Uchaguzi 2020 Hali si shwari ndani ya CCM, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Bashiru Ally amekemea vikali baadhi ya wanachama wanaopanga kukisaliti chama

'tunataka pia kujenga viwanda vya kusindika, kile kiwanda kilichokufa cha TANICA tunataka kukifufua, tunataka kuimarisha ushirika kwa kuwa na viongozi wenye uweledi, waaminifu na waadilifu."

Daah Yaani anavyoongea ni kama vile hii miaka 5 iliyopita serikali ilikua chini ya Chadema.
Yaani na ngonjera zote miaka mitano za Hapa Kazi Tu, hakuna rais aliyewahi kutokea Tanzania kama Magufuli, Magufuli ni mchapakazi, Magufuli ametumwa na Mungu, na utopolo wa aina hiyo, Bushiri hana aibu kabisa anakuja mbele ya wakulima kuwapa ahadi badala ya kuwathibitishia hapa kazi tu na uchapakazi wa Magufuli ulivyowanufaisha!!! Walikuwa preoccupied na kuua upinzani - nunua wabunge na madiwani, itisha chaguzi ndogo, nk na pesa ya mlipa kodi ikawa inateketea - ingeweza kuwekezwa kuongeza tija katika kilimo, ushirika, elimu, au afya. Wajukuu, vitukuu, na vilembwe wenu watakuja kuyatandika bakora kali makaburi ya akina bushiri na makufuli. Laana tupu!!!
 
TL kawapagaisha. Mnasubiri adondoke afe lakini kama ambavyo Mungu hakupenda iwe kwa risasi, haitatokea.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, ameeleza kuwa baadhi ya wanasiasa mpaka kuisha kipindi hiki cha Kampeni, wataokota makopo kwa kukosa uelekeo wa siasa.

ameyasema hayo leo tarehe 19 Septemba, 2020 katika kikao cha Halmashauri kuu ya wilaya ya Kyerwa.

"Wanaohama kutoka CCM wakidhani wananguvu, wakitoka wanageuka kama vichaa, wafuatilieni wote waliohama CCM, hakuna mwanaCCM maarufu kuliko CCM,"

Aidha Dkt. Bashiru amefafanua kuwa "Ukiona we maarufu ujue umeazimwa umaarufu huo na CCM , siku Chama kikikutupa ama ukikitupa umaarufu unakoma hapo hapo. Wapo watakaookota makopo ninawahakikishia."

"Kuna watu wapo miguu juu kama mende, tena miguu juu kwa raundi moja ya kampeni wakati zipo sita, wamejileta wenyewe, wajanja kama mzee Mrema na Cheyo wakasema hapa tunamuunga mkono Magufuli, waliobaki wote tusilaumiane, tutatumia nguvu zote za CCM bila kujali udhaifu wao, tutatumia uwezo wetu wote bila kujali udhaifu wao, tutawashinda, hadharani kwa kishindo.." Katibu Mkuu ameeleza

Aidha, Katibu Mkuu ameeleza namna Chama kilivyojipanga kuhakikisha kinaboresha maslahi ya wakulima na kukata mirija ya wanyonyaji katika biashara ya mazao ikiwemo zao la Kahawa.

"Tunataka kufanya utafiti badala ya kutegemea zao moja la kahawa. Hatumaanishi kwamba tunaliacha, tunataka pia kujenga viwanda vya kusindika, kile kiwanda kilichokufa cha TANICA tunataka kukifufua, tunataka kuimarisha ushirika kwa kuwa na viongozi wenye uweledi, waaminifu na waadilifu."

Katibu Mkuu amefafanua pia kwa kueleza kuwa, "Tunataka muwe na sauti kuhusu bei ya kahawa yenu, lakini tunataka kukata mirija ya unyonyaji wa jasho lenu , kama mirija ipo kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya tutaikata, kama ipo kwenye polisi tutaikata, kama ipo kwa walanguzi tutaikata, kama ipo kwenye Chama tutaikata, sasa si kutumbua majipu, zamu inayokuja ni kukata mirija ya unyonyaji."

Kikao hiko, kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, wakiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Ndg. Wilbroad Mutabuzi

Kikao hiko ni mfululizo wa vikao vya ndani vinavyoendelea nchi nzima, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha umoja, mshikamano, nidhamu na ushirikiano, kuhakikisha ushindi mkubwa unapatikana katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020.

Imetolewa na;
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
 
Maccm hawana akili kabisa. Shida wanahangaika na viongozi wkt Wtz ndio hawawataki...

Wasisahau kua waliwekeza kwenye kununua wabunge na madiwani lkn bado watz hawataki jusikia kuhusu ccm
 
Mnalipwa bei gani kusambaza huu ujinga ? Chama chenye viongozi waliopitisha Mhujumu uchumi Deo Mwanyika na Mtekaji Ramadhan Ighondu kina uhalali upi wa kutaka watu wawe wehu ?

Mtu anayeshinda kwa waganga ana uhalali gani wa kutisha wengine ?
Bashiru atulize mshono, lichama lenyewe limeisha mshinda nadhani wakuokota makopo ni yeye.
 
Labda kama ni diwani wa Kipawa
Ha ha haa! Mkuu, tarabu aisee. Mbavu zangu zitalegea. Ha haa haa!
===
Narudi kwenye mada.
Kwa mujibu wa katiba ya CCM toleo la hivi karibuni, kila mwanachama awe kiongozi asiwe kiongozi awe anagombea uwakilishi kwenye ngazi yoyotea asiwe anagombea analojukumu la kufafanua vyema ilani ya Chama, mafanikio yaliyofiwa na chama matarajio ambayo Chama kinayo katika kudumisha mapinduzi ya kuimarisha maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Mkuu, si diwani wa Kipawa tu ni kwa kila mwanaCCM anapaswa kuelezea mafanikio ya chama chake.
 
h
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, ameeleza kuwa baadhi ya wanasiasa mpaka kuisha kipindi hiki cha Kampeni, wataokota makopo kwa kukosa uelekeo wa siasa.

ameyasema hayo leo tarehe 19 Septemba, 2020 katika kikao cha Halmashauri kuu ya wilaya ya Kyerwa.

"Wanaohama kutoka CCM wakidhani wananguvu, wakitoka wanageuka kama vichaa, wafuatilieni wote waliohama CCM, hakuna mwanaCCM maarufu kuliko CCM,"

Aidha Dkt. Bashiru amefafanua kuwa "Ukiona we maarufu ujue umeazimwa umaarufu huo na CCM , siku Chama kikikutupa ama ukikitupa umaarufu unakoma hapo hapo. Wapo watakaookota makopo ninawahakikishia."

"Kuna watu wapo miguu juu kama mende, tena miguu juu kwa raundi moja ya kampeni wakati zipo sita, wamejileta wenyewe, wajanja kama mzee Mrema na Cheyo wakasema hapa tunamuunga mkono Magufuli, waliobaki wote tusilaumiane, tutatumia nguvu zote za CCM bila kujali udhaifu wao, tutatumia uwezo wetu wote bila kujali udhaifu wao, tutawashinda, hadharani kwa kishindo.." Katibu Mkuu ameeleza

Aidha, Katibu Mkuu ameeleza namna Chama kilivyojipanga kuhakikisha kinaboresha maslahi ya wakulima na kukata mirija ya wanyonyaji katika biashara ya mazao ikiwemo zao la Kahawa.

"Tunataka kufanya utafiti badala ya kutegemea zao moja la kahawa. Hatumaanishi kwamba tunaliacha, tunataka pia kujenga viwanda vya kusindika, kile kiwanda kilichokufa cha TANICA tunataka kukifufua, tunataka kuimarisha ushirika kwa kuwa na viongozi wenye uweledi, waaminifu na waadilifu."

Katibu Mkuu amefafanua pia kwa kueleza kuwa, "Tunataka muwe na sauti kuhusu bei ya kahawa yenu, lakini tunataka kukata mirija ya unyonyaji wa jasho lenu , kama mirija ipo kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya tutaikata, kama ipo kwenye polisi tutaikata, kama ipo kwa walanguzi tutaikata, kama ipo kwenye Chama tutaikata, sasa si kutumbua majipu, zamu inayokuja ni kukata mirija ya unyonyaji."

Kikao hiko, kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, wakiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Ndg. Wilbroad Mutabuzi

Kikao hiko ni mfululizo wa vikao vya ndani vinavyoendelea nchi nzima, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha umoja, mshikamano, nidhamu na ushirikiano, kuhakikisha ushindi mkubwa unapatikana katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020.

Imetolewa na;
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Hizi taarifa Membe anazo lakini?
 
FB_IMG_1600525018800.jpg
 
Back
Top Bottom