Uchaguzi 2020 Hali si shwari ndani ya CCM, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Bashiru Ally amekemea vikali baadhi ya wanachama wanaopanga kukisaliti chama

Kifo kikiwa kinamuita nyani huwa miti yote inateleza.

Kila mbinu imetumika kuwafifisha wagombea wa vyama vingine lkn imeshindikana.

Matokeo yake huyu Mgombea wa chama chama fulani ameanza kuwatafuta wachawi ndani ya chama chake.

Hizi ni dalili mbaya Sana kwa huyu mgombea, kwamba anaenda kuangukia pua kwenye uchaguzi huu. Atakosa msaada hata ndani ya chama chake.
 
Itakua alivyozomewa na wananchi kamuamua kuwafukuza viongozi wa chama

Huyu katibu mkuu wa ccm amekulia Bukoba toka akiwa msaidizi wa marehemu Kinyondo; wakati huo hata ndoto za kwenda Chuo kikuu hakuwa nazo; anazifahamu siasa za kule kwa ndugu zake ISHOMILE hivyo alitakiwa kuwa wa kwanza kumshauri Jiwe namna ya kunavigate siasa za Bukoba. Mtu wa kufukuzwa uanachama anatakiwa awe Bashiru na sio hao viongozi wa ccm kule Kagera!!!
 
Ha ha haa! Mkuu, tarabu aisee. Mbavu zangu zitalegea. Ha haa haa!
===
Narudi kwenye mada.
Kwa mujibu wa katiba ya CCM toleo la hivi karibuni, kila mwanachama awe kiongozi asiwe kiongozi awe anagombea uwakilishi kwenye ngazi yoyotea asiwe anagombea analojukumu la kufafanua vyema ilani ya Chama, mafanikio yaliyofiwa na chama matarajio ambayo Chama kinayo katika kudumisha mapinduzi ya kuimarisha maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Mkuu, si diwani wa Kipawa tu ni kwa kila mwanaCCM anapaswa kuelezea mafanikio ya chama chake.
Mngekuwa si wanafiki mngeweza kumwambia Bashiru kuwa anayeipigania CCM kwa sasa ni yule tu aliyepitishwa kugombea Ubunge/udiwani na viti maalumu vyote na baadhi waliogombea hawajashinda au waliokatwa wenye hope za kupata teuzi. Mwambieni wanachama wa kawaida (wamiliki wa kadi za chama) hawana morali ya kukitetea na kukipagania chama kama ilivyokuwa zamani unakutana na mwana CCM wa kawaida anaanza kukueleza mambo ya CCM na kukinadi chama, Si sasa. Mwambie hata waajiriwa wa CCM (sijui kama unawafahamu) hawana ile ari ya kukipigania chama japo wanalipwa mishahara na chama, Yeye kama katibu alitakiwa awe ameshalifahamu hili ajue cha kufanya, tatizo ni mshamba na hajawahi kuwa mwanaCCM ndio maana amekalia matamko. Kuwa mwana CCM kabla ya cheo ni IMANI na MAPENZI, na kwa bahati mbaya Imani hiyo imeshawatoka wengi, CCM itamfia!
 
Mngekuwa si wanafiki mngeweza kumwambia Bashiru kuwa anayeipigania CCM kwa sasa ni yule tu aliyepitishwa kugombea Ubunge/udiwani na viti maalumu vyote na baadhi waliogombea hawajashinda au waliokatwa wenye hope za kupata teuzi. Mwambieni wanachama wa kawaida (wamiliki wa kadi za chama) hawana morali ya kukitetea na kukipagania chama kama ilivyokuwa zamani unakutana na mwana CCM wa kawaida anaanza kukueleza mambo ya CCM na kukinadi chama, Si sasa. Mwambie hata waajiriwa wa CCM (sijui kama unawafahamu) hawana ile ari ya kukipigania chama japo wanalipwa mishahara na chama, Yeye kama katibu alitakiwa awe ameshalifahamu hili ajue cha kufanya, tatizo ni mshamba na hajawahi kuwa mwanaCCM ndio maana amekalia matamko. Kuwa mwana CCM kabla ya cheo ni IMANI na MAPENZI, na kwa bahati mbaya Imani hiyo imeshawatoka wengi, CCM itamfia!


Bashiru atabakia kusema atafunga mitambo; huku wenzie wanaifungua!!!
 
Huyu katibu mkuu wa ccm amekulia Bukoba toka akiwa msaidizi wa marehemu Kinyondo; wakati huo hata ndoto za kwenda Chuo kikuu hakuwa nazo; anazifahamu siasa za kule kwa ndugu zake ISHOMILE hivyo alitakiwa kuwa wa kwanza kumshauri Jiwe namna ya kunavigate siasa za Bukoba. Mtu wa kufukuzwa uanachama anatakiwa awe Bashiru na sio hao viongozi wa ccm kule Kagera!!!
Au huyu hapa
 

Attachments

  • Kesho Mgombea Urais wa JMT Mhe. @TunduALissu atakuwa Kagera. Wananchi wa Kagera ( 480 X 480 ).mp4
    2.3 MB
Tuwachague wapinzani ili tuwadai katiba mpya ambayo itatumika kuwaondoa na wao wakiharibu.
Kwa heshima kubwa, naomba nikuulize. Mkuu, umefanya upembuzi yakinifu wa kutosha na kugundua kuwa Katiba Mpya ndiyo itatuwafanya watanzania tuboreshe zaidi maisha yetu kiuchumi, kijamii huku Tanzania ikizidi kuimarika kimataifa katika nyanja zote...?

Ni hivi sasa Kenya wanataka kukarabati katiba yao ambayo ilikuwa mpya kuliko ya kwetu miaka michache illyopita! Mkuu unataka kuniambia Kenya walipata katiba 'mtumba'? Jibu nadhani ni hapana. Pia nafikiri kama sijakosea kuna uwezekano Kenya walitaka katiba mpya baada ya kushindwa kufanya upembuzi makini kujua hasa ni nini wanataka ili waboresha maisha yao wao kama wakenya na Kenya yao kwa ujumla.

Binafsi,nadhani Katiba mpya si- muarobani wa kutatua changamoto tulizonazo. Kwa katiba hii mnayoinoa 'kuu kuu' tukiwa makini kabisa na tukiendelea kujielewa kama nyakati hizi, hii katiba ya sasa inatosha kutuwezesha kufikia malengo tuliyojiwekea na tutakayojiwekea!

Hata hivyo, Mkuu nakurudisha kwenye aya ya kwanza ya post yangu hii. Mkuu ebu tufafanulie kinaga ubaga ni kwa namna gani Katiba mpya itaboresha maisha ya Watanzania wote na itatuhakikishia Muungano wetu kama nchi unaendelea kudumu.

Karibu.
 
Nimecheka sanasanaa..yani Muuza ndizi anatufokea???anapata wapi ujasiri huo yani kipindi hiki kwamfano??yani anatufokea sisi???Subiri
 
Wakuu, Katibu Mkuu wa Ccm ametishia kuwafukuza wanaccm ambao wamepanga kumpa kura tundu lisu na kufikia mahali Ya kusema kuwa, watafukuzwa na watataifishwa Mali zao.

Unajua watu wanafanya mzaha na siasa za kutisha na kutumia manguvu pasipo ueredi na mwisho kutatokea anguko kubwa lisilotegemewa, siasa inataka akiri sio nguvu, Katibu badala Ya kutumia maneno Ya busara anatishia watu kuwa atawafukuza huku akijua kuwa kupiga kura ni Siri ya mtu mmoja, hupaswi kutisha watu kisa watapiga kura Kwa mtu mwingne huku ukijua kuwa kura ni Siri, Katibu alipaswa kutafuta sababu Kuu Ya wanaccm kupanga kupiga kura upinxani

Nimeshukuru Sana Ccm kugundua kuwa watu wamepanga kupiga kura Kwa upinzani nikiwemo Mimi Mwana Ccm Kada na kuna watu nawajua zaid ya Mia watapiga kura upinzani, Katibu ameshindwa kutambua kuwa kuweka haya hadharani ameshtua wengne waliokuwa wakinyanyaswa na Mwenyekiti kujiunga kwenye huo msafara
Naomba kumuuliza Katibu kuwa Mwenyekiti Alikuwa anachukua wapinzani anawapa vyeo anatuacha sisi miaka Yote, anawachukua anawapa nafasi za kugombea ubunge huku sisi akikataza katakata hata kuwapinga Leo hiii anatutisha? Haingiii akirini Mimi na watu Wangu tulihangaishwa na upinzani Mwaka 2015 had tukafanikiwa kumweeka madarakani halafau akatudharau kusema kuwa yeye ni Ccm Mpya akatutenga Halafu tuingie kwenye sanduku la kura tumpigie haiwezekani, tutapiga kura Kwa wingi Sana Kwa upinzani liwalo liwe hata atutishie afanye anachofanya sisi tutaonesha hasira zetu kwenye sanduku

Astakafirulah
 
No wanakera mno, wanauzi mno, wao walijiita ni Ccm Mpya, walitudharau na kutunyanyasa, tuliumia Sana Mwaka 2015 kumuweka magufuli madarakani ushindi ule ulituumiza matokeo yake amekuwa akitunanyanyasa kabisaaa na uteuzi wote kaufanya yeye, hukusikia alipokuwa Singida alisema kuwa yeye ndie aliemuweka mkumbo Ubungo? Inamaaana Ubungo hakukuwa na watu Wa Ccm? Wanauzi bhana heli aondoke tuanze upya

Polee. Huku Ubungo niliwahoji wana-CCM wenzangu kwamba kulikoni Kitila aletwe Ubungo ihali yeye Kitila alijipanga kugombea Iramba na pia huku Ubungo hafahamiki? Na Kuna wana-CCM maarufu tu?

Kuna mkutano mmoja Kitila alikuwa ana nadiwa. Aliyekuwa anamnadi akawaambia watu kuwa Kitila katolewa Singida kaletwa Ubungo ili awakomboe wana-Ubungo.

Mama lishe mmoja akajibu "Sasa katolewa Singida, atatusaidiaje"?
 
Bashiru ameshaanza kupaniki, tumeshasema mara nyingi kwa hii nafasi anapwaya. Aache ukali CCM sio wanafunzi wake wa UD!
Na kuwaombea watu ambao mmetofautiana mitazamo waokote makopo ni fikira za kichawi. Kama angekuwa Katibu Mkuu makini tena msomi kama yeye, angewatakia kila lenye heri huko waendako! Yaani Magufuli, Kabudi na Buushiri unaweza kufikiri ni mapacha - wana mitazamo na kauli za ki-old stone age.
 
MNISOME VIZURI :
Kila MTU ni shahidi kuwa Awamu hii ndiyo awamu iliyoletwa na Mungu kwa ajili ya kuondosha uovu Tanzania :
Kwanza 2015 watu waliomba Sana juu ya Uchaguzi ule lakini wengi wakiwemo wale wanaojiita mitume na manabii Ambao ni makada wa CCM wa wazi kama Gwajima,Lusekelo, n.k. na baadhi ya mashekhe walikua wanaomba huku mawazo yao yakiwa kwa Lowassa.

Mungu akawabadili lugha zao ndani ya CCM Lowasa akakatwa . JK akiwa upande wa Asha Rose au Membe. Kinana akiwa na Lowassa . Nape akiwa na Kinana aliyemuachia Jimbo la Mtama ambalo amelifanya mali yake sasa na yupo tayari kumkatakata mtu yeyote kwa mapanga aliyoyaita mitama alimradi apate ubunge.Kosa kubwa!!
Mkapa akiwa na JPM.Wazee walikua na Lowassa.
Wengine hawakua na nguvu zaidi ya kusikilizia upepo wa wajumbe wengi unakwendaje.

Mwaka huo 2015 roho wa Madaraka na utawala akamwingia Mkapa akapindua meza na upepo wa madaraka na utawala ukamwangukia JPM kwa ghafla na mchezo ukaisha JPM akapita katikakati ya Lowasa na Membe.
Mwanzo wa Tanzania mpya iliyokua inamsubiri Kiongozi wake ajaye.
Baada ya maombi ,sala na dua za watanzania Mungu akamleta Yohana ili asawazishe njia kwa ajili ya Kiongozi ajaye.
Lowasa akakimbilia upinzani na kupata kura nyingi sana japo masanduku ya kura za magumashi yalikua yamejazwa kila mahali . Bado ilikua alimanusura JPM abwagwe.

JPM akaingia madarakani kwa ahadi nyingi nzuri zenye mvuto kwa wanafunzi wa vyuo ,wafanyakazi,wafugaji,wakulima, wafanyabiashara, kuwaunganisha watanzania bila kujali makabila yao vyama vyao.

Mwanzo wa Tanzania mpya isiyo na uovu ni pamoja na Tanzania isiyo na imani za kukifanya Chama cha mapinduzi kuwa ni kikubwa kuliko Mungu. Tumeona watu wakitekwa ,kununuliwa kwa rushwa za fedha na ahadi za madaraka. Wakurugenzi na maDC na maRC kugeuka kuwa watenda uovu mkuu juu ya wanadamu walioumbwa kwa mfano wa Mungu kwa sababu tu ya kutetea CCM na kusema kuwa itakaa madarakani Milele kama Mungu muumba wa Vyote! Uovu mkuu!!

Watu wakajiona kukaa ndani ya CCM ni kuwa salama kuliko kukaa ndani ya Mungu hata wale waliojiita manabii na mitume na maaskofu feki waliofundisha kuwa ukiwa ndani ya Yesu una ulinzi wakageuka na kutafuta ulinzi na amani yao kwa mwanadam na chama cha mapinduzi ikawa ndiyo ngao yao ili waweze kueneza injili . Yaani Bila kuunga mkono juhudi hata dini zilitishiwa kufutiliwa mbali na kulipishwa kodi walizokua wanadaiwa. Sikuwa nafahamu kuwa dini nazo zinalipa ada kwa watawala ili wapewe kibali cha kumtangaza Mwenye Dunia yaani Mungu. Mungu anapewa masharti ya kukanyaga Tanzania. Uovu mkuu!!

Mungu akabadili ndimi zao kuelekea kwenye Tanzania mpya kwa kuanza safari ya kuiangusha CCM ,ambayo ndiyo Babiloni mkuu kwa Tanzania. Katibu mkuu Komredi Kinana wakati huo akawa hapendezwi na Matumizi ya nguvu ktk siasa. Akaomba kustaafu akakubaliwa.
Akateuliwa Bashiru Ally mkereketwa wa Upinzani kuwa katibu Mkuu wa CCM. MTU ambaye hajawahi kuipenda CCM na dhulma zake na wizi wake wa kura na uonevu wake ,ghafla akawa katibu mkuu na akageuka kuitumikia katika misingi yake ya uovu. Bashiru aliyeamini katika haki kwa miaka mingi ghafla akageuka kuwa msimamozi wa dhulma na siasa chafu za kuhujumu watu kwa kutaifisha Mali zao. Yeye anapata Mapesa mengi kwa kuunga mkono dhulma anasahau kuwa wengine wamepata Mali kwa kujinyima na hata kulala mitaroni na kwenye mapango wakisaka Mali ili waendeshe maisha yao na familia zao. Yeye Bashiru anakuja kuwanyanganya mali zao ili watoto wake waishi maisha mazuri kwa kumfurahisha MTU mmoja na familia yake. Uovu mkubwa.

Akateuliwa Hamfrey Polepole kuwa msemaji mkuu wa CCM. MTU ambaye alipigania Katiba mpya na mfumo wa bora wa uongozi unaopunguza madaraka ya Rais kuteua kila MTU mwenye nafasi ya juu katika kufaidi keki ya taifa. Mfumo mbaya unaoweza kutuletea dikteta kwenye utawala. Hamfrey akabadilika na kujiunga na uovu wa CCM bila kujali Damu ya Dr.Sengondo Mvungi iliyomwagwa na majambazi kutokana na msimamo wake wa Kutetea katiba mpya. R.I.P Dr. Sengondo Mvungi( uliowaachia Jukumu LA kudai Katiba mpya wamerejea walikotoka kulinda Mali zao walizochuma kutokana na pesa walizopata wakati wa mchakato wa Katiba mpya)
Polepole akawaasi wa Tanzania kwa sabu ya kutetea tumbo lake akajiunga na misimamo ya Dhulma ya chama cha mapinduzi. Akaendesha siasa za Rushwa ya madaraka na ubabe wa kila namna huku akiwatisha wakurugenzi. Uovu mkuu!!

Wakaja wakina Kitilia Mkumbo ,Kabudi , Kafulila na wengine wakapewa nafasi ya kuongoza mapambano ya kuhakikisha haki na usawa katika Taifa hili vinafutika ili CCM iendelee kulinda makada wake waliopora Mali za Taifa hili kuanzia vyama vya ushirika ,viwanda ,nyumba za serikali, mashirika ya umma n.k . na Nchi ikawa kama kuku aliyenyonyolewa manyoya yote wakati wa Baridi na kuwekwa kwenye nyumba yenye A.C kwa kuaminishwa kuwa nyumba bora ni yenye A.C. na ndio maendeleo.

Mbunge wa Moshi kwa miaka Mingi akafariki ghafla mtu aliyekua nguzo kuu ya upinzani hasa Chadema. Bilionea aliyekua na mali zake bila kuonea mtu. Wasiwasi ukatujaa kuwa ni kwa nini CCM na serikali yake walizuia kwa nguvu kubwa sana Wanachama na wabunge wenzake Wasiuage Mwili wa marehemu Ndesamburo kwenye uwanja wa mashujaa pale Moshi. Yaani CCM na watawala wake wakahamishia uovu wao kwa marehemu na kuweka pingamizi mpaka LA kuaga maiti asiye na kauli tena!! Uovu mkuu!! Hayo yote yaliganywa na CCM ikijiaminisha kuwa itatawala milele bila ridhaa ya wanadam zaidi ya ridhaa ya Risasi na mabomu. Wakasahau kuwa Mabomu na risasi ni vinatengenezwa na binadamu lakini Binadamu ameumbwa na Mungu. Hivyo binadamu ni lazima aheshimiwe kwanza.

CCM wakatangaza soko la wanasiasa wa upinzani wanaotaka kurudi CCM kwa Rushwa ya wazi na ahadi za vyeo.
Wwkatumia dhulma kuwapitisha mpaka wakapoteza maisha ya Akwilini bila kujali haki. Dhulma ikapiteza maisha ya mtoto wa maskini ili Walioshiba ndani ya CCM wazidi kushiba ! Uovu mkuu!!

Wapinzani Maslahi wakakimbilia vyeo na ubunge wa Dhulma kule CCM.

Hofu ikatanda Nchi nzima. Kila mtu akakaa kimya mbele ya kuwekwa ndani,kufilisiwa, kuuawa,kutekwa na kuteswa. Na kila aina ya uovu dhidi ya binadamu. Wabunge na bunge lao wakafurahia maisha hayo ya kudhulumu wapinzani ili wao waendelee kubaki Bungeni. Majaji wakafurahia teuzi na maslahi yao wanayopata wakajitenga na haki na kukaa upande wa Dhulma hata walipoambiwa wahukumu kesi ya Tume huru ili uchaguzo uwe huru na haki wakatupilia mbali na kutangaza kuwa tume ipo huru.Wakajiunga na dhulma ili wapate raha na familia zao kupitia mpango wa CCM wa kutawala milele pamoja na Mungu.
Uovu mkuu!!

Watu wasiojulikana wakaunga mkono juhudi kwa kumpiga Lisu Risasi. WanaCCM wakalipuka kwa Shangwe kwa kuona kuwa sasa hawana tena mpinzani Tanzania watatawala milele kama Mungu. Uovu mkuu!!

Mungu akaamua kusimama Mwenyewe ili aonyeshe kuwa yeye ndiye aliyewaumba wanadamu wote na hakuwapa Chama cha siasa Bali amri zake Kumi na sheria za haki. Haki haina Chama wala kabila. Mungu ni Mungu wa haki. Haki huinua Taifa. Mungu akamponya Lisu.
Lisu akarudi Tanzania . Njia ya kuifanya Tanzania mpya ikaanza kung'aa. Watu wakarejeshewa furaha mioyoni mwao. Nchi imelipuka kwa furaha , vyama vya siasa vimeanza kunawiri. Haki inaanza kuonekana itarejea.
Hofu imewageukia akina Bashiru. Wanawayawaya wanawatisha watu ,wanaogopa mahakama ya kimataifa inawanyemelea. Wametumia vibaya madaraka na mamlaka waliyoyapewa. Kama sio leo lakini kesho watavuna walichopanda. Heshima Polepole na Bashiru waliyojijengea kwa kupigania Haki na Katiba yenye misingi ya haki na utawala bora wameipoteza kwa sababu ya ubinafsi wa kuweka mtu mmoja mbele badala ya Taifa na vizazi vijavyo.

Mungu akaikinga Tanzania na Korona ili Uchaguzi ufanyike Tanzania mpya izaliwe .
Mungu alimtanguliza Yohana ili kuiandaa mioyo ya wa Tanzania kuwa kitu kimoja katika kuileta Tanzania Mpya yenye haki itakayowaunganisha wote bila kujali makabila na vyama na dini. Haki kila mtu anaitaka mana hakuna anayependa kudhulumiwa . Hata hao watu wa Tume wabaotumiwa na CCM kudhulumu watanzania kura zao hawapendi kudhulumiwa.
.
Tanzania mpya inakuja.
Watanzania wote tumchague Lisu ili tuachane na Tanzania ile ya dhulma na kutishana ,kuoneana ,kufitiniana kwa sababu ya kujipendekeza, unafiki, kutekana ,kufilisi watu waliotafuta mali zao kutokana na chuki tu za kisiasa na kukomoana .

IPO wazi kabisa Endapo Mpinzani atapata kura nyingi na wabunge wengi atatangazwa.
Mfano Lisu akitangazwa siku hiyo hiyo dola lote linahamia kwake. Tume inakua huru na hakuna wa kuigusa. Bashiru hana ubavu wa kuzuia Mtu asitangazwe mana anaootangazwa Lisu kuwa Rais basi nguvu ya JPM inakua imepotea na Polepole anabaki kama mjumbe tu wa kamati ya Harusi.Ghafla Lisu ndio anakua na Power yote. Tukumbuke uongozi na madaraka ya kupitia kampeni na Uchaguzi unakuwa na watu nyuma yake ndani na nje ya vyombo vyote vya dola . Hofu ni pale watu wanapodhani kuwa mtu atakosa kura hivyo kumuunga mkono wazi wazi haiwezekani.

Watu wamchague Lisu kwa kura nyingi mana hata wale watu wa Tume wameapa kwa Mungu kutenda haki. Haki zao zipo kikatiba na Mungu ndiye anyeweza kuwalinda dhidi ya waovu kama alivyomlinda Lisu.
 
Back
Top Bottom