Halima Mdee aibuka shujaa Kawe

Halima Mdee aibuka shujaa Kawe

Mbunge wa Kawe-CHADEMA Halima Mdee amepongezwa na wananchi wa eneo la Mji Mpya Mzimuni kwa jitihada zake kubwa zilizopelekea kupatikana mradi wa maji eneo hilo.

Wakihojiwa na Clouds TV wananchi kadhaa wa eneo hilo wamesema kwamba wamekuwa wakipata shida ya maji kwa miaka mingi na maji waliyokuwa wanatumia ni ya chumvi tu.Wamesema hiyo ni kero ya miaka mingi ambayo wabunge wote waliopita walishindwa kutatua.

Hata hivyo wananchi hao wa vyama tofauti tofauti vya kisiasa wamesema alipokuja Halima Mdee na kusikiliza matatizo ya wananchi hao kwa muda mfupi ametafuta ufadhili ambao kwa kushirikiana na Manispaa eneo hilo limepatiwa mradi wa maji safi.

Wananchi hao wamewataka wabunge wengine kuiga mfano huo huku wakimwagia sifa kemkem mbunge huyo wa Kawe.

Source:Clouds TV Habari.
Aongeze nyama Kwenye mifupa aliyotupatia mtoa mada, Kama vile majina ya wafadhili, KIASI Cha Fedha kilichotokewa kwa ajili ya Mradi na idadi ya watu watakaonufaika na Mradi huo na unaanza lini na kukamilika lini.
 
wewe molemo si ndio mnashirikiana na slaa na mchumba wake slaa kuhakikisha mnaondoa uongozi wa kawe hasa ule unaomuunga kamanda mdee pamoja nakumchafua mitandaoni kwamba hafanyi kazi yoyote mmeona kawapiga chenga ya mwili ndo mnaanza kujifanya mnamsifia.
huo ni unafiki mkubwa sana .
mnadhani hamfahamiki?
iweje mjifiche kwenye shamba la maharage nakudhani hamuonekani?
hata kamanda wetu wa kawe mdee anaujua unafiki wako .
pole sanaaa.

Mtahangaika sana.....
 
Aongeze nyama Kwenye mifupa aliyotupatia mtoa mada, Kama vile majina ya wafadhili, KIASI Cha Fedha kilichotokewa kwa ajili ya Mradi na idadi ya watu watakaonufaika na Mradi huo na unaanza lini na kukamilika lini.

Mkuu niliripoti kama ilivyotolewa.
 
Hivi ni kweli slaaa hampendi mdee, mbona kazi hapo CDM

huwezi kuamini mkuu ila habari ndo hiyo.
na hii chuki haijaanza muda mrefu imeanza juzijuzi tu hapa baada ya mshumbusi kumuwekea slaa katelelo na kisha kumuomba amsaidie ili agombee kawe 2015.
visa anavyofanyiwa yule dada kwa mtu mwenye moyo mwepesi angeshakufa kwa pressure lakini yule dada ni jembe hatujawahi juta kumchagua na katu hatutojuta.
ana sifa kama za kamanda zitto.
 
Mwenyewe mdada namkubali sanaaa, mafisadi ccm waige mambo kama hayo siyo washindani kuzulumu rasilimali za waTz tu
 
hahahaaaa mtahangaika sana kawe lakini iron lady mdee atawatoa udenda mwisho wa siku.
ya vunjo yamekushinda ya kawe utayaweza weye?
slaa naye ya karatu yamemshinda saahizi hawataki hata kumsikia kama unabisha muulize mzee maasai mwenyekiti wa halmashauri ya karatu nini kilitokea baada ya maasai kumpa slaa kiwanja japo ajenge nyumba yakujisitiri yeye akalazimisha hati ya kiwanja iandikwe jina la mshumbusi.
hahahaaaa nimeamini ule mpango wenu wakumpindua na mbowe kugombea urais unaenda kwa kasi.
but jisogezeni sogezeni maana moto wa lekadutigiteeeeee hamtauweza .


Tatizo ni kuishi kwa hisia na umbeya, Mnampa sifa huyo Molemo ambazo sio zake hata kwani mnabatiza watu majina ambayo sio yao..........ndio shida ya utoto na kuwa na akili za samaki.......
 
hahahaaaaaaaa!
usilolijua litakusumbua.
huyo molemo na tabia zake anafahamika kama njaa mkuu.
hapa hamna cha mtoto wala samaki molemo na genge lake lote watuachie kamanda wetu mdee sisi ndo wapiga kura wake hatumuhitaji huyo mchumba wa slaa wala diwani wa kunduchi maana naye kashinda huo udiwani kwa influence ya mdee.
tunajua mbinu zenu siku ile mlikodi wahuni mkawapa pesa waandamane hadi makao makuu eti ni wananchi wa kawe wanapeleka malalamiko yao kwa slaa kwamba hawamtaki mbunge.
mligongaje mwamba?
nadhani mnakumbuka.
zitto the next prezidaa mdee the next minister of laws and constitution.
 
Huu ndiyo mfano wa kuigwa na wabunge wengine kwamba kero za wananchi ni lazima zitafutiwe ufumbuzi. Mbunge lazima awe na mikakati mbalimbali yenye lengo la kutatua kero za wananchi. Bravo Mhe. Mdee.
 
maadui wa kamanda mdee ndani ya chadema
slaa
mshumbusi
janeth rite
molemo.
si kweli kuhusu molemo na dr slaa labda yule waitara wa trm ndio namsikia sikia akimpondea saana halima na hata kumuita majina ya ajabu
 
si kweli kuhusu molemo na dr slaa labda yule waitara wa trm ndio namsikia sikia akimpondea saana halima na hata kumuita majina ya ajabu

mkuu habari ndo hiyo sisi ndio wanakawe tunajua michezo yote ya slaa na genge lake.
huyo waitara unayemsema yeye ni bendera fata upepo tu si kwamba ana bifu na halima.
labda umechanganya waitara ana bifu na ester matiko mbunge wa viti maalumu tarime kutokana na kwamba kapata viti maalumu kwa mgongo wa kura za waitara lakini sasa hivi kamgeuka ameungana na heche ambaye ni hasimu mkubwa wa waitara tarime maana wanagombania lile jimbo.
hao ndo core characters wenye bifu na mdee!
 
Prof Tibaijuka aungukuwa anafatilia matukio haya na kuingia JF angekuwa na wivu make pamoja na uprof wake ubunifu zero. Mito inakauka kwa sababu ya uatataji miti hovyo, mnyauko, vifo vya watoto wadogo na wakina mama kwa sababu ya miundombinu mibovu. Hivi kati ya mdee na Tibaijuka nani anapaswa kuwa mbunifu mpaka kuandika proposols za kutafuta rasilimali nje ya kutegemea wafadhili kwa ajili ya kutatuta matatizo ya wananchi. Muleba tafakari chukua hatua.
 
mkuu habari ndo hiyo sisi ndio wanakawe tunajua michezo yote ya slaa na genge lake.
huyo waitara unayemsema yeye ni bendera fata upepo tu si kwamba ana bifu na halima.
labda umechanganya waitara ana bifu na ester matiko mbunge wa viti maalumu tarime kutokana na kwamba kapata viti maalumu kwa mgongo wa kura za waitara lakini sasa hivi kamgeuka ameungana na heche ambaye ni hasimu mkubwa wa waitara tarime maana wanagombania lile jimbo.
hao ndo core characters wenye bifu na mdee!
kaka huyu waitara nilikuwa namsikiaga tu mimi nimebahatika kukaa naye kanipa lift na gari aina ya ford kutoka vingunguti kuja hapa kinondoni maneno yake dhidi ya halima yalikuwa machafu saana na ikafika sehemu nikamuasa sana awe anakuwa na mipaka sana ingawa hata huyo ester naye alimtaja taja lakini hapa kuhusu mdee anaongea sana wallah huyu alikuwa threat pia
 
Laiti mngejua. Mdee ameharibu sana jimboni kwake na sasa hakubaliki tena kama alivyokuwa anakubalika awali. Kitendo cha Clouds kumrusha hewani ni cha kibiashara zaidi, mbunge huyo ametoa hela clouds ili kituo hicho kijaribu kufunika madhambi yake baada ya kuharibu mambo jimboni. Inasemekana Mdee hana mahusiano mazuri na viongozi wa jimbo kata na matawi
 
Wewe dada nilikupenda sana kwa kasi yako ya kufanya kazi ulipo kwenda bungeni tu naona umebadilika sana kuna bomba la maji uloweka wewe mpaka leo bado halina maji sasa sijui kulikoni huu ni mwaka wa 5 unawambia nini wananchi wako
 
Hilo bomba la maji liko wapi? je umemtafuta diwani wa kata yako na kumwuliza? Fuata taratibu kabla hujamlaumu Mbunge. Si kila jambo anafanya Mbunge; kuna wajumbe wa mtaa, wenyeviti wa mtaa, watendaji wa kata na hatimaye unafika kwa diwani. Inaitwa Chain of Command. Wewe unataka kuwaruka wote hawa, ufike kwa Mbunge, ili yeye sasa aanze kufuatilia huku chini na kuwauliza wenzake: Kulikoni?

Si kwenye jimbo la Kawe pekee. Majimbo YOTE nchini watu hawataki "shida" ya kuwaona watendaji waliopo ngazi za chini. Huku ndiko madudu yote yanakamuliwa, yakimfikia Mbunge, kazi yake inakuwa bora zaidi. Watu wanayaona matatizo, wanayafumbia macho: Si kazi yangu. Ni ya Mbunge, au ya Diwani.

Huyo Mbunge na Diwani ni binadam kama wewe. Ana kazi zake, ana familia, hatarajii kuishi kwa huo Ubunge au Udiwani pekee. Ana wasaidizi. Diwani hushirikiana na madiwani wenzake na watendaji wa ngazi za chini. Hatua ya mwisho kabla hoja haijaenda Bungeni au Wizarani ni kwa Mbunge.

Au umetumwa wewe umkomoe Halima Mdee?
John Mnyika unalizungumziaje hili?
 
Back
Top Bottom