hali ya uchumi serikalini ni mbaya sana

na mtaani napo hali mbaya leo mfuko wa sukari kg50, sh 90000 bei ya jumla wakati jk anaingia madarakani ilikua sh 35 000

Kwa kweli maisha ni magumu sana, hivi sukari inapandaje bei iwapo miwa tunalima wenyewe, mashamba ni yetu ya asili si ya kukodi, umeme viwanda vya sukari hawauziwi na Tanesco (wanafua wenyewe), kuna justification gani ya kupandisha bei zaidi ya asilimia 200 in 5 years
 
sio kweli wala sitaki kuamini hivyo ,nenda TCRA UONE MABOSI WANAVYOENDA NJE NA KURUDI KAKA kARIAKOO.KAMA UNABISHA KAFANYE RESEARCH HALAFU UJE KUNIAMBIA
 
Aisee, Nawashukuruni sana wakuu..

OC = Other Charges!

Kwahiyo pesa ya ku-run Wizara zetu inatolewa on monthly basis and on merits?
 
OC maana yake "Other Charges" apart from mshahara huwa kuna hela inatoka Hazina inaitwa OC kwa ajili ya ku-run office. Kununulia karatasi, wino, kulipia internet, umeme,fax,simu, chai asubuhi, kulipa vibarua, kununua vifaa kama computer, printers, photocopier, posho za vikao,mafuta ya gari,vifaa vya usafi na mengine mengi kama hayo. Huwa kwa idara moja ya wizara ina matumizi ya bilioni 5-10 kwa mwaka.

if that is the case kuna haja ya mtu kuitwa mwanasiasa wa ccm kweli? wanaropoka majukwaani ovyo but nothing is being done wanaendesha nchi kama kiosk
 
nchi sasa ina ugonjwa wa kwashakoo (malnutrition) dawa ya huu ugonjwa kwa nchi ni hali nzuri ya uchumi..... je vyanzo vya nchi vya kipato vitaongezekaje wakati wananchi walipa kodi wanaumia na hata biashara na kazi hawawezi kufanya shauri ya ugumu wa maisha
 
Hali ya uchumi imekuwa mbaya sana katika idara zote za serikali kuliko hata ile iliyowahi kuripotiwa wakati wa uchaguzi. Chanzo cha kuaminika kutoka idara moja nyeti kinasema wamepelekewa waraka mzito wa kuwaamuru kurudisha hazina OC walizokuwa wamepelekewa kwa ajili ya matumizi ya kazi za serikali. Kwa ufupi hata OC zenyewe kuna wizara yenye idara kama kumi inapelekewa sh miliion kumi which means kila idara ipewe million moja kwa mwezi na bado wanataka pesa hizo zirudishwe kwa kisingizio kuna watu hawajalipwa mishahara kwa hiyo bora kazi zote zisimame mishahara ilipwe. hali inatisha especially kwa sukari kufikia 2000 kwa kilo. Tunaenda wapi?
My Take: huu ni mkakati maalumu wa kutafuta fungu la kuilipa dowans.
Amueni wananchi wakati ni huu wa kufanya kama Tunisia.

Mbona watumishi wa serikali wote wameisha lipwa mishahara ? ww unasemea mishahara ipi sasa ? Hizi ni habari za udaku na hapa si sehemu yake, na picha yako nzuri ulivyo pendeza nataka kuleta posa nikuoe
 
hebu achaneni na bubge hivi mmeshajiuliza hiyo semina ya wiki mbili kwa wabunge wote hao ya kumsikiliza fisadi hosea mtu ambaye wao wanatakiwa kum discipline inatumia zaidi ya milion 20 kwa siku bila kujumlisha mafuta yao na perdiem kulikua na umuhimu kweli? Kweli kuna seminar gani ndefu kiasi hicho ya one size fits them all, wabunge wapya na wa zamani wanafundishwa sane thing na same instructo, sawa na wanafunzi wa darasa la kwanza na la saba kusoma somo moja kwa mwalimu mmoja

Mkuu hapo ndio kuna tatizo kubwa sana hasahasa kwenye hizi serikali zetu za kifisadi. Watu wanahisi wakipata cheo serikalini maana yake ni kuzua safari na vikao visivyo na tija almradi wanapata hizo per diems, night out allowanses et cetera. Kwa kiasi kikubwa inachangiwa na mfumo wa serikali wenyewe ambapo mara nyingi hutoa mshahara kiduchu usiokidhi hata robo mwezi. Matokeo yake watu maofisini wanahaha kutafuta madili na hapo kazi hazifanyiki na unakutana na ma-four by four tu mikoani. What a shame. Tuige wenzetu hata kwa Mandela tu jamani tufanye kazi na tuache ujanja ujanja wa ki-RA.
 
Mbona watumishi wa serikali wote wameisha lipwa mishahara ? ww unasemea mishahara ipi sasa ? Hizi ni habari za udaku na hapa si sehemu yake, na picha yako nzuri ulivyo pendeza nataka kuleta posa nikuoe

Mkuu nadhani una utani na huyu mdada na mambo ya posa yametoka wapi?
watu hawazungumzii mishahara hapa mkuu,kama kazi hazifanyiki,miradi ya maendeleo hakuna na hata pesa za uendeshaji wa ofisi kila siku hamna ni aina gani ya kazi hiyo?hata hiyo mishahara itakwama kwa kuwa hakuna uzalishaji
usije kuwa ni mmoja wao unasubiri tarehe tu wakati hufanyi kazi
 
Mbona watumishi wa serikali wote wameisha lipwa mishahara ? ww unasemea mishahara ipi sasa ? Hizi ni habari za udaku na hapa si sehemu yake, na picha yako nzuri ulivyo pendeza nataka kuleta posa nikuoe

wewe toa mbwembwe hapa.una uhakika kwamba watu wamelipwa au unaropoka tu.
 
hapo umeongea, kama wanasema hawana pesa basi tunataka tusikie hata bunge limeahirishwa au wapunguziwe salary zao, hapo tutajua kama wako serious lasivyo tutaingia street like egypt
Hivi ule mkutano wa Bunge letu ''tukufu'' wa mwezi wa pili bado upo pale pale?

Nadhani wangeanza kwa kuuahirisha huo kwanza.

Wananchi wafanye kama Tunisia? - ile sumu tuliyopuliziwa ya ''amani, utulivu na mshikamno'' itachukua muda mrefu saaana ku-expire.
 
Mbona watumishi wa serikali wote wameisha lipwa mishahara ? ww unasemea mishahara ipi sasa ? Hizi ni habari za udaku na hapa si sehemu yake, na picha yako nzuri ulivyo pendeza nataka kuleta posa nikuoe

Kama unafanya kazi serikalini kweli tuambie: Posho za nyumba zimelipwa mwezi huu uliopita? Na si mwezi Januari tu hata miezi ijayo hazitalipwa maana kuna waraka umetolewa kuzifuta. Au nao ni udaku?
 
Hivi ule mkutano wa Bunge letu ''tukufu'' wa mwezi wa pili bado upo pale pale?

Nadhani wangeanza kwa kuuahirisha huo kwanza.

Wananchi wafanye kama Tunisia? - ile sumu tuliyopuliziwa ya ''amani, utulivu na mshikamno'' itachukua muda mrefu saaana ku-expire.

Mkuu kwenye maswala ya kupiga Kabobo (mambo ya bunge) una sema letu
ikija kwenye kudahi haki (Hapo nyekundu) unazungumzia wafanye, wakina nani wafanye? wewe utakuwa wapi wakati huo?
 
tukinukishe kama tunisia na egypt tu... watanzania bana sijui tunasubiri nini

mishahara hakuna na sukari ndio hiyo buku mbili kilo
 
Mbona watumishi wa serikali wote wameisha lipwa mishahara ? ww unasemea mishahara ipi sasa ? Hizi ni habari za udaku na hapa si sehemu yake, na picha yako nzuri ulivyo pendeza nataka kuleta posa nikuoe

kaka sio watumishi wote espscially kwenye ofisi za makatibu tawala wa mikoa,...mimi ni mmojawapo nimepokea mshahara leo tarehe moja feb..na oc zinazokuja ni aibu ikifika inafanyiwa proration(pro rata basis) idara yetu ya ukaguzi tulishawahi kupata 400,000/=...napiga CPA yangu nikimbie utumishi wa umma hakufai
 
It's get seriously horrible by a minunte! I prefer not to laugh nor cry but hold my breath and summon my strength to fight any form of evil till my last breath.

Mambo yamebadilika, tena bila kutarijiwa kwa upande wa watawala. Walidhani bzness as usual lakini ime-backfire ile mbaya. Swali nalojiuliza kwa muda huu ni kwa utaratibu/njia gani Jk na CCM waliweza kuifisadi Hazina namna hiyo. Kwa sababu kuna misaafu ya kuongoza mambo ya fedha Hazina na kuna watu wenye dhamana na uwezo (kitaaluma)...au ndio yale yale ya taaluma bila maadili?

Kuna siku, nadhani hiyo siku haiko mbali ambapo mbivu na mbichi zote zitajulikana na kila alichostahili mtenda basi atapewa iwe haki au adhabu.
 
Mafuta ya alizeti kabla ya uchaguzi yalikuwa TShs. 2000 kwa lita. Leo bei ni TShs. 3,500 kwa lita....Tanzania Tanzania Naipenda kwa moyo wote.....
 
Back
Top Bottom