Hali ya serikali ni tete? Mpaka sasa mishahara kitendawili

Hapa ndipo ninapopata taste ya ile wanayoilalamikia CDM...."CCM wasijifanye wasemaji wa vyama vingine!" Je, nikuletee mkataba wangu wa kazi ili uone kama sijaajiriwa?! salary yangu ya October 2011 nilipata November 03; na hii ni kwa wenzangu wote na hakuna kibarua hapo!
Unafanya kazi kwa wahindi unategemea mshahara tar 25, sahau ndugu. Hii serikali inaunga unga sana suala la mishahara na matumizi mengine. Kumbuka wachina kibao wajenga mabarabara ya magufuli wamesepa kurudi kwao kwa kutolipwa. Na trend inajulikana matumizi kuliko mapato.
 
Mkuu NasDaz unatetea nini? Hoja iliyopo ni kwamba Serikali inashindwa kugaramia matumizi yake ya kawaida Kama mishahara ya watumishi wake. Hii ni Hali ya hatari inayoonyesha udhaifu katika mipango ya fedha(budget) ya serikali. Pamoja na mifano yako elewa kwamba " lakuvunda halina ubani". Furahia mshahara wako ulioupata nov 03
 
Fanyeni kazi acheni kupiga umbeya mwisho wa mwezi bado tayari mshaanza kulalama hela ya mwisho wa mwezi. Je mngelikuwa mnafanya kazi katika kampuni binafsi ambapo mshahara hutoka tarehe 30 si mngelia nyie vp!!!!
Mnalo babu mie niko sekta binafsi tumevuta salary tangu jana nyie wa serikali ya JK ngojeni tareh igote, wanawasubiri STANBIC tena.
 
Mkuu hilo liko wazi wala hakuna ubishi hapo. Mkwawa wamebandikiwa tangazo kuwa mshahara utachelewa mwezi huu. Na pia tukumbuke wiki kama tatu zilizopita serikali ilisema kufikia novemba 15 ingekuwa imetoa post za walimu kwani maandalizi ya pesa yalikuwa yamekamilika na wangeripoti vituoni mwazoni mwa desemba lakini mpaka leo wako kimya.hii inaonesha pia kuwa mambo si mazuri serikalini, atleast kipesa.sijui wanafanya kazi gani au wanaona vyepesi kukusanya kodi kutoka kwa wafanyakazi ambako ni rahisi na kuwaacha wengine waendelee kudunda?au ndo kusema wanakusanya na kuhifadhi mifukoni mwao?kila siku ni kutuimbia tu uchumi unakua kwa kasi, yako wapi sasa?
 
Sijui safari hii watachukua wapi! Rostam siamini kama atakubali. My be NSSF yetu macho. Karibu kwenye NGO.
usisahau kuwa serikali iliahidi kulipa malimbikizo ya madai ya walimu. Hapo ngoma inogile! Lakini poa tu Mh. Mkulo atapiga goti kwa Cameroon, au vipi!
 
Fanyeni kazi acheni kupiga umbeya mwisho wa mwezi bado tayari mshaanza kulalama hela ya mwisho wa mwezi. Je mngelikuwa mnafanya kazi katika kampuni binafsi ambapo mshahara hutoka tarehe 30 si mngelia nyie vp!!!!
uwe unafanya utafiti kabla hujasema. serikali ilitangaza kutoa mishahara kila tarehe 24 ya mwezi. sasa kama mwezi huu unatoa tarehe 24 na unaofuata ukatoa tarehe 30..huo ni mwezi wenye siku 28?
 
Acheni yeye apande mapipa akale huko majuu .Hivi next visit yake ni lini na atakuwa Nchi gani na watu wangapi ?
 
usisahau kuwa serikali iliahidi kulipa malimbikizo ya madai ya walimu. Hapo ngoma inogile! Lakini poa tu Mh. Mkulo atapiga goti kwa Cameroon, au vipi!
Mkuu naomba nikusahihishe, huyo Kameruni hakusema mwenye shida apige goti... alisema Nchi ikitaka msaada ishike ukuta na Tanzania haijasema lolote lenye kuonyesha msimamo mzito. Membe alibwata-bwata hapa kutuzuga kisha siku chache baadaye wakampokea Prince Charles kwa heshima zote, tunazijua haki za binadamu lakini kitendo cha kuliweka hili la ushoga kama sharti la misaada kwa nchi maskini ni matusi makubwa mno. Binafsi nalipinga kwa nguvu zote.

Nakumbuka niliona mahali hapa JF, member mmoja kaandika Kameruni alimwambia JK... "umezidi kuomba-omba, ukitaka msaada sasa shika ukuta..."

Tunarudi enzi za Mwinyi, mashule yamefungwa kabla ya muda, serikali imefilisika

Serikali corrupt hazikusanyi kodi - Mwalimu Nyerere !!!!
Ni kweli aisee!

Yule mzee alisema itabaki tu kufukuzana na wamachinga barabarani.
 
Fanyeni kazi acheni kupiga umbeya mwisho wa mwezi bado tayari mshaanza kulalama hela ya mwisho wa mwezi. Je mngelikuwa mnafanya kazi katika kampuni binafsi ambapo mshahara hutoka tarehe 30 si mngelia nyie vp!!!!
kwa kawaida tunalipwa tarehe 25 hadi 25 ya mwezi unaofuata hapo sio mwezi; nahisi wewe ni mbovu wa hesabu
 
Mwambie mangi pale dukani aekisitendi contract mpaka kwenye thate hivi ndo uanze ku offset madeni mkuu. I think it can be done! Uongo mazee, post yangu ya 800 hii.
 
ni kweli mwezi uliopita serikali ilichukua pesa hapa TCRA......

Hivi TCRA si ndo ile Mamlaka ya Mawasiliano na kufanya nini cjui ambao wameshindwa kabisa kusimamia zoezi la usajili wa namba za simu?! anyway, habari za namba za simu sio issue; my interest ni kujua biashara inayofanywa na TCRA hata wawe na fedha za kulipa wafanyakazi wa serikali!!!
 
Fanyeni kazi acheni kupiga umbeya mwisho wa mwezi bado tayari mshaanza kulalama hela ya mwisho wa mwezi. Je mngelikuwa mnafanya kazi katika kampuni binafsi ambapo mshahara hutoka tarehe 30 si mngelia nyie vp!!!!
mkuu mwisho wa mwezi inategemea kama serikali huwa yalipa tar 25 kila mwezi basi mwisho wa mwezi sio tarehe 30 kuna wajiri wengine mwisho wa mwezi nitarehe 20,mwisho wa mwezi ni mzunguko wa siku thelathini tarehe haijalishi inategemea mwajiri anaanza kuhesabu lini mwezi wake,hope unshanfahamu
 
Mkuu NasDaz unatetea nini? Hoja iliyopo ni kwamba Serikali inashindwa kugaramia matumizi yake ya kawaida Kama mishahara ya watumishi wake. Hii ni Hali ya hatari inayoonyesha udhaifu katika mipango ya fedha(budget) ya serikali. Pamoja na mifano yako elewa kwamba " lakuvunda halina ubani". Furahia mshahara wako ulioupata nov 03

Sitetei mtu ila napinga hali ya mtu kujiona yupo kwenye position fulani then akachukulia wote ndo wapo hivyo hivyo!!!! By the way, hata mtoa mada ameonesha utata kwamba last month kuna mtu ali-post kwamba serikali wamefilisika kv wamechelewa kulipa mishahara. mtoa mada anasema, alimuona jamaa ni mzushi kv yeye alikuwa amelipwa on time!! Kwahiyo, ikiwa watu last month walisema serikali wamechelewa kulipa salary na yeye akaona ni uzushi kv yeye alikuwa ameshalipwa; sasa inakuwaje leo hii kv yeye hajalipwa ndo azani wenzake wote hawajalipwa?! Na yule niliyemnukuu asiwasemee wenzake, ana uhakika gani kwamba sekta binafsi wote wamelipwa?! hakuna kutetea hapo, tunaangalia logic kwa kuacha siasa pembeni!!
 
Unafanya kazi kwa wahindi unategemea mshahara tar 25, sahau ndugu. Hii serikali inaunga unga sana suala la mishahara na matumizi mengine. Kumbuka wachina kibao wajenga mabarabara ya magufuli wamesepa kurudi kwao kwa kutolipwa. Na trend inajulikana matumizi kuliko mapato.

Pole sana!!!
 
Back
Top Bottom