Halima Mdee ahamishiwa central police baada ya masaa 72

Halima Mdee ahamishiwa central police baada ya masaa 72

Not every human being fit the real definition of human being,and the number of human beings today,if any,that number itself is not real-Binadamu leo hii ni wachache sana na huenda hakuna kabisa....
Acha kututafsiria porojo zako. Kiingereza chenyewe kobovuu.
 
Wanamjenga na kumuimarisha kisiasa hongera JPM kwa kuujenga upinzani bila ya kukusudia
Hauko 'serious' kabisa kama unashabikia midomo inayotoa maneno kwa spidi wakati wenye midomo hawana breki. Hivi hao ndo wanajengwa kisiasa, unavyotaka tuamini, au wanaongezewa spidi ya kujibomoa!
 
Not every human being fit the real definition of human being,and the number of human beings today,if any,that number itself is not real-Binadamu leo hii ni wachache sana na huenda hakuna kabisa.

Mtu unaridhika kulala ndani na familia yako huku mwenzako umemuweka jela kwasababu zisizoeleweka na wala nafsi haikusuti alafu kila siku uko kanisani /msikitini eti unaomba Mungu/unaomba uombewe!

Soon tutaacha hata kuzikana kutokana na aina hii ya sisiasa!

Mwenyemuzi Mungu ingilia kati.
Humanity is zerooooo kabsaaaa nashangaa sn watu wanavyomshambulia utafikiri labda kaua ,kwani magufuli karopoka Mara ngapi tena maneno ya kukashifu watu na tena ambayo huwezi kuyaongea kwa watu ambao wako kwa wakati mgumu,Leo hii mtu anajaribu kujitetea kwa namna anavyoona mnasema amemkashifu, this is too much ,si mseme tu tz theres no human right tukaelewa ,,,,,ila mungu atawalipiza mkumbe kuna watu wanfunga na kuomba kwa kuwaombea watu kama halima mdee,....tumewachokachoka
 
akitoka huko atakuwa mwanamke anaejiheshimu..na anayeheshimu jamhuri.

Rais wa jamhuri sio raihisi rahisi kama wanavyodhani..huwezi kumdhalilisha Mheshimiwa kwa kumkosea adabu..

anyooshwe tu hamna namna..
Nyerere angekuwa na akili kama zako mpaka sasa tungekuwa tunatawaliwa
 
Pole dada Halima! Yana mwisho haya, kama sio kipindi chetu basi watoto na wajukuu wetu wataushuhudia huo mwisho! Mungu aendelee kukupigania na kukulinda kwa yote yanayokusibu! Hata wakati wa kupigania Uhuru kina Nyerere walionekana vioja na baadhi ya watu lakini walifanikisha lengo lao! Umejitolea kuwasemea watanzania wengi ambao hawana ujasiri huo! Hata wanaokukebehi mioyoni mwao ukweli wanaujua ila ndio hivyo tena kujipendekeza, njaa na ujinga vimewajaa!

Hivi ni tusi gani alilotukana Halima au ni kivipi amehatarisha usalama wa nchi? Jamani tupendane wanadamu hivi vyeo ni mambo ya mpito tu!
 
Mwalimu Nyerere alisema "Kwa katiba hii ni rahisi kwa kiongozi kuwa dikteta".
Awamu hii baada ya kuunganisha wananchi kuwa kitu kimoja kwenye mapambano ya kubadilisha mfumo ndio kwanza tunajenga ufa mkubwa baina ya Watanzania wenye itikadi tofauti. Tukubali kutofautiana kimawazo na kukosoana ili nchi isonge bila vinyongo na sononi.
 
Ukimsema mtu mjinga unahatarisha usalama wa nchi? Basi hii ni ajabu sana
Halima Mdee kutamka kuwa Rais anachukulia kauli zake kuwa sheria mmemuhukumu kuwa kauli yake hiyo ni kuhatarisha usalama wa nchi.....


Na wale ambao wanataka kuigeuza nchi yetu Burundi kwa kuandamana na kubeba mabango na kupendekeza Katiba ya nchi yetu ibadilishwe ili Magu badala ya kutawala vipindi viwili vya miaka mitano, mitano wale hawatarishi usalama wa Taifa, kwa kuwa mapendekezo yao yanamfurahisha Mkulu?
 
akitoka huko atakuwa mwanamke anaejiheshimu..na anayeheshimu jamhuri.

Rais wa jamhuri sio raihisi rahisi kama wanavyodhani..huwezi kumdhalilisha Mheshimiwa kwa kumkosea adabu..

anyooshwe tu hamna namna..
Tumemwonya huku mtsndaoni,hasikii kwa kujaa kiburi.
Pengine dunia sasa itamfunza.
 
Hivi kwenye ile hotuba ya Mh. Mdee hakukuwa na tusi au lugha isiyokuwa ya staha(Kama angekuwa bungeni) kweli?
 
Nadhani sasa RC nae kaongeza ya kwake 48. Waendesha mashtaka watakuwa wameambiwa waipitie upya tena na tena ile speech ya Halima mdee na waje na makosa yasiyopungua 6 ili Jumatatu au Jumanne wampandishe kizimbani kwa Pilato. Kwa jinsi mambo yanavyokwenda, usikute wakaja na makosa kama haya:

1) Kupingana na kauli ya Rais hadharani
2) Kuwateteta ''makahaba'' walioamua kupata mimba kwa hiari na raha zao na sasa eti wanatetewa warudi shule
3) Kushawishi Umma kwamba Rais ni incompetent na alipaswa kupewa semina elekezi kabla ya/baada ya kuokota dodo kwenye jangwa la Sahara
4) Kutaka kuuaminisha Umma kwamba Rais wetu wa wanyonge ni chizi na anaweza kufikiria siku moja kuwaambia wananchi wake wanyonge watoke vifua wazi au watembe peku
5) Kumdhalilisha Rais kwamba hana huruma kwa raia wake wa kike waliompigia kura na kwamba ati ni mfuasi makini wa mfumo dume
6) Kuinstigate wabunge wafikirie kumfunga brake one of these days ili asideal na majizi. Hii ni sawa na kuhujumu uchumi, na hapa atapaswa kurudi ndani maana kosa la uhujumu uchumi halina dhamana (kama huamini, kamuulize Manji)
 
Ni kweli mkuu. Baadhi ya maRais wa Afrika wanajua kwamba chochote wanachokisema hata wakiwa wamelewa, kinakuwa law automatically. Ukipingana na kauli ya Rais, unakuwa mhaini na unaonekana kama unatishia amani ya Nchi kwa kuinstigate watu wamdharau Rais. ''Rais wa Wanyonge'' hapaswi kupingwa ati...

Kuna tofauti ya Kumpinga Rais na kumtukana Rais!
Kwanini kila Siku wasumbuliwe hao hao Wachache Mbona Wapinzani wengine hawasumbuliwi japo wanampinga Rais

, kwanini hakamatwi Mchungaji Msigwa japo yeye ni mpingaji Mkubwa wa Rais Tena kwa hoja kuliko hao Watukanaji?
 
Kama baada ya miaka 50 na shee serikali ya Ccm ilishindwa kutengeneza miundombinu ya Kawe Mdee hawezi kuwa mbuzi wa kafara.
Na kwa usawa huu wa bajeti kutokamilika kwa walau 40% fedha za maendeleo tutegemee janga la kitaifa sio Kawe tu.
Aendelee kukaa huko selo, barabara tutatengeneza wenyewe.
 
Not every human being fit the real definition of human being,and the number of human beings today,if any,that number itself is not real-Binadamu leo hii ni wachache sana na huenda hakuna kabisa.

Mtu unaridhika kulala ndani na familia yako huku mwenzako umemuweka jela kwasababu zisizoeleweka na wala nafsi haikusuti alafu kila siku uko kanisani /msikitini eti unaomba Mungu/unaomba uombewe!

Soon tutaacha hata kuzikana kutokana na aina hii ya sisiasa!

Mwenyemuzi Mungu ingilia kati.
Acheni ushabiki kwani aliyemtia ndani Halima ni JPM?
 
Naomba mnielewa. Mdee hawezi kutoka mpaka akae miezi 4~6ndani
 
Back
Top Bottom