Mzalendo_Mwandamizi
JF-Expert Member
- Dec 12, 2007
- 1,116
- 4,773
Kuna mtu kanitumia taarifa kuhusu yaliyojiri kwenye "msako wa dola" kwenye bureaux de change, nimebaki mdomo wazi.
Kilichofanywa na wahusika (inasemekana ni mchanganyiko wa polisi, wanajeshi na "watu waliovaa kiraia") sio cha kistaarabu. Kwa sababu hata kama kuna genuine concerns kuhusu maduka ya kubadilishia fedha za kigeni kuhujumu uchumi, lazima taratibu zifuatwe.
Presumption of innocence ni muhimu sana kwa sababu imagine mfanyabiashara mwadilifu anapovamiwa kama jambazi kisha ikabainika hakufanya kosa, kwanini huyu mtu asiichukie serikali/nchi yake na huenda kutamani kulipa kisasi huko mbeleni?
Maji hufuata mkondo. Magufuli anaamini kuwa hata mbu akitua kwenye korodani basi kitumike kifaru kumuangamiza. Unfortunately, mara zote matumizi ya nguvu bila akili huzaa matokeo hasi.
Twawajua vema polisi wetu. Hivi wakivamia duka la fedha za kigeni, kuna uwezekano wowote wa mwenye duka kutokutwa na hatia? I mean hawa wahuni wamebobea katika kubambikizia watu kesi sambamba na kupora mali za raia.
Ni rahisi kulaumu. Ni rahisi kushutumu. Ni rahisi kutukana. Lakini si lawama wala shutuma au matusi yanayoweza kuleta ufumbuzi wa tatizo. Tufike mahala tukubaliane kuwa Rais wetu anahitaji msaada. In fact mwenyewe amekuwa mahiri wa kuomba msaada wa sala/dua zenu. Something is seriously wrong with Jiwe. Na nina wasiwasi kuwa taifa litapofika mahala pa kuelewa hali halisi, itakuwa too late kurekebisha damage iliyokwishafanyika.