Hali ya usalama nchini inazidi kuwa tete

Hali ya usalama nchini inazidi kuwa tete

Kilichokuwa kiwe uchaguzi mkuu Tanzania kwa mujibu wa katiba yake, kimepita na yaliyotokea sote tunayafahamu!

Bado taifa halijatulia, bado fukuto lipo, la dhuluma, la maumivu, la ukatili mkubwa uliitokea nknk
Hofu kwa upande wa pili ni kubwa zaidi.. Nadhani intelijensia inawapenyezea hali halisi... Ni lazima lifanyike jambo la maamuzi magumu sana kwa upande wao ili kuweza kutamatisha hii hali

Kamatakamata na utekaji unaoendelea havina afya kwa taifa bali vinazidisha uchungu na maumivu kwa yaliyokwisha tokea

Haya mambo yanazidisha usugu na kuzalisha uasi... Haitakaa itokee watu wanyamaze mazima kama matakwa yao ya kikatiba hayatatekelezwa

Kiasili binadamu amezaliwa kuongea, ni vigumu sana kumziba mdomo asiongee! Kwa kufanya hivyo unazalisha kitu kingine hatari zaidi

Wakosoaji waachiwe waongee ndio njia pekee iliyobaki ya kuwapunguzia maumivu na fukuto mioyoni mwao! Haitakaa itokee kuwanyamazisha wote kwa kuwateka, kuwapoteza, kuwatesa, kuwabambikia kesi kubwa zisizo na dhamana ama kuwaweka kizuizini kwa kesi ghushi

Kufanya hivyo hakuleti suluhu bali kunaongeza tatizo ambalo siku likikomaa tufani yake itakuwa na mshindo mkubwa sana!

Ukiwabufaza waliopo kwa mbinu mbalimbali kuna kundi lingine kubwa nyuma yao litaibuka. Ambalo ni
Kubwa zaidi
Baya zaidi

Kwaweli tumechoka kuzika, tumechoka kupoteza ndugu jamaa na marafiki,
Tumechoka kuhudhuria kesi za michongo
Kutibu majeraha na majeruhi wa ukatili vituo vya police
Wahanga ni wengi sana na kila mhanga ana chain ya watu wasiopungua 20! Mnadhani tunalipeleka wapi taifa

Taifa linaingia kwenye mdororo mkubwa wa kiuchumi.. Madhara yake yataonekana mwakani.. Badala ya kuwekeza kwenye umoja wa kitaifa ili nguvu kazi iliyopo itumike kwenye uzalishaji.. Tumewekeza kwa machawa na kutaka kufubaza nguvu kazi hiyo! Je mnadhani tutafika?

Tunatumia muda mwingi na rasilimali kuwinda watu

Tunatumia muda mwingi na rasilimali kuwateka

Tunatumia muda mwingi kuwatesa na kuwadhalilidha

Tunawaumiza kwa kuwasababidshia majeraha na ulemavu

Nao wanatumia muda mwingi kujitibu, kujiuguza na kuhudhuria kesi za mchongo.. Huu ni uhujumu uchumi
Tunazalisha yatima wajane na wagame bila kujua.. Familia zinasambaratika.. Breadwinners wengi katika familia ndio hao walioko kwenye madhila ya kila aina!

Je wenye hekima na uthubutu wameisha Tanganyika!?View attachment 3518334
Huyu sidhani kama ni mtanzania uraia wake uchunguzwe
 
Inategemea na hekima yao

Hivi hao wanaokamatwa huwa wanakamatwa bila sababu ?

Kwanini hamuwakemei kipindi ambacho wanafanya makosa ? Uadilifu wenu uko wapi ?

Mnapowakosoa viongozi wa juu katika yale wanayo yakosea, basi wakosoeni na wale ambao wanawakosea hao viongozi huu ndio uadilifu na utimamu wa akili.

Sasa wanapowatukana viongozi au kuchochea uvunjifu wa amani mnakaa kimya lakini wakipewa stahiki zao mnakuja kulalama. Akili zenu mnazitumia kwenye nini ?

Wajawema walio pita walikuwa wanajifunza kwanza adabu kabla ya Elimu, au wanasoma muda mwingi kuhusu adabu na Elimu muda kidogo. Wafunzeni vijana adabu, wafunzeni wanaharakati adabu Bali wafunzeni baadhi ya viongozi wa dini adabu.

Kama hujui maana ya neno ADABU uniambie nikueleweshe, na ujue nina maanisha nini.
 
Ni kweli kabisa huyo sio mtanzania huyo ni raia halali wa Tanganyika
Huwa nawahurumia sana na harakati zenu mfu hizo,, lakini ujue tu kuwa
Kazi na utu tunasonga mbele na Dr Samia Suluhu Hassan 🇹🇿
 
Naomba nitoe rai
Machawa wote watakaokuja na mapambio kisha kuwapondq.. Please nawasihi msiwajibu chochote..wakaushieni kabisa maana wako kwenye project maalum ya msasa na dodoki
Hao ni kuwatazama kama kinyesi bila kuwajibu ndio dawa yao maana wanakuja kwa lengo la kutafuta attention. Mtu mwenye akili timamu hawezi comment ufala wanaoandika wao machoko hawa.
 
CCM wametengeneza Samuya ambaye amekuja kuwa hatari na katili kuliko mnyama wowote wa porini, mbaya zaidi hawana udhibiti naye.
 
Hao ni kuwatazama kama kinyesi bila kuwajibu ndio dawa yao maana wanakuja kwa lengo la kutafuta attention. Mtu mwenye akili timamu hawezi comment ufala wanaoandika wao machoko hawa.
Sawa sawa na sometimes ikibidi basi ni kuwatumia picha kaka hii
6c530119-7b29-4433-81c7-ea8b120b9342.jpeg
 
uzuri ni matishio madogomadogo yanayotolewa mitandaoni na wanaojita wanaharakati ambao kimsingi huwawezi wakuta kwenye jamii ambazo wazalendo walio wengi wanaendelea na majukumu yao ya kila siku
Sawa mkuu awamu yenu hii furahini tu!
 
Vikosi vilitumia nguvu kubwa kwa kipimo kipi, unamuona Simba unapelela kichwa unategemea atakubusu. Tumepewa akili ili zitusaidie kupambanua mambo, siyo kuongeza idadi ya watu wapumbavu duniani humu.
 
Vikosi vilitumia nguvu kubwa kwa kipimo kipi, unamuona Simba unapelela kichwa unategemea atakubusu. Tumepewa akili ili zitusaidie kupambanua mambo, siyo kuongeza idadi ya watu wapumbavu duniani humu.
Umepewa akili kisoda! Namna ya kuzuia maandamano inajulikana ..
Kuna risasi za mpira, maji washa,mabomu ya machozi..
Au kama vipi weka sheria hapa hata ya hapahapa kwetu( nchi yenye uduwanzi wa kutosha) ..unasema tumepewa akili ila kiukweli wewe hujapewa shingo yako imebeba jaba tupu!
 
Umepewa akili kisoda! Namna ya kuzuia maandamano inajulikana ..
Kuna risasi za mpira, maji washa,mabomu ya machozi..
Au kama vipi weka sheria hapa hata ya hapahapa kwetu( nchi yenye uduwanzi wa kutosha) ..unasema tumepewa akili ila kiukweli wewe hujapewa shingo yako imebeba jaba tupu!
unasema tumepewa akili ila kiukweli wewe hujapewa shingo yako imebeba jaba tupu!😀😀😀
 
Back
Top Bottom