Hali ya serikali ni tete? Mpaka sasa mishahara kitendawili

Fanyeni kazi acheni kupiga umbeya mwisho wa mwezi bado tayari mshaanza kulalama hela ya mwisho wa mwezi. Je mngelikuwa mnafanya kazi katika kampuni binafsi ambapo mshahara hutoka tarehe 30 si mngelia nyie vp!!!!

Nadhani huelewi ulinenalo, unaposema mwisho wa mwezi bado wamaanisha nini? Mwezi una siku ngapi? Kama huwa unapokea mshahara trh 25 basi watakiwa kupokea trh 25b tena isizidi... na hata ukihesabu siku utapata ni siku ngapi kisha check mwezi huwa una siku ngapi! unaposaini mkataba wa kazi kuna kipengele cha tah ya kupokea mshaara na siku zote huwa haizidi thr 28, hiyo ndo kawaida.
 
Ni kweli bandugu kuna jamaa moja ambia mimi salary slip iko pelekwa kwa benki tangia alhamisi lakini napata benki haiko na kitu hata kwa masaa haya..alafu hii jamaa ingine ambia sisi mshahara tarehe 30 kwani kama jana napata 24 alafu leo napata 30 kweli hyo ni mwezi moja au napata mwezi na masiku 6?sasa serekari nalipa sisi kwa masiku 30 ama masiku 36?mimi iko naona bantu leo balipwa baada kwa masiku over 30 days

Hiki kiswahili ni cha kwako au umejifanyisha?! Na kama ni cha kwako ilikuwaje ukaingia kwenye payroll ya serikali?! By the way, salarly slip ilienda benki kufanya nini? Kwani benki ndio mwajiri wako hata salary slip iende huko?! Au unamaanisha payroll?! na kama unamaanisha payroll, payroll inapelekwa na mwajiri na hawezi kupeleka payroll bila cheki! By the way, kama ni payroll, ni payroll ya namna gani unaizungumzia?! manake, kwa majority ya wafanyakazi, payroll huwa inapelekwa NMB Head Office na ni soft copy na payroll ya aina hiyo huwa inatoka hazina na ndiko huko huko unakotoka mkwanja.....sasa inakuwaje hazina wapeleke payroll bila cheki? wakati huo walitarajia nani apeleke hiyo cheki?! How come Bank wapokee payroll inayoonesha (say) total amount TZS 10m, na wao wamepewa cheki ya 5m? wata-balance vipi?
 
Nawashangaa sana mnaobisha juu ya serikali hii kutokuwa na mipango madhubuti.Hebu chukulia mfano huu, wafanyakazi wa mamlaka ya hali ya hewa wanatakiwa kulipwa allowance ya asilimia 25 ya mshahara wake kila ifikapo tarehe 15 ya kila mwezi.Ajabu ni kwamba hivi sasa tunalipwa asilimia 9 tu ya mshahara wetu.Kila tukidai hilo wanajibu serikali haina fedha.Mwezi huu Novemba allowance hiyo kiduchu imelipwa tarehe 23.Sasa hatujuia mshahara utalipwa lini maana hadi leo hii hakuna kitu kilinachosomeka.Na ukondoo wa wafanyakazi wengi ambao unatokana na kutokuwa na elimu inayostahili ndani ya TMA ndiyo inayofanya wawe wa kusema ndiyo kwa kuogopa kuondolewa kazini.
Ndugu zangu serikali hii ya sasa ni matatizo matupu.Unahitaji kuwa na ujasiri wa namna yake kuitetea mbele ya watu.

Ukiona hivyo, ndo wana mpango wa kuiondoa hiyo!!! TANESCO wenzenu walikuwa nayo hiyo na iliondolewa zaidi ya miaka mitano iliyopita....wenyewe walikuwa wanaiita PP! Kaa chonjo, kama ulikuwa unaipangia bajeti hiyo, basi acha kufanya hivyo na ichukulie ni kama PRODUCER SURPLUS! NUnafahamu wht's Producer Surplus? chukulia unaenda na gunia la vitunguu kariakoo kupiga bei. Unatoka nyumbani ukiwa na nia ya kwenda kuliuza kwa Sh. 100,000/=. Unafika K/koo unakuta soko kwa upande wako ni zuri na hivyo unauza Sh.150,000/=. Hiyo extra 50k ndio producer surplus therefore ukienda siku nyingine ukakuta unauuza kwa ile ile 100k, usilalamike!
 
Fanyeni kazi acheni kupiga umbeya mwisho wa mwezi bado tayari mshaanza kulalama hela ya mwisho wa mwezi. Je mngelikuwa mnafanya kazi katika kampuni binafsi ambapo mshahara hutoka tarehe 30 si mngelia nyie vp!!!!
Usibishie kitu usichokijua weye, sometimez uwe unakaa kimya. Serikali ina madeni kibao, hata pesa za kulipia mishahara wafanyakazi haina, imejaa mikopo tu. Madenti wanapolia kwamba hawana mikopo toka HESLB sio kwamba wanatania, serikali imefulia. Sie wazabuni hatujalipwa hadi leo, na wewe unakuja kutuongezea hasira.
 
Mkuu, kama unadhani indicator ya serikali kufilisika si kucheleweshewa mishahara watumishi wa umma basi kwako ni kigezo gani? Tatizo hapa si fluctuation ya mishahara, bali hoja ya kufilisika inachagizwa na serikali kukopa fedha TCRA, Stanbic, CRDB na kwingineko ili kulipa mishahara. Kama kweli hivyo ndivyo, those are indicators of a collapsing govt financially, which may lead to bankrupcy. Hoja ni kwanini serikali ikope kwa ajili ya kulipa mishahara?

Bado kuchelewa ulipaji wa mishahara sio indicator ya kufilisika....wakati mwingine ni utendaji mbovu tu. By the way, serikali itakopaje TCRA?! Kwani hiyo TCRA ni ya nani?! Kwani ni hela toka wapi ndio maalumu kwa ajili ya mishahara?! By the way, kama unakubali watu kama Stanbic wanaikopesha serikali, then serikali is far from kufilisika......katu wawezi kumkopesha mtu anayefilisika, labda ungeniambia wanakopa benki ya wanawake, ningekuelewa!

 
Ukitokea chaguzi ndogo kama mbili ivi mfululizo kwa mda mfupi am sure serikali itatangaza mufilisi.
Expense za Igunga madhara yake ni ya mda mrefu
 
Kwa kweli hali ni mbaya sana kwa watumishi wa serikali ila kinachonishangaza ni kwamba kila mtu anaumia kivyake,there is no collective complaints.
hivi vyama vya wafanyakazi havioni hili tatizo? mpaka leo tarehe 1 december mshahara wa mwezi november haujalipwa na bado tumekaa kimya?

kweli watz ni wavumilivu.
 
Back
Top Bottom