Uchaguzi 2020 Hali si shwari ndani ya CCM, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Bashiru Ally amekemea vikali baadhi ya wanachama wanaopanga kukisaliti chama

Kwa kuwa hakuna mwenye ubavu wa kuninyima haki yangu ya Mauti basi hakuna mwenye uwezo wa kubadili msimamo wangu wa kutetea Znz~ Mzee Aboud Jumbe Rais alietawala muda mrefu zaidi Znz
We jamaa umekomboka kifikra.
Bravo
 
"Wanaohama CCM wakidhani wananguvu,wakitoka wanageuka kama vichaa, wafuatilieni wote waliohama CCM, hakuna mwanaCCM maarufu kuliko CCM, ukijiona maarufu ujue umeazimwa umaarufu na CCM , siku Chama kikikutupa ama ukikitupa umaarufu unakoma. Wapo watakaookota makopo nawahakikishia" Bashiru Ally.
 
😍😍😍👍
 
Kura ni siri ya mtu. Wana ccm wengi wasiopenda udhalimu, dhulma na mienendo yote isiyofaa watachagua raisi, madiwani na wabunge wa upinzani. Dr. Bashiru utajuaje???

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Kwa heshima kubwa, naomba nikuulize. Mkuu, umefanya upembuzi yakinifu wa kutosha na kugundua kuwa Katiba Mpya ndiyo itatuwafanya watanzania tuboreshe zaidi maisha yetu kiuchumi, kijamii huku Tanzania ikizidi kuimarika kimataifa katika nyanja zote...?

Ni hivi sasa Kenya wanataka kukarabati katiba yao ambayo ilikuwa mpya kuliko ya kwetu miaka michache illyopita! Mkuu unataka kuniambia Kenya walipata katiba 'mtumba'? Jibu nadhani ni hapana. Pia nafikiri kama sijakosea kuna uwezekano Kenya walitaka katiba mpya baada ya kushindwa kufanya upembuzi makini kujua hasa ni nini wanataka ili waboresha maisha yao wao kama wakenya na Kenya yao kwa ujumla.

Binafsi,nadhani Katiba mpya si- muarobani wa kutatua changamoto tulizonazo. Kwa katiba hii mnayoinoa 'kuu kuu' tukiwa makini kabisa na tukiendelea kujielewa kama nyakati hizi, hii katiba ya sasa inatosha kutuwezesha kufikia malengo tuliyojiwekea na tutakayojiwekea!

Hata hivyo, Mkuu nakurudisha kwenye aya ya kwanza ya post yangu hii. Mkuu ebu tufafanulie kinaga ubaga ni kwa namna gani Katiba mpya itaboresha maisha ya Watanzania wote na itatuhakikishia Muungano wetu kama nchi unaendelea kudumu.

Karibu.
Tatizo kubwa la nchi za Dunia ya Tatu Ni Gorvanance' ie uendeshaji na management ya Uchumi,Siasa,na masuala yote ya huduma za Jamii.Hapa ndio tukipokwama!
Katiba Bora Ni Muarabaini ya yote!
Nchi yetu Ni masikini na inaRasilimsli za kutosha!
Tatizo Ni namba Bora ya kutumia Rasilimali zilizopo kuboresha maisha.
Mfano ...katiba ya Sasa inamla Madaraka makubwa Sana Rais,hiki hakufai...Ni lazima kuwe na check and balance..!
Fikiria ujenzi wa Daraja la Baharini la Surrender pale Koko Beach !
Huu Ni uamuzi usio na busara Wala tija...fedha hizo zingeweza kuchimba visima lukuki vya maji,au kujenga mabwawa ya maji kuvuna maji ya mvua na kuendekeza kikimo Cha mbogamboga,ambazo zinahitajika Sana nchini na nje ya nchi!
Hili lingewezekana kupitia mijadalayenye tija!
Kuna watu wanaushi kando ya mito na maziwa lakini hawana maji salama ya kunywa!
Daraja la Koko Beach linawahusu !?
Leo hii tuna Bunge lisilo na meno! haliwezi kujadili miswaaada kwa maslahi ya walipa Kodi!
Hii yote Ni matunda ya Katiba mbovu!
Hii Ni mifano michache tu !
Mojawapo ya urithi mbovu kabisa wa Nyerere Ni huu!
Na yeye alikiri!
Lissu lete Katiba Mpya ,tuanzie alipoishia Warioba!
 
Watu hawatakubali kila kitu wanachopanga Mwaka huuu kinakataa Kwa sababu wanaamini Sana bunduki kuwa itwwasaidia

Ni kweli unaweza kuamini katika bunduki, mabavu na wizi wa kura lakini kuna mahali inafika Umma unakataa Kama iivotokea wakti Nicolae Ceaușescu wa Romania enzi zile....!!

Nicolae Ceaușescu was a Romanian communist politician and leader. He was the general secretary of the Romanian Communist Party from 1965 to 1989, and the second and last Communist leader of Romania. Wikipedia
 
Kifo cha CCM ndio pona ya Watanzania wote.
Hivyo vitisho vipo wakati bado upinzani upo.
Siku upinzani ukifa hao wanaojaribu kukiasi chama watafanyiwa yale ya Lisu.
Mana lengo kuu la kina Bashiru ni kuhakikisha Katiba inabadilishwa na kumwongezea mwenye nchi muda wa kutawala Tanzania ili akamilishe miradi yake anatojenga.

Nafikiri mkubwa ndiye anayelipa Kodi ya kuendesha nchi hii mana kila kitu anafanya yeye.
 
"Wanaohama CCM wakidhani wananguvu,wakitoka wanageuka kama vichaa, wafuatilieni wote waliohama CCM, hakuna mwanaCCM maarufu kuliko CCM, ukijiona maarufu ujue umeazimwa umaarufu na CCM , siku Chama kikikutupa ama ukikitupa umaarufu unakoma. Wapo watakaookota makopo nawahakikishia" Bashiru Ally.
Sio kwa sababu ya CCM Bali ni matumizi ya dola ndio pona ya CCM. Leo hii kila kitu CCM instumia nguvu lakini ni wepesi sana.
CCM ni wazee tuu waliobaki mana wengi wamefichwa wasipate taaria kupitia vyombo vya habari. Hata hao wazee wangepata information basi wasingebaki mana wangejua kuwa Chama chao kimeharibiwa
Hao akina Polepole na Bashiru ndio wanaokivuruga Chama . Vijana wengi sana wakike na wa kiume wapo Upinzani. Hao ndio Jeshi kamili. Wengi wakiwa wanajua haki zao za kuchagua mtu wanayemkubali na sio kulazimishwa.

CCM wapo wakiopewa na Noah za makinikia na waliokosa Mgao . Waliopata ndio watakaomchagua Mgombea wa CCM na wabunge wake. Hata hivyo wanaCCM wengi hawakupata mgao wa Noah za makinikia. Hao watapiga kura za hasira kwa kuona wenzao wanakula bata na Noah zao .
 
Tatizo kubwa la nchi za Dunia ya Tatu Ni Gorvanance' ie uendeshaji na management ya Uchumi,Siasa,na masuala yote ya huduma za Jamii.Hapa ndio tukipokwama!
Katiba Bora Ni Muarabaini ya yote!
Nchi yetu Ni masikini na inaRasilimsli za kutosha!
Tatizo Ni namba Bora ya kutumia Rasilimali zilizopo kuboresha maisha.
Mfano ...katiba ya Sasa inamla Madaraka makubwa Sana Rais,hiki hakufai...Ni lazima kuwe na check and balance..!
Fikiria ujenzi wa Daraja la Baharini la Surrender pale Koko Beach !
Huu Ni uamuzi usio na busara Wala tija...fedha hizo zingeweza kuchimba visima lukuki vya maji,au kujenga mabwawa ya maji kuvuna maji ya mvua na kuendekeza kikimo Cha mbogamboga,ambazo zinahitajika Sana nchini na nje ya nchi!
Hili lingewezekana kupitia mijadalayenye tija!
Kuna watu wanaushi kando ya mito na maziwa lakini hawana maji salama ya kunywa!
Daraja la Koko Beach linawahusu !?
Leo hii tuna Bunge lisilo na meno! haliwezi kujadili miswaaada kwa maslahi ya walipa Kodi!
Hii yote Ni matunda ya Katiba mbovu!
Hii Ni mifano michache tu !
Mojawapo ya urithi mbovu kabisa wa Nyerere Ni huu!
Na yeye alikiri!
Lissu lete Katiba Mpya ,tuanzie alipoishia Warioba!
Kuna mambo yanahitaji mjadala mpana na mawazo mbadala mfano suala la Bima ya Afya ni jambo rahisi sana kuwapatia watanzania wote bima kwa Mwaka mmoja tu na Wizara ikaingiza mabilioni ya fedha. Serikali ikachangia kidogo sana. Tofauti na ujinga wanaoufanya akina Polepole na Bashiru Wa kununua wapinzani na kuwahonga vyeo na ubunge .
Pesa hizo zingeongezewa kwenye mradi wa bima ya Afya na watu maskini wangetibiwa kwa kuchangia matibabu yao kwa kutumia Bima.
Kumwachia mtu mmoja na marafiki zake kupanga kila kitu bila kusikiliza maoni ya watu matokeo yake wanadhani kuwa kukosolewa ndio kunakowakwamisha . Yani mtu akikosoa anaonekana ni mbaya kuliko Mla Rushwa na mwizi wa fedha za umma anayeunga mkono .
Lugumi Leo yuko wapi na kesi yake? Wapi mawaziri wsliojihusisha na ufisadi?Au wameachwa kwa sababu wanazidi kuunga mkono juhudi huku wakiwa wameficha matrilioni ya fedha za umma kwenye familia zao na majumani mwao. Wanaoneka ni watu safi kwa sababu ya kusifia utadhani kusifia kunakuza pato la nchi na kuongeza kodi ?
 
Back
Top Bottom