Hali si njema: Pengine Jiwe anahitaji dua/sala zaidi

Hali si njema: Pengine Jiwe anahitaji dua/sala zaidi

Kuna mtu kanitumia taarifa kuhusu yaliyojiri kwenye "msako wa dola" kwenye bureaux de change, nimebaki mdomo wazi.

Kilichofanywa na wahusika (inasemekana ni mchanganyiko wa polisi, wanajeshi na "watu waliovaa kiraia") sio cha kistaarabu. Kwa sababu hata kama kuna genuine concerns kuhusu maduka ya kubadilishia fedha za kigeni kuhujumu uchumi, lazima taratibu zifuatwe.

Presumption of innocence ni muhimu sana kwa sababu imagine mfanyabiashara mwadilifu anapovamiwa kama jambazi kisha ikabainika hakufanya kosa, kwanini huyu mtu asiichukie serikali/nchi yake na huenda kutamani kulipa kisasi huko mbeleni?

Maji hufuata mkondo. Magufuli anaamini kuwa hata mbu akitua kwenye korodani basi kitumike kifaru kumuangamiza. Unfortunately, mara zote matumizi ya nguvu bila akili huzaa matokeo hasi.

Twawajua vema polisi wetu. Hivi wakivamia duka la fedha za kigeni, kuna uwezekano wowote wa mwenye duka kutokutwa na hatia? I mean hawa wahuni wamebobea katika kubambikizia watu kesi sambamba na kupora mali za raia.

Ni rahisi kulaumu. Ni rahisi kushutumu. Ni rahisi kutukana. Lakini si lawama wala shutuma au matusi yanayoweza kuleta ufumbuzi wa tatizo. Tufike mahala tukubaliane kuwa Rais wetu anahitaji msaada. In fact mwenyewe amekuwa mahiri wa kuomba msaada wa sala/dua zenu. Something is seriously wrong with Jiwe. Na nina wasiwasi kuwa taifa litapofika mahala pa kuelewa hali halisi, itakuwa too late kurekebisha damage iliyokwishafanyika.

View attachment 1034210
Asante Mungu. Kura yangu haukwenda kwa mtu huyu. Moyo wangu una amani kwani mimi siyo chanzo cha mateso kwa watanzania. Asante mkuu wa majeshi.
 
Ukiingia kwenye mitandao post zinazoandikwa na watu utafikili nchi imefika mwisho yaani Kila siku wanatia watu uoga juu ya uongonzi uliopo lakini ukiwa mtaani maisha yanaenda,kiukweli ni Tanzania pekee ndio fedha za kigeni zinafanya matumizi kiholela nendeni South Africa muone wanavyodhibiti fedha za kigeni ni benki tu ndio sehemu ya kubadilishia fedha za kigeni kiukweli bureau de change baadhi hutumika kuiba fedha za kigeni na kutoroshwa. Na raisi tunashukuru amejua hilo japo kwa namna njia inayotumika inaweza kuwa sio nzuri kwa baadhi ya watu kiukweli hayo maduka hutumika kutorosha fedha za kigeni.Tena wengine huzipaki kwenye maiti wakati wakiwarudisha ndugu zao waliokufa nchini kurudi kwao acheni ujinga uchumi unajengwa kwa kuchukua hatua wataalamu wa Vita wanasema '"casuality are necessary ""
 
poleni watanzania wenzangu kwa kuletewa jiwe,mkuu jiwe hajui kuwa ukitenda kwa haki lazima Mungu atakubariki na utaona mambo chanya katika Maisha yako..hivyo hivyo ukifanya kinyume utaona matokeo yake...pride itakuua mkuu Rais na 2020 u step down...
 
Kuna mtu kanitumia taarifa kuhusu yaliyojiri kwenye "msako wa dola" kwenye bureaux de change, nimebaki mdomo wazi.

Kilichofanywa na wahusika (inasemekana ni mchanganyiko wa polisi, wanajeshi na "watu waliovaa kiraia") sio cha kistaarabu. Kwa sababu hata kama kuna genuine concerns kuhusu maduka ya kubadilishia fedha za kigeni kuhujumu uchumi, lazima taratibu zifuatwe.

Presumption of innocence ni muhimu sana kwa sababu imagine mfanyabiashara mwadilifu anapovamiwa kama jambazi kisha ikabainika hakufanya kosa, kwanini huyu mtu asiichukie serikali/nchi yake na huenda kutamani kulipa kisasi huko mbeleni?

Maji hufuata mkondo. Magufuli anaamini kuwa hata mbu akitua kwenye korodani basi kitumike kifaru kumuangamiza. Unfortunately, mara zote matumizi ya nguvu bila akili huzaa matokeo hasi.

Twawajua vema polisi wetu. Hivi wakivamia duka la fedha za kigeni, kuna uwezekano wowote wa mwenye duka kutokutwa na hatia? I mean hawa wahuni wamebobea katika kubambikizia watu kesi sambamba na kupora mali za raia.

Ni rahisi kulaumu. Ni rahisi kushutumu. Ni rahisi kutukana. Lakini si lawama wala shutuma au matusi yanayoweza kuleta ufumbuzi wa tatizo. Tufike mahala tukubaliane kuwa Rais wetu anahitaji msaada. In fact mwenyewe amekuwa mahiri wa kuomba msaada wa sala/dua zenu. Something is seriously wrong with Jiwe. Na nina wasiwasi kuwa taifa litapofika mahala pa kuelewa hali halisi, itakuwa too late kurekebisha damage iliyokwishafanyika.

View attachment 1034210
Mi Nina wasiwasi kuna intelligence agencies za nje,zikishirikiana na watu wetu,waliopo kwenye taasisi nyeti kama bunge,jeshini,ndani ya utumishi wa umma,wameamua Ku "destabilise" hii nchi.
Na hapa Namba moja peke yake,hawezi kufanya kitu,maana amezungukwa na wachumia tumbo watupu,.
Hata kwenye korosho,ametereza,lakini hata asingeingilia kati mchakato wa korosho,wakulima wangeendelea kupigwa tu,pesa ingeenda kwenye mifuko binafsi,hawa wanaolia sasa HV,wanatoa machozi ya mamba tu.
Kikwete,Mkapa,Mwinyi,msaidieni nchi inaenda pabaya,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumshukuru Mungu alishasema katiba siyo kipaumbele chake. Akiigusa tuandike maumivu ya karne.
 
Kwa hiyo wamezitoa kamera ili wasiumbuke kama lile tukio la clouds . unachukua pesa ya mtu bila kuihesabu si wizi huu utamrudishiaje ?
 
Sijui kwanini watu hawaoni hili jambo ambalo lipo wazi "HIKI KIJIJI KIMEFILISIKA"
Ya Ugiriki yanakuja soon. Nao walificha jipu la Tako mwisho wakashindwa Kukaa.
Subirini mpaka mishahara itakapoanza kuruka mwezi ndio akili zitawakaa sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mahali kwenye bandiko lako umekiri uwepo wa hujuma, hizo hujuma zinafanywa na kina nani , na kwa malengo gani, na je ni sahihi kuacha hizo hujuma ziendelee?? kama watanzania wazalendo tunatakiwa kufanya nini kwa hao wanaotuhujumu??
Zinafanywa na polisisiemu
 
Ukiingia kwenye mitandao post zinazoandikwa na watu utafikili nchi imefika mwisho yaani Kila siku wanatia watu uoga juu ya uongonzi uliopo lakini ukiwa mtaani maisha yanaenda,kiukweli ni Tanzania pekee ndio fedha za kigeni zinafanya matumizi kiholela nendeni South Africa muone wanavyodhibiti fedha za kigeni ni benki tu ndio sehemu ya kubadilishia fedha za kigeni kiukweli bureau de change baadhi hutumika kuiba fedha za kigeni na kutoroshwa. Na raisi tunashukuru amejua hilo japo kwa namna njia inayotumika inaweza kuwa sio nzuri kwa baadhi ya watu kiukweli hayo maduka hutumika kutorosha fedha za kigeni.Tena wengine huzipaki kwenye maiti wakati wakiwarudisha ndugu zao waliokufa nchini kurudi kwao acheni ujinga uchumi unajengwa kwa kuchukua hatua wataalamu wa Vita wanasema '"casuality are necessary ""
Mkuu umeishia darasa la ngapi?
 
Huyo ndiye kiongozi mliyetuletea, tulieni amalize mihula yake miwili, tena wewe UKIWA Afisa wa Idara nyeti uliyeasi; bado ulishiriki kumnadi kwa udi na uvumba huku ukijua kuwa asingelifaa taifa.
Nakushauri utulie uunge mkono juhudi, sisi huku nyumbani tumezoea hali ya dhuluma na uonevu, hatujui lini kutapambazuka.
.....nani kakwambia atatoka baada ya mihula miwili unadhani biashara ya binadamu aliyofanya unadhani aifanya kwa bahati mbaya? anaongeza praise team ili akilianzisha tutakaompinga tuwe wachache

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Ana Nia Mbaya", na Tanzania? Sidhani!

Mimi naona ni tatizo jingine, lakini sio 'kuwa na nia mbaya.'

Nadhani anatamani sana, kama tulivyo wengi wetu, kuiona Tanzania nzuri, yenye maendeleo, (utulivu,raia wenye mshikamano, n.k.).

Katika kuitafuta Tanzania ya namna hiyo, hapo ndipo anaposhindwa vibaya sana. Anadhani akivunja vunja yote tuliyokuwa nayo na kuanza anavyotaka yeye tutaifikia haraka kwenye Tanzania anayotamani kuiona!

Sasa changanya kuwa na nia hiyo na njia mbaya zinazotumika na udhaifu wa kibinaadam alionao kila mtu; hapo ndipo tunapoingia kwenye mchanganyiko huu usioeleweka tunaoushuhudia sasa hivi.

Kwa hiyo, "sio kuwa na Nia Mbaya" ndio inayomsukuma afanye haya yanayoonekana.
Inaweza kuwa kweli lkn kwanini hataki kusikia nakufuata ushauri zaidi ya yule aliemkasimu urais ambae nae hana la maana analojua zaidi ya uhalifu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wakati unapukiza kwa Lengo la kuchochea Moto na kunawakati unapuliza kupuliza joto lipungue.

Sasa tunapilize ili tupate matokeo gani?
 
Naona wakati unatimia wa kila mtu kuona nia mbaya wa huyu mtu Kwa Taifa letu japokuwa mlitushambulia Sisi tulioona hili mapema kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile

Kuna watu wene hikma na busara zao walisema kuwa Magufuli hakustahili kupewa Ikulu ya Magogoni hata kwa nyukta moja wakabezwa na kutukanwa sana...!Naona sasa wameanza kuelewa na bado sana......!pp
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom