Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,444
- 7,808
Leo waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu, Kazi, Ajira na wenye ulemavu akiwa Bungeni amekanusha mifuko ya hifadhi ya Jamii kutokuwa himilivu. Alipohojiwa na Esther Bulaya juu ya ripoti ya CAG kusema vinginevyo, ameendelea kushikilia msimamo wake kwa madai ripoti hiyo inaishia June 2021.
Waziri Ndalichako: Mheshimiwa mwenyekiti, jambo jingine ambalo wananchi wanalizungumzia ni uhimilivu wa mifuko, naomba nilihakikishie bunge lako tukufu kwamba mifuko hii bado ni himilivu, bado itaendelea kulipa mafao kwa wastaafu.
TAARIFA
Esther Bulaya: Napenda nimpe taarifa mheshimiwa waziri, taarifa ya mkaguzi mkuu na mdhibiti wa Serikali amesema mifuko ina hali mbaya, sio himilivu na ipo kinyume na utaratibu wa ukwasi wa asilimia 40, mlipolipa trilioni 2 walau imefika asilimia 30.
PSSSF kwa miaka ya karibuni, mapato yake ya michango ni madogo kuliko mahitaji ya wazee wastaafu wanaotakiwa kulipwa, iko himilivu wapi?
Mwenyekiti: Mheshimiwa Profesa Ndalichako unapokea taarifa?
Prof. Ndalichako: Mimi siipokei hiyo taarifa kwasababu taarifa ya CAG ni ya mpaka Juni 2021.
Bulaya anaongea
Mwenyekiti: Nani amekuruhusu kuongea mheshimiwa Bulaya, hili ni Bunge.