Muumbuaji
Member
- Aug 24, 2016
- 70
- 84
Asubuhi ya leo nimetoka kumuona mgonjwa katika wodi ya watoto waliovunjika mifupa iliyopo Muhimbili chini ya taasisi ya MOI. Nilichokikuta kinasikitisha sana, na nilichosimuliwa na wazazi/walezi wanaowatazama watoto hao kinasikitisha zaidi
Nilichoona:
Vitanda vyote 23 katika wodi A vina wagonjwa wawili wawili, yaani maana yake kuna wagonjwa 46. Ukubwa wa wodi kwa uzoefu wangu wa metric units, ni 6m x 18m = 108 sq. metres
Kwa lugha ya ujumla, chumba chenye eneo la mita za mraba 108 kinatumika kuwalaza watoto 46, na hapo bado waangalizi wao wanaoshinda nao, ambao nao wapo 46, kufanya jumla ya msongamano wa watu 92 ndani ya kaeneo hako! Hapo nimeamua kuneglect watu wanaofika na kuondoka kwa lengo la kuwaona wagonjwa, kama mimi. Hiyo ni hali ya population density ambayo niliiona kwa macho yangu
Nilichosimuliwa:
Mzazi wa mtoto niliyeenda kumuona pamoja na mzazi wa mtoto mwezie wanaoshea kitanda, wamenieleza jinsi huduma ya hovyo inavyotolewa. Daktari anapopita hamuangalii mgonjwa na kutumia utaalamu wake kujua hali yake, bali anamuuliza muangalizi kuwa mgonjwa anaendeleaje, chochote atakachosema muangalizi ndicho hicho daktari anaandika na kuondoka kwenda kitanda kingine!
Hana muda wa kuangalia kiungo cha mtoto kilichovunjika kinaendeleaje, bali anatumia maelezo ya muangalizi pekee, halafu wala hachanganyi utaalamu wake, anaandika na kuondoka. Dada wa pembeni akalalamika kuwa ameambiwa asaini document ambayo hajui inahusu nini, na kwa kutumia udhaifu wa uelewa wa watu wetu, daktari/muuguzi amemsainisha tu.
Watoto wamewekewa mawe yananing'inia tu, hawapewi dawa yoyote! Jamani hakuna siasa hapa, waliopo Dar waende wodi ya watoto waliovunjika viungo leo hii wakafanye mahojiano hata kwa siri siri, halafu waje tuone kama kuna kuongeza chumvi au ndio hali iliyopo!
Wito:
Serikali iachane na siasa katika afya za wanadamu wananchi wake. Wataalamu wanaposema kuna upungufu wa vifaa,rasilimali watu au miundombinu ya hospitali, hatua za kurekebisha zichukuliwe, au walau watu waambiwe ukweli ili wajipange na wagonjwa wao kukabiliana na hali ya hospitalini. Wagonjwa wanaposema kuna uzembe wa wafanyakazi, hatua zichukuliwe. Hakuna haja ya kubishana kwenye vyombo vya habari kuficha uovu
Karibuni Muhimbili wodi ya watoto waliovunjika viungo, nyuma ya wodi ya Sewa Haji
cc: HKigwangalla