Hali ya wakulima wa Vanilla inatisha Kyerwa, Karagwe na Bukoba Vijijini

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
Hali ya wakulima wa Vanilla inatisha Kyerwa, Karagwe na Bukoba vijijini leo nimepata taarifa kuwa wakulima wameanza kung,oa zao hili kutokana na ukosefu wa wanunuzi nimeambiwa mwaka jana waliuza kilo moja kwa Tsh.25, 000/ mwaka huu hakuna wanunuzi kabisa ata aliyejitokeza anataka kununua kilo moja kwa Tsh.3, 000/ (elfu tatu) hii ni dharau kwa wakulima, hii ni dhihaka kwa wakulima serkali iko kimya ata wabunge wa Kagera wote wako kimya, Mkuu wa mkoa yuko kimya, wakuu wa Wilaya wako kimya uku wakulima wakishuhudia mazao yao yakiendelea kunyaukia ndani baada ya kuyavuna.

Tunaitaka serkali iingilie kati ili kuondoa hofu kwa wakulima na kuwatia moyo.

Tunawezaje kuinasua Kagera kwenye mkia wa uchumi ikiwa hatuwezi kuwasaport wakulima kwa kuwatafutia masoko? Kwani Kagera tuliwakosea nini? Kwanini mkoa unabaguliwa?

Ruhusu Waganda na Wakenya waje wanunue Vanilla zetu kwa bei ya soko bila masharti.
Kahawa iko hoi, Vanilla imekosa soko kabisa mnataka wakulima wa Kagera waende wapi?

Basi tuachie tutafute nchi ya kujiunga nayo.@hussenbashe View attachment 2683417
image_9c03b3b7-6237-4986-895a-43835ebb778a.jpg
 
Tatizo serikali hii ni dhaifu mno.kila siku matapeli yanajitanganga kwenye luninga kuhamasisha kilimo cha vanila na kuwadanganga wakulima watauza kwa milioni kwa kilo lakini wakiivisha hakuna mnunuzi na serikali iko kimya.bora ulime mazao ya chakula kuliko huo upuuzi wa kilimo cha vanila
 
Back
Top Bottom