Hali ya usalama nchini inazidi kuwa tete

Hali ya usalama nchini inazidi kuwa tete

Acheni maneno ya uzushi ,uongo, uchonganishi na fitina. Najua mnaumia sanaa baada ya maombi yenu mabaya na nia zenu ovu kwa Taifa letu kushindwa vibaya sana. Najua mlikuwa mnatamani na Kuwa na kiu kubwa sana ya kutaka kuona machafuko yakitokea hapa Nchini na Amani na usalama vikitoweka kama ukungu.

Lakini baada ya kushindwa na watanzania kuwashitukieni na kugoma kuendelea kuwaungeni mkono mmebakia na maumivu sana. Mnaumia na kuchanganya kabisa mnapoona watanzania wakiendelea kuwa wamoja,kuiunga mkono serikali na Rais wetu Mpendwa.

Mnateseka sana mioyo yenu na kujaribu kuendelea kuleta vijimaneno vya uzushi ,uongo na uchonganishi kila uchao. Hata hivyo hamtafanikiwa hata kidogo.mtaendelea kushindwa vibaya sana. Tena kama wewe ulipiga sana malamli yako . Sasa aibu imekushika na unaanza kuja kujibaraguza hapa ukifikiri wote ni wajinga kama wewe.
Mzee wa kububujikwa na machozi hali sio nzuri, kama ni wale utajua kama ni sisi hutajua.
 
Walioshiriki wote kwenye zile vurugu, ni suala la muda tu, kila mtu kwa wakati wake atafikiwa, salama yako uwe umetangulia mbele ya haki. Tulipokuwa tunawaasa kuhusu kutunza amani tuliitwa majina ya kila aina na kutukanwa matusi yote. Sasa ni wakati wa kila mtu abebe mzigo wake. Umekaa Tanzania unajazwa ujinga na mtu ambaye yuko nje ya nchi. Ni muda wa kujifunza in a hard way.
 
Huyu mwamba wamuachie tu wakimdhuru itakuwa mbaya sana.
Hakuna ubaya wowote unaweza tokea.

Hadi kitendo hicho cha kuteka kinafanyika na hakuna wa kutoa pua au hamsha hamsha toka Polepole, Buyobe nk, leo ndiyo uje utoe mguu mmmh laahulaa lakwata.

Not today!.
 
Kilichokuwa kiwe uchaguzi mkuu Tanzania kwa mujibu wa katiba yake, kimepita na yaliyotokea sote tunayafahamu!

Bado taifa halijatulia, bado fukuto lipo, la dhuluma, la maumivu, la ukatili mkubwa uliitokea nknk
Hofu kwa upande wa pili ni kubwa zaidi.. Nadhani intelijensia inawapenyezea hali halisi... Ni lazima lifanyike jambo la maamuzi magumu sana kwa upande wao ili kuweza kutamatisha hii hali

Kamatakamata na utekaji unaoendelea havina afya kwa taifa bali vinazidisha uchungu na maumivu kwa yaliyokwisha tokea

Haya mambo yanazidisha usugu na kuzalisha uasi... Haitakaa itokee watu wanyamaze mazima kama matakwa yao ya kikatiba hayatatekelezwa

Kiasili binadamu amezaliwa kuongea, ni vigumu sana kumziba mdomo asiongee! Kwa kufanya hivyo unazalisha kitu kingine hatari zaidi

Wakosoaji waachiwe waongee ndio njia pekee iliyobaki ya kuwapunguzia maumivu na fukuto mioyoni mwao! Haitakaa itokee kuwanyamazisha wote kwa kuwateka, kuwapoteza, kuwatesa, kuwabambikia kesi kubwa zisizo na dhamana ama kuwaweka kizuizini kwa kesi ghushi

Kufanya hivyo hakuleti suluhu bali kunaongeza tatizo ambalo siku likikomaa tufani yake itakuwa na mshindo mkubwa sana!

Ukiwabufaza waliopo kwa mbinu mbalimbali kuna kundi lingine kubwa nyuma yao litaibuka. Ambalo ni
Kubwa zaidi
Baya zaidi

Kwaweli tumechoka kuzika, tumechoka kupoteza ndugu jamaa na marafiki,
Tumechoka kuhudhuria kesi za michongo
Kutibu majeraha na majeruhi wa ukatili vituo vya police
Wahanga ni wengi sana na kila mhanga ana chain ya watu wasiopungua 20! Mnadhani tunalipeleka wapi taifa

Taifa linaingia kwenye mdororo mkubwa wa kiuchumi.. Madhara yake yataonekana mwakani.. Badala ya kuwekeza kwenye umoja wa kitaifa ili nguvu kazi iliyopo itumike kwenye uzalishaji.. Tumewekeza kwa machawa na kutaka kufubaza nguvu kazi hiyo! Je mnadhani tutafika?

Tunatumia muda mwingi na rasilimali kuwinda watu

Tunatumia muda mwingi na rasilimali kuwateka

Tunatumia muda mwingi kuwatesa na kuwadhalilidha

Tunawaumiza kwa kuwasababidshia majeraha na ulemavu

Nao wanatumia muda mwingi kujitibu, kujiuguza na kuhudhuria kesi za mchongo.. Huu ni uhujumu uchumi
Tunazalisha yatima wajane na wagame bila kujua.. Familia zinasambaratika.. Breadwinners wengi katika familia ndio hao walioko kwenye madhila ya kila aina!

Je wenye hekima na uthubutu wameisha Tanganyika!?View attachment 3518334
Mkuu umeonge na kushauri kwa uchungu sana, hii mbinu ya kuteka ,kuumiza watu kwa kesi za kijinga imefeli na mbaya zaidi inazidi lipasua Taifa.

Kweli kunahitajika mahamuzi magumu, kikundi cha watekaji wote kinatakiwa kunyazishwa haraka sana, naishia hapa
 
Lissu legeza kama umetushika pabaya
Upo gerezani unatunyima usingizi
Tukikutoa utatulaza na viatu
 
SAMWEL MGAYWA AMETEKWA MWATUROLE GEITA JANA JUMAMOSI 20.12.2025

Ficha utambulisho wangu Habari mtumishi naomba unisaidie kupost hii taarifa kuna mdogo wangu anaitwa SAMWEL MGAYWA anafanya kazi ya M-pesa hapa Geita mjini maeneo ya mwaturole jana walikuja watu wakajitambulisha kama police wakiwa na gari aina ya crown T 270 DCK wakamchukua wakaondoka naye tumetafta vituo vyote vya GEITA hayupo na inasemekana aliyemteka ni police yupo kituo cha police GEITA mjini

Naomba mtupazie sauti kwa Watanzania wenzetu
1766330276228.jpg
 
Back
Top Bottom