Halmashauri ya Wilaya ya Ngara (M) Kagera ifanyiwe Ukaguzi wa Ndani wa Dharura ili kudhibiti Upotevu wa Fedha za Umma Unaoonekana Kukithiri hivi sasa

Joined
Nov 15, 2019
Posts
49
Reaction score
128
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ni Miongoni mwa Halmashauri 8 zinazounda Mkoa wa Kagera ikiwa na Jumla ya Vitongoji 389, Vijiji 75, Mitaa 34, Kata 22 na Tarafa 4.

Mapema mwaka huu Halmashauri hii iliwasilisha Rasimu ya Mpango wa Maendeleo na Bajeti kwa Mwaka 2025/2026 huku wadau wengi wa maendeleo ya wilayani hapa wakiwa wamefanikiwa kuipitia vilivyo na kwa upana wake, na mimi nikiwa miongoni mwa wadau hao.

Katika Rasimu hiyo, Kipengele cha Mapitio ya Bajeti kwa Mwaka 2024/2025 iligundulika wazi KUKOSEKANA kwa uwiano kati ya hesabu ya kile kilichoandikwa katika matumizi ikilinganishwa na hali halisi ya kile kinachoonekana Mtaani (vijijini) kwenye UHALSIA.

Lakini pia, wadau tumekuja kubaini kuwa baadhi ya matumizi ya fedha ndani ya Halmashauri zetu huwa hawazingatii thamani ya fedha yaani Value for Money kiasi cha kuweka uwiano kati ya Mradi ulioandikwa na gharama zake na kulinganisha na thamani ya Mradi.

Tumejikuta kwenye Halmashauri zetu tukiwa na Ripoti za Bajeti za Kupikwa na walengwa ili kuwavutia serikali kuu na kule wanapopeleka ripoti hizo na siyo uhalsia wa kile kinachofanyika. Fedha za umma zimekuwa zikitumiwa hovyo kiasi cha kutotambua thamani ya walipa kodi katika Halmashauri husika.

NINATAMBUA kuwa, kwa Mujibu wa Kifungu cha 48(1) cha Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Namba. 9 ya Mwaka 1982 Sura ya 290 Toleo la Mwaka 2019 ya sheria za Tanzania, imeelekezwa kuwa Hesabu za kila Halmashauri ya Wilaya na za Mamlaka za Miji zitakaguliwa na Mkaguzi wa ndani aliyeajiriwa na mamlaka husika.

Kwa kulitambua hilo na kwa kuthamini nguvu waliyonayo Wakaguzi wa Ndani pamoja na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, ninawaomba waweze kuweka kambi Halmashauri ya Ngara ili waweze kuikagua kabla Baraza la Madiwani halijavunjwa ili kuweza kubaini dosari nyingi ambazo zingine sijaweza kuziainisha hapa ambazo huenda pengine zikaja kuwa sehemu ya matokeo ya Ukaguzi wao.

Zingatia: Kuna Viongozi na Watumishi wa Halmashauri wamejilimbikizia mali, kuna decorations za majengo na miradi inayoripotiwa kwamba imejengwa wakati wamepaka rangi, kuna shida kubwa na nyingi sana Ngara!.
 
Unaposhare document ya serikali mtandaoni kama hiv, umeisoma Data Protection Act kweli? Nia yako ya kumchafua mtu inaweza kukuletea shida, nenda kwa step
 
Hakuna Document ambayo iko attached hapo. Hata iliyokuwa attached by fault nayo nimeiondoa pia. Pia The Personal Data Protection Act CAP 44 Revised Edition of 2023 niko nayo makini kuliko kawaida. Hakuna anayeweza kupublish contents kama hizi zenye maslahi ya kijamii bila maandalizi
 
Hali hiyo unayoiona Ngara iko Halmashauri karibu zote Nchini.

Kila sehemu watu wanakula kwa urefu wa kamba zao.

Hayo uliyoyabainisha yanafahamika ila hakuna wa kumfunga Paka kengele, zaidi zaidi wataanza kukuundia zengwe, fitina, ulozi na kila aina ya uhafidhina maana umegusa mikate yao.
 
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ni Miongoni mwa Halmashauri 8 zinazounda Mkoa wa Kagera ikiwa na Jumla ya Vitongoji 389, Vijiji 75, Mitaa 34, Kata 22 na Tarafa 4.

Mapema mwaka huu Halmashauri hii iliwasilisha Rasimu ya Mpango wa Maendeleo na Bajeti kwa Mwaka 2025/2026 huku wadau wengi wa maendeleo ya wilayani hapa wakiwa wamefanikiwa kuipitia vilivyo na kwa upana wake, na mimi nikiwa miongoni mwa wadau hao.

Katika Rasimu hiyo, Kipengele cha Mapitio ya Bajeti kwa Mwaka 2024/2025 iligundulika wazi KUKOSEKANA kwa uwiano kati ya hesabu ya kile kilichoandikwa katika matumizi ikilinganishwa na hali halisi ya kile kinachoonekana Mtaani (vijijini) kwenye UHALSIA.

Lakini pia, wadau tumekuja kubaini kuwa baadhi ya matumizi ya fedha ndani ya Halmashauri zetu huwa hawazingatii thamani ya fedha yaani Value for Money kiasi cha kuweka uwiano kati ya Mradi ulioandikwa na gharama zake na kulinganisha na thamani ya Mradi.

Tumejikuta kwenye Halmashauri zetu tukiwa na Ripoti za Bajeti za Kupikwa na walengwa ili kuwavutia serikali kuu na kule wanapopeleka ripoti hizo na siyo uhalsia wa kile kinachofanyika. Fedha za umma zimekuwa zikitumiwa hovyo kiasi cha kutotambua thamani ya walipa kodi katika Halmashauri husika.

NINATAMBUA kuwa, kwa Mujibu wa Kifungu cha 48(1) cha Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Namba. 9 ya Mwaka 1982 Sura ya 290 Toleo la Mwaka 2019 ya sheria za Tanzania, imeelekezwa kuwa Hesabu za kila Halmashauri ya Wilaya na za Mamlaka za Miji zitakaguliwa na Mkaguzi wa ndani aliyeajiriwa na mamlaka husika.

Kwa kulitambua hilo na kwa kuthamini nguvu waliyonayo Wakaguzi wa Ndani pamoja na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, ninawaomba waweze kuweka kambi Halmashauri ya Ngara ili waweze kuikagua kabla Baraza la Madiwani halijavunjwa ili kuweza kubaini dosari nyingi ambazo zingine sijaweza kuziainisha hapa ambazo huenda pengine zikaja kuwa sehemu ya matokeo ya Ukaguzi wao.

Zingatia: Kuna Viongozi na Watumishi wa Halmashauri wamejilimbikizia mali, kuna decorations za majengo na miradi inayoripotiwa kwamba imejengwa wakati wamepaka rangi, kuna shida kubwa na nyingi sana Ngara!.
Tatizo la kuchagua madiwani wasiojitambua🤔!. Bila kuwa na madiwani mahili Mkurugenzi ambaye ni wakuja tuu atawaburuza na mwisho wa siku yeye atarudi kwao alikotoka, hata akifa atarudishwa kwao hana machungu na nyie. Ila nyie madiwani ndiyo wazawa wa hapo mmezaliwa hapo, mmekulia hapo, na mtazikwa hapo, sasa kupanga ni kuchagua.
 
Back
Top Bottom