Wakati wanazindua mwaka 2015 , sehemu kubwa network yao ilikuwa inasoma 3g, siku hizi maeneo yale yale yaliyokuwa na 3g sasa yanasoma edge, nahisi wamepunguza baadhi ya transmitters za 3g.
Wafunge biashara TCRA wako wapi sis wanyonge tunateseka!
 
Network kila ikiwa ngumu ndio battery ya simu yako inakukufa, kama unataka kutunza sim yako tafuta mtandao wenye network safi
 
Network kila ikiwa ngumu ndio battery ya simu yako inakukufa, kama unataka kutunza sim yako tafuta mtandao wenye network safi
Sahihi kabisa mimi huw na experience nikisafiri. simu inabadilisha sana uwezo wa kukaa na chaji safarini, , sababu ya kutafuta network.
 
Haina band za 4G vipi wakati Voda inasoma 4G, Airtel 4G , Tigo 4G .. Halotel tu ndio haisomi

Infinix hot 10

Labda laini inashida
4g ni tofauti na 3g kila mtandao Una band yake, inawezekana ikashika 4g ya Voda ikakataa ya tigo.

Nimeangalia simu yako ina band 7 ya Halotel, badili line ama tafuta ya mtu ya 4g utest.
 
4g ni tofauti na 3g kila mtandao Una band yake, inawezekana ikashika 4g ya Voda ikakataa ya tigo.

Nimeangalia simu yako ina band 7 ya Halotel, badili line ama tafuta ya mtu ya 4g utest.
Ooh kumbe, sikua najua, shukrani

Ngoja ni test lain nyingine nione, ila pia kuna mtu kanishauri nibadili lain pia
 
Ooh kumbe, sikua najua, shukrani

Ngoja ni test lain nyingine nione, ila pia kuna mtu kanishauri nibadili lain pia
Ukitest ya rafiki ya Halotel ikikubali ina maana confirmed itakuwa ni tatizo LA line, utabadili ukiwa na Amani.
 
Halotel Wamechemka saana.
Maeneo mengi hamna Mtandao, Katikati ya Jiji la Mbeya eneo la Isyesye na Nanenane kwenda Uyole hakuna Mtandao kabisa.
Hata Kutuma Msg za Kawaida zinasumbua kweli.
Wameshindwa na hawafanyi Utafiti.

Mfano Vijijini Vodacom wako Vizuri kwa Upande wa Internet kuliko Mtandao wowote hapa Tanzania.
All the Way kutoka Mbeya Mpaka Unaingia Darslam Halotel humo Njiani huenda ikakamata 25 % wakati Vodacom ni zaidi ya 95% una access Mtandao.
Hawa Jamaa wanapaswa Kujirekebisha Vinginevyo watawafuata Airtel.
 
Back
Top Bottom