Billie
JF-Expert Member
- Aug 13, 2011
- 13,709
- 23,147
Hee! Yamekua hayo? Unafki wangu uko wapi mkuu? Kuhoji ama?
Huyo ndiye kiongozi mliyetuletea, tulieni amalize mihula yake miwili, tena wewe UKIWA Afisa wa Idara nyeti uliyeasi; bado ulishiriki kumnadi kwa udi na uvumba huku ukijua kuwa asingelifaa taifa.Kuna mtu kanitumia taarifa kuhusu yaliyojiri kwenye "msako wa dola" kwenye bureaux de change, nimebaki mdomo wazi.
Kilichofanywa na wahusika (inasemekana ni mchanganyiko wa polisi, wanajeshi na "watu waliovaa kiraia") sio cha kistaarabu. Kwa sababu hata kama kuna genuine concerns kuhusu maduka ya kubadilishia fedha za kigeni kuhujumu uchumi, lazima taratibu zifuatwe.
Presumption of innocence ni muhimu sana kwa sababu imagine mfanyabiashara mwadilifu anapovamiwa kama jambazi kisha ikabainika hakufanya kosa, kwanini huyu mtu asiichukie serikali/nchi yake na huenda kutamani kulipa kisasi huko mbeleni?
Maji hufuata mkondo. Magufuli anaamini kuwa hata mbu akitua kwenye korodani basi kitumike kifaru kumuangamiza. Unfortunately, mara zote matumizi ya nguvu bila akili huzaa matokeo hasi.
Twawajua vema polisi wetu. Hivi wakivamia duka la fedha za kigeni, kuna uwezekano wowote wa mwenye duka kutokutwa na hatia? I mean hawa wahuni wamebobea katika kubambikizia watu kesi sambamba na kupora mali za raia.
Ni rahisi kulaumu. Ni rahisi kushutumu. Ni rahisi kutukana. Lakini si lawama wala shutuma au matusi yanayoweza kuleta ufumbuzi wa tatizo. Tufike mahala tukubaliane kuwa Rais wetu anahitaji msaada. In fact mwenyewe amekuwa mahiri wa kuomba msaada wa sala/dua zenu. Something is seriously wrong with Jiwe. Na nina wasiwasi kuwa taifa litapofika mahala pa kuelewa hali halisi, itakuwa too late kurekebisha damage iliyokwishafanyika.
View attachment 1034210
Huwezi itofautisha ccm na dolaIkishamshinda itarekebishwa karne nzima. Tukifanikiwa kuondoa uzwazwa wa kuishabikia CCM tutafanikiwa.
Pili CCM ilazimishwe kuviachia vyombo vya Dola. Ibaki kuwa chama cha siasa
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi kutoka kwa huyo au hao waliovamia mpaka kwa jiwe, kuna ngazi ngapi hapo umeziruka? Iweje usianze kutupa lawama kwa ngazi ya juu ya hao waliokuja kuvamia bali utupe lawama juu kabisa? Si sawa kabisa
Kama ingekuwa kila madudu yanayofanywa na watendaji wa serikali ni maagizo kutoka juu kusingekuwepo na mlolongo wa wanaotumbuliwa, si kweli kwamba watendaji wote waliopo serikalini ni wapya, hapana wengine wapo tangu enzi hizooo, wakisubiri kustaafu, huenda uwezo wao wa kubadilika na kuendana na kasi iliyopo ni mdogo na hawawezi kuachia ngazi wenyewe, kwahiyo wamekuwa wakijifanyia mambo ndivyo sivyo, na ndio maana taarifa zikimfikia anachukua hatua stahiki. Tukilaumu pia Tusifu.Wanatii maagizo
Muda ule alikua anakula hela za kina kinana kwny Kampeni 2015 aliona wengine mafala.Naona wakati unatimia wa kila mtu kuona nia mbaya wa huyu mtu Kwa Taifa letu japokuwa mlitushambulia Sisi tulioona hili mapema kabisa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hujaguswa.Namuombea Raisi wetu atuvushe salama kipindi kigumu. We shall overcome by Dr Martin Luther jr
Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu...wewe ni team ulanzi!Aisee mdindifu nchi ili na imemshinda
Naona wakati unatimia wa kila mtu kuona nia mbaya wa huyu mtu Kwa Taifa letu japokuwa mlitushambulia Sisi tulioona hili mapema kabisa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo anapanda mahindi akitarajia avune korosho!!? Nia ya kuvuna korosho anayo lkn yeye anapanda mihogo ili aje avune Korosho!??"Ana Nia Mbaya", na Tanzania? Sidhani!
Mimi naona ni tatizo jingine, lakini sio 'kuwa na nia mbaya.'
Nadhani anatamani sana, kama tulivyo wengi wetu, kuiona Tanzania nzuri, yenye maendeleo, (utulivu,raia wenye mshikamano, n.k.).
Katika kuitafuta Tanzania ya namna hiyo, hapo ndipo anaposhindwa vibaya sana. Anadhani akivunja vunja yote tuliyokuwa nayo na kuanza anavyotaka yeye tutaifikia haraka kwenye Tanzania anayotamani kuiona!
Sasa changanya kuwa na nia hiyo na njia mbaya zinazotumika na udhaifu wa kibinaadam alionao kila mtu; hapo ndipo tunapoingia kwenye mchanganyiko huu usioeleweka tunaoushuhudia sasa hivi.
Kwa hiyo, "sio kuwa na Nia Mbaya" ndio inayomsukuma afanye haya yanayoonekana.
Mara ya mwisho kusikia utumbuaji ilikua lini?Kama ingekuwa kila madudu yanayofanywa na watendaji wa serikali ni maagizo kutoka juu kusingekuwepo na mlolongo wa wanaotumbuliwa, si kweli kwamba watendaji wote waliopo serikalini ni wapya, hapana wengine wapo tangu enzi hizooo, wakisubiri kustaafu, huenda uwezo wao wa kubadilika na kuendana na kasi iliyopo ni mdogo na hawawezi kuachia ngazi wenyewe, kwahiyo wamekuwa wakijifanyia mambo ndivyo sivyo, na ndio maana taarifa zikimfikia anachukua hatua stahiki. Tukilaumu pia Tusifu.