Uchaguzi 2020 Hali si shwari ndani ya CCM, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Bashiru Ally amekemea vikali baadhi ya wanachama wanaopanga kukisaliti chama


Yaani mtu unalipwa kwenda kuwaona wasanii wa sanaa na wasanii wa siasa... kwanini usiende?? Na ikibidi unazomea kabisa...!!
 
Katibu wa ccm anahangaika kama kuku anataka kutaga
 
Bravo Wahaya. Ngoma inogile. Kura yenu mmeshaanza kupiga. Bwana yule OUT.
 
Upuuzi mtupu.
 

Siyo hayo tu, kuna watu hawajaathiriwa moja kwa moja na mfumo mbovu wa uongozi wa magu lakini roho zao zipo upinzani, hata kama hujaguswa ile kuona wapinzani wananyanyaswa na kupewa kesi za kubambikiwa, Mpinzani mmoja amenusurika kuuawa kwa risasi nyingi na uchunguzi haujafanyika hadi leo, kuona watu wakifilisiwa kwa sababu ambazo ni petty ambapo zingetumika njia zisizo na madhara kumuadhibu mhusika (Manji) badala ya kuharibu biashara zake zilizotoa ajira za maelfu ya watu, kuona Rais akiisigina katiba kwa miaka mitano mfululizo, kuona Rais amejigeuza mungu-mtu kila mtu anamwabudu, kuona kuna sehemu zikididimizwa kimaendeleo na zingine zikipendelewa, na madudu mengine mengi, haya mambo yamechosha watu lazima sote tuwe upinzani.

WaTz tuache ubinafsi tujifunze kupaza sauti na kufanya maamuzi kwaajili ya wengine, kwa yanayoendelea nchini haihitaji uathiriwe moja kwa moja ndipo uone upinzani ni mbadala. Yanayoendelea ni machafu tuyapinge kwa nguvu zote hata kama unajiona uko safe kwa sasa.

Tuwachague wapinzani ili tuwadai katiba mpya ambayo itatumika kuwaondoa na wao wakiharibu. Hakuna chama kinachotakiwa kujiona kina hati miliki ya kuiongoza nchi hii pekeyao, CCM hawawezi kutupa katiba mpya kwasababu hawajawahi kuiahidi, Shime watanzania.
 
Wanaoitwa "wasaliti" ni wachache tu; wala Katibu Mkuu hakutakiwa kulizungumzia hilo kwani ni haki yao ya kikatiba. Sumaye, Lowassa, Kingunge na Mwapachu walikuwa ni "wasaliti" wakuu sana mwaka 2015 lakini tunajua yalivyoisha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…