Tanzania Njema Yaja
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 3,041
- 2,417
Mkuu hii naona ni pamoja na kuhamia mkoa ilipo ile hosp ya vichaa.....Poleni sana, ila mimi siwezi kumuombea kwa sababu ana ulafi na uroho wa usalama wake
Mkuu hii naona ni pamoja na kuhamia mkoa ilipo ile hosp ya vichaa.....Poleni sana, ila mimi siwezi kumuombea kwa sababu ana ulafi na uroho wa usalama wake
Ila huyu mgonjwa kuna wakati anaenda Nijeria kwa TBJ labda unyenyekevu wa TBJ utambadili soon na kuwa mtu wa watu.....Migonjwa ya design yake huwa haifi haraka na ina maudhi balaa. Gonjwa bishi hata kwa madaktari, yani hata dawa za kumtibu yeye mwenyewe anataka kujipangia ilihali tiba aijuae yeye ni za tunguri na kupiga ngoma za kupunga majini.
Huyo mgonjwa alikuwa afe kabisa, alikata kauli Nov. 2015, ugonjwa wa mamvi ulimshika, akakata kauli, alikaa wiki bila kuongea, ghafla akazinduka, sindano ya Pombe kali aina ya Magufuli alichomwa... si akasimama... anadunda..!! na Alipozinduka, aliimba sana, Sisi mbele kwa mbeleee, mtaisoma namba eeehh... sisi mbele kwa mbeleeee...!!
Mgonjwa sasa hv hafi tena, anatembea na HAPA KAZI TU...!!
Na juzi kati, sauti ilisikika ktk kikao huko Dodoma cha huyo mgonjwa, kwambaaaa... kama Nov. 2015 hajafa, hatakufa tenaaaaa....!!! ataishi mileleee...!! Hapa Kazi tu..!!
🙄😛😀😀😀
Hodi humu ndani?
kuugua ni jambo la kawaida, na kuugua sio kufa. wangapi wazima, tena wauguzaji, hufa na kuwaacha wagonjwa? magonjwa mengi ya siku hizi huletwa na mtindo wa maisha kama ulaji mbaya, kutofanya mazoezi nk. lakini pia kuna maradhi ya kurithi, ambayo naamini ndio yanayomsumbua mgonjwa. historia ya ukoo wake inaonesha umekuwa na magonjwa sugu kizazi hadi kizazi. lakini tusikate tamaa. japo wasima dawa nyingi katumia, tiba mbadala mmejaribu? kuna taarifa kuwa mgonjwa wako anachagua sana dawa na hata wanaotaka kumwona na walau kumpa ushauri wakifika wodini hataki kuwaona, anafumba macho, je ni kweli? mshauri awe na amani ya nafsi, nayo ni tiba pia.
